Special Thread: Wauza TV aina zote kwa bei nzuri tuuziane hapa

Kuna matapeli maarufu kwenye mtandao wa Instagram, hii account yenye jina la zanzibar_electronics_og ni matapeli ambao ukiangalia utadhani ni wafanyabiashara wakubwa kulingana na followers, lakini hawa ni matapeli ambao hawana duka physically na wala hawana bidhaa yoyote, wanawaibia watu kwa kuwaahidi wafanye malipo na kisha watawatumia bidhaa zao, wamekua wanabadilibadili jina la kampuni, walijifanya wapo Darajani, Zanzibar ila kesi zilivokuwa nyingi sasa wamebadili wanadai duka lao lipo Chakechake Pemba, angalizo hakuna duka la electronics hapo kwenye sehemu. Tafadhali tusaidiane kuwaokoa ndugu zetu wasitapeliwe zaidi. Sambaza kwa wengine wengi. Ahsanteni sana.
 
Ninayo
HISENSE SMART TV 49INCH
MPYA KWENYE BOX NIMEVUNJA KIOO KWENYE USHUSHAJI... HAIJAWAHI KUTUMIKA NI MPYA
INA TATIZO LA KIOO TU

NJOO NA OFFER YAKO

 

Attachments

  • IMG_20210209_213020.jpg
    30 KB · Views: 3
Nahitaji smart tv bajeti yangu ni 500,000. Iwe star x au hisense. Npo Tarime mjini.
0762908352.
Note: iwe nchi 43
Mkuu kama una ndugu dar niconect nae aje aone HISENSE SMART TV 40INCH original from china hii ni used imekuna na mazaga mengine kwenye contena
Hii tv ni tofauti na HISENSE za kariakoo View attachment 1698753View attachment 1698754View attachment 1698758View attachment 1698755View attachment 1698756View attachment 1698757View attachment 1698760View attachment 1698761
 
Nahitaji kujua bei ya tcl inch 43 pamoja na Sony home threate ya watt 1000 yenye speak nne za kusimama
 
Nauza Android Tv mpya kabisa niliinunua kwa ajili ya matumizi yangu binafsi lakini imenipasa niiuze kutokana na matatizo. Ipo kwenye box, saiz ni inch 50, ina play store, ina bloetooth,,ina internal memory 12gb.... Ina risiti na warranty ya miaka 3 ... Nahitaji laki 9 .... Nipo Kinondoni studio 0746960666
 

Duh! Kweli nimeponea chupuchupu.. katika harakati zangu za kutafuta TV nilipata wazo la kuwacheki wanaofanya online delivery kwenye mtandao wa instagram, ndio nikakutana na hawa jamaa wanaojiita Zanzibar _electronics.

Nilivyoona followers wengi sikuwaza sana nikajua hawa ni wa uhakika!

Nikachukua namba zao zilizopo kwenye bio na kuwacheki moja kwa moja whatsapp.. wakawa wakinipa bei zao za TV tofauti tofauti.

Baadae nilipata kununua TV kwa mshkaji wangu kwa bei ya kishkaji na pesa nyingi ilibakia. Nikawa sina interest tena za kununua runinga.

Hawa jamaa wakawa wananikumbushia karibu kila siku.. “Vipi boss, lini utakuwa tayari ufanye malipo tukutumie mzigo mpaka ulipo?”

Nikawa nawapotezea tu kwa kuwa sikuwa na haja tena. Mpaka nafuta namba zao sikujua kabisa kama ni matapeli!

Hapa kweli nilichomoka!
 
Natafuta king'amuzi cha azam bila dish nina 50000/- cash niambie wapi ulipo nije kufata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…