Historia iliyofichwa.
Je, wajua, Kyiv ilishawahi kuwa na nguvu kuliko Moscow?
Na kuna kipindi Ukraine na Marekani wakawa hawapatani?
Ngoja nikuletee kidogo hii historia na kukuelezea kwanini Rais wa Urusi ana hasira na Ukraine.
Tuanzie karne ya 9, kulikua na taifa linaitwa
Kievan Rus, hapa waliishi watu wanaoongea
Slavic na mji wa
Kyiv ndo ulikua mji wao. Kati ya mwaka 980 – 1015 taifa hili la
Kievan Rus liliongozwa na
Grand Prince Volodimer, kwa kirusi wanamitwa
Vladimir na kwa KiUkraine wanamitwa
Volodimer na haya ndo majina na maRais wan chi hizi 2 leo hii.
Sasa Urusi, Belarus na Ukraine wakakubalina kuhusiana na hili taifa wanaloongea Slavic. Yakawekwa mabadiliko makubwa sana na baada ya hapo Ukraine ikawa chini ya utawala wa Urusi. Katika miaka ya 1900 haya mataifa mawili yalikua chini ya Jamhuri ya uSoviet.
Urusi ikiwa ndo ya kwanza kwa kuwa yenye nguvu zaidi kati ya Jamhuri 15 za uSoviet na Ukraine Jamhuri ya pili kwa nguvu ndani ya Jamhuri za uSoviet.
Ikiwa na:
- Viwanda vya kutengeneza silaha za kijilinda.
- Aridhi kubwa ya kilimo.
- Ikimiliki wingi wa nyuklia za Jamhuri ya uSoviet.
Kipindi cha vita baridi Ukraine ilikuwa Archrival wa Marekani, nimekosa Kiswahili cha neon Archrival.
1991, Umoja wa Jamhuri za Kisovieti ukafa, Ukraine ikawa huru na Urusi pia.
Ukraine akarithi:
- 176 Intercontinental Ballistic Missiles
- 1,249 Nuclear warheads
- 44 Strategic bombers
- 700 Nucleat Tipped Cruise Missiles
- 2,000Tactical Nuclear Weapons
Lakini wakawapa Urusi mwaka 1994 kwa makubaliano ya kubadilishana ya kwamba Urusi iihakikishie Ukraine Ulinzi na Usalama na Urusi ikaahidi kuheshimu Ukraine Sovereignty. Hii ikapelekea kusainiwa kwa
THE BUDAPEST AGREEMENT signatories wakiwa Belarus UK, Kazakhstan, US na hao wahusika wawili.
Twenda sasa mwaka 2013
Viktor Yanukovych alikua ndo Rais wa Ukraine alionekana kuwa ni:
- Mpinga rushwa mkubwa kwanza
- Mtu asiyeyumbishwa kwa kile anamini kuwa ni sahihi (Heavy Handed)
- Lakini zaidi ya yote alikua ni wa Upande wa Urusi (Pro-Moscow)
Mwaka 2013 alikataa dili la biashara na Umaoja wa Ulaya, dili ambalo lingeleta mahusiano makubwa ya kibiasha lakini nyuma ya pazia haikua ivyo japo wananchi waliaminishwa ivyo. Ivyo ikamfanya Yanukovych kuchukua msaada wa $15 billion kutoka Urusi, watu wengi wa Ukraine wakaaminishwa na upinzani kwamba wameuzwa kwa Urusi, kwaiyo kukatokea machafuko na maandamano yaliyoitwa
EUROMAIDAN.
EURO kwa sababu maandamano yalihusu kutaka kujiunga upande wa Ulaya na
MAIDAN kwa sababu maandamano yalitokea
Kyiv Maidan, ambayo leo hii tunaifahamu kama
Independence Square. Hapa waandamanaji wakupiga kelele kumtaka Yanukovych kusaini dili la Ulaya ama Yanukovych aachie madaraka.
Urusi wakawa upande wa Rais Yanukovych na Ulaya ikawa upande wa waandamanaji.
Feb 2014 serikali ya Yanukovych ikadondoshwa na Rais kutolewa nje ya Ukraine na akakimbilia Urusi.
Sasa sio kila raia wa Ukraine alikua na furaha na jambo hili, wengi wa upande wa Mashariki ambao wanaongea lugha ya Kirusi walitaka Yanukovych abaki madarakani, alipoondolewa watu wachache walihisi kutokutendewa haki na upande wa pili Urusi ikawa imeshajawa na hasira kuhusu propaganda za watu wa Ulaya kutokana na kupoteza kibaraka wake pale Ukraine.
Sasa ili kuweka mambo sawa Moscow ikachukua Cremia, kwanini Cremia?
Cremia ni peninsula ambayo iko katika Black Sea, 1954 kiongozi wa Umoja wa Jamhuri za Kisoviti Nikita Khrushchev alitoa Cremia kwa Ukraine, aliwapatia Jamhuri ya Kisovieti ya Ukraine kutoka kwa Jamhuri ya Kisovieti ya Urusi,
why?
Khrushchev alifanya ivyo ili kutengeneza uhusiano wa kindugu kati ya watu Ukraine na Watu wa Urusi, wakati huo wote Ukraine na Urusi wakiwa ni sehemu ya Umoja wa Jamhrui za Kisovieti, kwaiyo kutolewa kwa Cremia kwa Ukraine haikuwa na maana sana kwa kipidni icho.
1991, Ukraine ikawa huru na Cremia ikaungana na kuwa Ukraine, hii peninsula ikapewa umuhimu kidogo:
Ikabaki kuwa ni base a jeshi la Urusi na Urusi ikaahidi kuiheshimu Cremia
Mawazo mengi ya Warusi wanaamini mpaka kesho Cremia haikutakiwa kuachwa ijiunge na Ukraine kipindi cha huku nyuma. Kwaiyo mwaka 2014 kibaraka wa Urusi alipoondilewa pale Ukraine kama Rais Urusi ikaamua kuichukua Cremia kwa kuchukua majengo ya serikali na mpaka kufikia mwezi wa 3 mwaka 2014 penisula nzima ya Cremia ikawa chini ya jeshi na ikafutaiwa na kura za maoni za kujiunga Urusi.
Je kura hii ya maoni ilikuwa harali? Jibu la swali hili linategemea unamuuliza nani?
- Ukimuuliza Putin, anasema kura ile ya maoni ilikuwa kwa ajili ya uhuru wa Cremia
- Kwa waliobaki USA na Ulaya waliona hili kama kuchukuliwa kwa nguvu kwa Cremia
Sasa baada ya hapa tatizo likahamia upande wa mashariki mwa Ukraine, Urusi ikaanza kuwapa misaada watu wanaotaka kujitenga na Ukraine tokea hapo, silaha na fedha, mpaka kufika July 17,2014 inadondoshwa ndege ya
Malasia Airlie Flight ikiwa ana watu 298 ambao wote walipoteza maisha, Majeshi ya Ukraine yakamua kutaka kuwaondoa waasi katika maeneo ya
Lugaskn na Donetsk.
Hapa waasi wakaanza kupoteza nguvu ivyo jeshi la Urusi likaingilia kati na kuanza kupambana upande wa waasi. Kilichofuata baada ya hapo ni mlolongo wa mazungumzo kati ya Urusi na Mataifa ya Ulaya, hii ikapelekea kuzaliwa kwa
MINSK AGREEMENTS mwaka
2014 ikiwa na makubali ya:
- Ceasefire
- Military withdrawal
- Election in rebel held areas
Sasa miaka 8 leo hii MINSK AGREEMENT imeachwa na hakuna anayefuatilia tena.
Ukraine inabaki kuwa ni nchi kubwa ukitoa Urusi, ina eneo la 603,550 SQ KM ikiwa na idadi ya watu 44 milioni na GDP ya $155.6 billion, Per Capital Income zaid ya $3,727.
Leo hii Ukraine imegawanyika kati ya Mashariki na Magharibi, ambapo upande wa Magharibi wanajiona wao ni wa Kiulaya Ulaya ziaidi na wa Mashariki wao wanajiona wako karibu zaidi ya Urusi na kuweza kusaidiwa kwa lolote. Magharibi wengi wanaongea Kiukraine na Upande wa Mashariki wengi wanaongea Kirusi. Magharibi wanawaona warusi kama wakorofi na upande wa Mashariki wao wanaona wamebeba historia yao ya Urusi. Ukraine itaendelea kuwa katika vita miaka nenda miaka rudi, wamekuwa wakipambana na waasi wa Luhansk na Donetsk kwa muda mrefu bila kusahau Donbas.
Mzozo wa sasa ni kwamba Putin hataki Ukraine ijiungwe na NATO.
Kuna mengi yamefichika hapa:
- Kuna Domestic Politics, Putin alipochukua Cremia ushawishi wake na nguvu ndani ya Urusi uliongezeka maradufu, karibia watu 9 kati ya 10 ndani ya Urusi waliona ni sawa kwa alichofanya.
- Kuichukua Cremia kulifanya Urusi ianze kunekana dunia tena kwamba imerudi
- Warusi wengi pia wanaona uhuru wa Ukraine ilikua ni kosa kubwa sana walifanya, ni kweli Ukraine ilitawaliwa na Urusi huko nyuma, kuthibitisha hili kwamba Ukraine ilikua chini ya Urusi angalia 1 kati ya 6 ya watu wa Ukraine lazima ana Urusi ndnai yake, 1 kati ya 3 ya watu wa Ukraine lazima aonee Kirusi kama lugha mama yake
- Kwaiyo Putin yuko sahihi anaposema kihostoria walikua wamoja.
Na kosa kubwa la Ukraine wao walikubali kuwa
Russified,
CATHERINE THE GEAT shipped russias nd to this part of the world, na shule zikaanza kufundisha kwa kutumia lgha ya Kirusi, mwaka 1800 lugaha ya KiUkraine ikafutwa rasmi. Mwaka 1930 Stalin akaafanya Ukraine ikumbwe na njaa na wengi wa raia wa Ukraine wakafariki kwa njaa na kasha eneo kujazwa na Warusi zaidi nan do mana mpaka leo hii uande wa Mashariki wa Ukraine una watu wanaoongea zaidi lugha ya kurusi kwa kuwa ilitengenezwa kuwa ivyo, upande huu wa Mashariki una Coal, Fertile Land na Chuma pia.
NCHI ZA SLAVIC, RUSSIA, UKRAINE, POLAND, CZECH REPUBLIC, BELARUS, SERBIA, BULGARIA, SLOVAKIA, CROATIA, BOSNIA & HERZIGOVINA, SLOVENIA, NORTH MACADONIA, MONTENEGRO.
HOLY RUS hiki kitu tutakiongelea siku nyingine.