LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mrusi mjanja, hapa ataingia kwa kigezo cha kusaidia watu wenye asili ya russia, hii vita mwishowe itapiganwa hapo hapo ukraine tu, hawa nato nao wakiingiza jeshi ni kwa ajili ya kuwasaidia ukraine kukomboa donetsk na luhask na sio kuishambulia ardhi ya russia, nae mrusi atafanya hivyo hivyo, akishinda mrusi basi hapo ndio kaishamega hayo maeneo, ila akishindwa basi ndio bai bai,asahau Ukraine, itajiunga NATO kwa jeuri kubwa.
 
Ukraine ni wapumbavu.

Wataoumia ni wao sio marekani wala urusi

Kimbembele cha kutaks kuwa huko NATO kitawaponza bora wabaki nyutro
 
[emoji16][emoji16][emoji16] Jumuia ya Umoja wa kimataifa itamuacha mrusi akotoe huo msaada!? Expecialy NATO !?
Kuna msaada kuutoa ni mpaka upate Access na unayempatia msaada. Hapo tunaweza kusema NATO wangemwekea Russia kauzibe.

Lakini msaada huu wanaotoa Warusi haukwepeki, maana ni Jirani. Ana access ya moja kwa moja na wahanga, ambao ni Raia wanaokimbia Vita. Tena Lugha zao zinafanana kwa kiasi kikubwa. Ni Ndugu kwa namna moja au nyingine.

USA na NATO wanaweza kupata wakati mgumu kuipatia Ukraine misaada ya kibinadamu kuliko ilivyo kwa Russia.

Ukraine hawezi kumkwepa Mrusi kimahusiano na kiushirikiano, labda ahame nchi.[emoji3][emoji3]
 
Take it from me, hakuna vita hapo!

Kwa watu wa dini wenye mioyo minyoofu, hiyo ni ishara kubwa sana kwamba sasa uovu wa wanadamu umefikia kikomo kama ilivyokuwa wakati wa Gharika na Sodoma na Gomora...

Umesema hakuna vita hapo, alafu inasema Mungu amesubiri muda mrefu sasa enough is enough!.

Nini kita tokea sasa kama enough is enough.
 
Ukraine yupo katika wakati mgumu sana pengine wanajuta kuwa katika eneo la kimkakati.

Aidha wachague vita wachakae,ama wakubali kuwa watumwa wa russia.

Ukraine Wakichagua vita basi ujue nchi itakuwa uwanja wa mapambano na tutaona miamba yote duniani ikionyesha war technology zake.
 
Kwa jinsi ilivyo its better akae na urusi atafute suluhu kuliko kuruhusu nchi yake kugeuka uwanja wa vita,
Malaki ya raia watapoteza maisha na miundombinu itaharibika na haitarudi kuwa kama zamani tena
 
Mkuu keshaingia sasa, waeleze US na NATO wamdunde
Hakuna sehemu NATO walisema wataingiza jeshi kupambana na Russia.

NATO walisema wataweka vikwazo,walichofanya ni kuisaidia Ukraine vifaa vya kijeshi na utalaamu na intelligentsia.

Ni ngumu jeshi la NATO kupigana na Russia kwa sababu Ukraine sio member ila ni rafiki tuu.

So ni jukumu la Ukraine kupigania ardhi yao.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Russia Kesha ingia Sasa , unalipi jipya !? Futa hii comment please .. then muachage kuifananisha Russia na vitu vya kijinga
Nani alisema Russia hata ingia? NATO wamekuwa clear kwamba Russian akiingia atakumbana na msururu wa vikwazo hakuna sehemu walisema wataingiza jeshi kupigana.

Mwenye wajibu wa kupigana ni Ukraine kwa sababu sio member wa NATO hakuna wanajeshi wa NATO wataenda mstari wa mbele labda kutoa usaidizi wa vifaa,tiba na pesa na mafunzo nothing else.

Kwa hiyo tunasubiria msururu wa vikwazo
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom