LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Kwa jinsi ilivyo its better akae na urusi atafute suluhu kuliko kuruhusu nchi yake kugeuka uwanja wa vita,
Malaki ya raia watapoteza maisha na miundombinu itaharibika na haitarudi kuwa kama zamani tena

Kabisa, bora nusu shari kuliko shari kamili.
 
Nani alisema Russia hata ingia? NATO wamekuwa clear kwamba Russian akiingia atakumbana na msururu wa vikwazo hakuna sehemu walisema wataingiza jeshi kupigana.

Mwenye wajibu wa kupigana ni Ukraine kwa sababu sio member wa NATO hakuna wanajeshi wa NATO wataenda mstari wa mbele labda kutoa usaidizi wa vifaa,tiba na pesa na mafunzo nothing else.

Kwa hiyo tunasubiria msururu wa vikwazo
Gia angani
 
Nani alisema Russia hata ingia? NATO wamekuwa clear kwamba Russian akiingia atakumbana na msururu wa vikwazo hakuna sehemu walisema wataingiza jeshi kupigana.

Mwenye wajibu wa kupigana ni Ukraine kwa sababu sio member wa NATO hakuna wanajeshi wa NATO wataenda mstari wa mbele labda kutoa usaidizi wa vifaa,tiba na pesa na mafunzo nothing else.

Kwa hiyo tunasubiria msururu wa vikwazo
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] USA si walitoa mkwara kwamba wataipiga Russia au nilisikia vibaya ,, Anyway Russia Kama Russia sio nchi ya kutishiwa na vikwazo wamefika hapo walipofika leo baada ya kufanikiwa kuvishinda / kuvivuka vikawazo kibao walivyo wahi kuwekewa , pindi unapo mpa changamoto binaadamu mwenye akili timamu ndio unazidi kumpa njia ya kuja na best solution, so USA NA NATO imekula kwao tu wakubali Hilo [emoji16][emoji16]
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] USA si walitoa mkwara kwamba wataipiga Russia au nilisikia vibaya ,, Anyway Russia Kama Russia sio nchi ya kutishiwa na vikwazo wamefika hapo walipofika leo baada ya kufanikiwa kuvishinda / kuvivuka vikawazo kibao walivyo wahi kuwekewa , pindi unapo mpa changamoto binaadamu mwenye akili timamu ndio unazidi kumpa njia ya kuja na best solution, so USA NA NATO imekula kwao tu wakubali Hilo [emoji16][emoji16]
Wapi walipotoa huo mkwara,unaweza weka hapa link?
 
Russia asifikiri hii itakuwa ni Crimea nyingine na asifikiri akiivamia Ukraine dunia watabaki wamekaa tu kwenye fensi.

Ukraine lazima watapigana kuilinda nchi yao na mataifa marafiki hawatakuwa mbali nao ila shida itakuwa kwa Russia kwani madhara watakayopata uchumi wao utawapelekea kuwa The Banana Republic.
Kishaingia, nendeni Sasa mkapambane nae
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Umesema hakuna vita hapo, alafu inasema Mungu amesubiri muda mrefu sasa enough is enough!.

Nini kita tokea sasa kama enough is enough.
Nimesema: Kwa wanadini wenye mioyo minyoofu, wanajua vizuri sana kwamba hiyo ndiyo ishara ya mwisho kabisa.
Dunia hii iliumbwa, ina mwenyewe.

Imechafuliwa mno!(kumbuka Sodoma na Gomora). Mwenye Mali yake hataki uchafu. Anataka kuisafisha(kama wewe upangishe nyumba yako kwa nia nzuri, usafiri kama kwa miaka30 hivi, unarudi unakuta machangudoa watupu wamepangishwa na uliyempangisha)
Bila shaka utawaondoa hao watu!

By the way, tayari mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa USA na Urusi wanakutana kupanga siku ambayo Putin na Biden watakutana ili ku-shake hands peacefully!! I told you!
 
Nimesema: Kwa wanadini wenye mioyo minyoofu, wanajua vizuri sana kwamba hiyo ndiyo ishara ya mwisho kabisa...
Hahahaa hakuna kitakacho badilika hapo, vikwazo tayari vimesha wekwa na luhansk donesk tayari ni nchi kwa muda kidogo, baadae watajiunga na russia.
 
Putin anataka kurejesha Hali yake ya mipaka ya zamani kabla ya kuvunjika,anajikosha tuu.

Screenshot_20220222-185556.png


Screenshot_20220222-185850.png
 
Historia iliyofichwa.

Je, wajua, Kyiv ilishawahi kuwa na nguvu kuliko Moscow?

Na kuna kipindi Ukraine na Marekani wakawa hawapatani?

Ngoja nikuletee kidogo hii historia na kukuelezea kwanini Rais wa Urusi ana hasira na Ukraine.


Tuanzie karne ya 9, kulikua na taifa linaitwa Kievan Rus, hapa waliishi watu wanaoongea Slavic na mji wa Kyiv ndo ulikua mji wao. Kati ya mwaka 980 – 1015 taifa hili la Kievan Rus liliongozwa na Grand Prince Volodimer, kwa kirusi wanamitwa Vladimir na kwa KiUkraine wanamitwa Volodimer na haya ndo majina na maRais wan chi hizi 2 leo hii.

Sasa Urusi, Belarus na Ukraine wakakubalina kuhusiana na hili taifa wanaloongea Slavic. Yakawekwa mabadiliko makubwa sana na baada ya hapo Ukraine ikawa chini ya utawala wa Urusi. Katika miaka ya 1900 haya mataifa mawili yalikua chini ya Jamhuri ya uSoviet.

Urusi ikiwa ndo ya kwanza kwa kuwa yenye nguvu zaidi kati ya Jamhuri 15 za uSoviet na Ukraine Jamhuri ya pili kwa nguvu ndani ya Jamhuri za uSoviet.

Ikiwa na:

  • Viwanda vya kutengeneza silaha za kijilinda.
  • Aridhi kubwa ya kilimo.
  • Ikimiliki wingi wa nyuklia za Jamhuri ya uSoviet.
Kipindi cha vita baridi Ukraine ilikuwa Archrival wa Marekani, nimekosa Kiswahili cha neon Archrival.

1991, Umoja wa Jamhuri za Kisovieti ukafa, Ukraine ikawa huru na Urusi pia.

Ukraine akarithi:

  • 176 Intercontinental Ballistic Missiles
  • 1,249 Nuclear warheads
  • 44 Strategic bombers
  • 700 Nucleat Tipped Cruise Missiles
  • 2,000Tactical Nuclear Weapons
Lakini wakawapa Urusi mwaka 1994 kwa makubaliano ya kubadilishana ya kwamba Urusi iihakikishie Ukraine Ulinzi na Usalama na Urusi ikaahidi kuheshimu Ukraine Sovereignty. Hii ikapelekea kusainiwa kwa THE BUDAPEST AGREEMENT signatories wakiwa Belarus UK, Kazakhstan, US na hao wahusika wawili.

Twenda sasa mwaka 2013 Viktor Yanukovych alikua ndo Rais wa Ukraine alionekana kuwa ni:

  • Mpinga rushwa mkubwa kwanza
  • Mtu asiyeyumbishwa kwa kile anamini kuwa ni sahihi (Heavy Handed)
  • Lakini zaidi ya yote alikua ni wa Upande wa Urusi (Pro-Moscow)
Mwaka 2013 alikataa dili la biashara na Umaoja wa Ulaya, dili ambalo lingeleta mahusiano makubwa ya kibiasha lakini nyuma ya pazia haikua ivyo japo wananchi waliaminishwa ivyo. Ivyo ikamfanya Yanukovych kuchukua msaada wa $15 billion kutoka Urusi, watu wengi wa Ukraine wakaaminishwa na upinzani kwamba wameuzwa kwa Urusi, kwaiyo kukatokea machafuko na maandamano yaliyoitwa EUROMAIDAN.

EURO
kwa sababu maandamano yalihusu kutaka kujiunga upande wa Ulaya na MAIDAN kwa sababu maandamano yalitokea Kyiv Maidan, ambayo leo hii tunaifahamu kama Independence Square. Hapa waandamanaji wakupiga kelele kumtaka Yanukovych kusaini dili la Ulaya ama Yanukovych aachie madaraka.

Urusi wakawa upande wa Rais Yanukovych na Ulaya ikawa upande wa waandamanaji.

Feb 2014 serikali ya Yanukovych ikadondoshwa na Rais kutolewa nje ya Ukraine na akakimbilia Urusi.

Sasa sio kila raia wa Ukraine alikua na furaha na jambo hili, wengi wa upande wa Mashariki ambao wanaongea lugha ya Kirusi walitaka Yanukovych abaki madarakani, alipoondolewa watu wachache walihisi kutokutendewa haki na upande wa pili Urusi ikawa imeshajawa na hasira kuhusu propaganda za watu wa Ulaya kutokana na kupoteza kibaraka wake pale Ukraine.

Sasa ili kuweka mambo sawa Moscow ikachukua Cremia, kwanini Cremia?

Cremia ni peninsula ambayo iko katika Black Sea, 1954 kiongozi wa Umoja wa Jamhuri za Kisoviti Nikita Khrushchev alitoa Cremia kwa Ukraine, aliwapatia Jamhuri ya Kisovieti ya Ukraine kutoka kwa Jamhuri ya Kisovieti ya Urusi, why?

Khrushchev alifanya ivyo ili kutengeneza uhusiano wa kindugu kati ya watu Ukraine na Watu wa Urusi, wakati huo wote Ukraine na Urusi wakiwa ni sehemu ya Umoja wa Jamhrui za Kisovieti, kwaiyo kutolewa kwa Cremia kwa Ukraine haikuwa na maana sana kwa kipidni icho.

1991, Ukraine ikawa huru na Cremia ikaungana na kuwa Ukraine, hii peninsula ikapewa umuhimu kidogo:

Ikabaki kuwa ni base a jeshi la Urusi na Urusi ikaahidi kuiheshimu Cremia


Mawazo mengi ya Warusi wanaamini mpaka kesho Cremia haikutakiwa kuachwa ijiunge na Ukraine kipindi cha huku nyuma. Kwaiyo mwaka 2014 kibaraka wa Urusi alipoondilewa pale Ukraine kama Rais Urusi ikaamua kuichukua Cremia kwa kuchukua majengo ya serikali na mpaka kufikia mwezi wa 3 mwaka 2014 penisula nzima ya Cremia ikawa chini ya jeshi na ikafutaiwa na kura za maoni za kujiunga Urusi.

Je kura hii ya maoni ilikuwa harali? Jibu la swali hili linategemea unamuuliza nani?

  • Ukimuuliza Putin, anasema kura ile ya maoni ilikuwa kwa ajili ya uhuru wa Cremia
  • Kwa waliobaki USA na Ulaya waliona hili kama kuchukuliwa kwa nguvu kwa Cremia
Sasa baada ya hapa tatizo likahamia upande wa mashariki mwa Ukraine, Urusi ikaanza kuwapa misaada watu wanaotaka kujitenga na Ukraine tokea hapo, silaha na fedha, mpaka kufika July 17,2014 inadondoshwa ndege ya Malasia Airlie Flight ikiwa ana watu 298 ambao wote walipoteza maisha, Majeshi ya Ukraine yakamua kutaka kuwaondoa waasi katika maeneo ya Lugaskn na Donetsk.

Hapa waasi wakaanza kupoteza nguvu ivyo jeshi la Urusi likaingilia kati na kuanza kupambana upande wa waasi. Kilichofuata baada ya hapo ni mlolongo wa mazungumzo kati ya Urusi na Mataifa ya Ulaya, hii ikapelekea kuzaliwa kwa MINSK AGREEMENTS mwaka 2014 ikiwa na makubali ya:

  • Ceasefire
  • Military withdrawal
  • Election in rebel held areas
Sasa miaka 8 leo hii MINSK AGREEMENT imeachwa na hakuna anayefuatilia tena.

Ukraine inabaki kuwa ni nchi kubwa ukitoa Urusi, ina eneo la 603,550 SQ KM ikiwa na idadi ya watu 44 milioni na GDP ya $155.6 billion, Per Capital Income zaid ya $3,727.

Leo hii Ukraine imegawanyika kati ya Mashariki na Magharibi, ambapo upande wa Magharibi wanajiona wao ni wa Kiulaya Ulaya ziaidi na wa Mashariki wao wanajiona wako karibu zaidi ya Urusi na kuweza kusaidiwa kwa lolote. Magharibi wengi wanaongea Kiukraine na Upande wa Mashariki wengi wanaongea Kirusi. Magharibi wanawaona warusi kama wakorofi na upande wa Mashariki wao wanaona wamebeba historia yao ya Urusi. Ukraine itaendelea kuwa katika vita miaka nenda miaka rudi, wamekuwa wakipambana na waasi wa Luhansk na Donetsk kwa muda mrefu bila kusahau Donbas.

Mzozo wa sasa ni kwamba Putin hataki Ukraine ijiungwe na NATO.

Kuna mengi yamefichika hapa:

  • Kuna Domestic Politics, Putin alipochukua Cremia ushawishi wake na nguvu ndani ya Urusi uliongezeka maradufu, karibia watu 9 kati ya 10 ndani ya Urusi waliona ni sawa kwa alichofanya.
  • Kuichukua Cremia kulifanya Urusi ianze kunekana dunia tena kwamba imerudi
  • Warusi wengi pia wanaona uhuru wa Ukraine ilikua ni kosa kubwa sana walifanya, ni kweli Ukraine ilitawaliwa na Urusi huko nyuma, kuthibitisha hili kwamba Ukraine ilikua chini ya Urusi angalia 1 kati ya 6 ya watu wa Ukraine lazima ana Urusi ndnai yake, 1 kati ya 3 ya watu wa Ukraine lazima aonee Kirusi kama lugha mama yake
  • Kwaiyo Putin yuko sahihi anaposema kihostoria walikua wamoja.
Na kosa kubwa la Ukraine wao walikubali kuwa Russified, CATHERINE THE GEAT shipped russias nd to this part of the world, na shule zikaanza kufundisha kwa kutumia lgha ya Kirusi, mwaka 1800 lugaha ya KiUkraine ikafutwa rasmi. Mwaka 1930 Stalin akaafanya Ukraine ikumbwe na njaa na wengi wa raia wa Ukraine wakafariki kwa njaa na kasha eneo kujazwa na Warusi zaidi nan do mana mpaka leo hii uande wa Mashariki wa Ukraine una watu wanaoongea zaidi lugha ya kurusi kwa kuwa ilitengenezwa kuwa ivyo, upande huu wa Mashariki una Coal, Fertile Land na Chuma pia.

NCHI ZA SLAVIC, RUSSIA, UKRAINE, POLAND, CZECH REPUBLIC, BELARUS, SERBIA, BULGARIA, SLOVAKIA, CROATIA, BOSNIA & HERZIGOVINA, SLOVENIA, NORTH MACADONIA, MONTENEGRO.

HOLY RUS hiki kitu tutakiongelea siku nyingine.

Slavic_Countries_correct.png

 
Madai yake yame kataliwa na majeshi anarudisha home.

Nimepitia thread moja humu ya jana,,,tayari majeshi ya urusi yameshaingia, na tayari washazamia majimbo mawili Donetsk na luhansk kwa ajili ya kulinda amani
 
Back
Top Bottom