LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Russia waliwapa silaha watanzania vita ya Idi amini .Na warusi walisomesha watanzania wengi .Kwa hiyo Tanzania wapo loyal kwa mrusi
Usicho kielewa!
mrusi alitaka ku-balance ile vita kwa kuwauzia Uganda ndege vita na kutuuzia sisi unti aircraft misile!
Tuliishiwa heat seaking misile!; ndege za Uganda zikawa zinatamba hadi mchana Mwanza!
Kumwendea Mrusi atupe hizo silaha akadai hard cash au tuingie mikataba migumu!
Kukosa Hekima ya Nyerere kuiomba Algeria na Msumbiji na wakatupa Steller misile!; ile vita ingekuwa ya muda mrefu na kutuweka kwenye hali mbaya!
 
Haikuwa sahihi kuingia mpaka Uganda ili tumpindue.
 

Kwenye vita rais atajulikana je alipo?

Kwani hata Putin anajulikana alipo, sembuse Zelensky?
 
Okay sawa!
Kwahiyo solution ni kwenda kumpiga na kuiharibu nchi ya mwenzie!? Duh
Mwaka 1962 USA walipogundua kuwa USSR walikuwa wanaweka makombora ya nuklia nchini cuba, dunia ilisimama kwa muda wa karibia mwezi mmoja baada ya kutishia kukizamisha kisiwa chote cha cuba endapo mpango huo usingesitishwa. Sasa ebu fikiria kama USSR wasingesitisha huo mpango mambo yangekuwaje?
 
Usa vs vietnam (russia) wamarekan walikufa kama njugu....
Russia vs ukraine (nato).....
Kama kweli us na france wanajiandaa kuingilia kati hii ngoma Nafikiri kuna harufu ya WWIII
 
Acha ujinga huo. Vita ni mbaya. Waombee mema badala ya kufurahia kana kwamba ni Kariakoo derby
Kwan wao wanawaombea mnavyouana congo na sudan n maeneo mengine africa?? Mbona wao wako busy na issue zao..Mbona waafrika mnapenda kujifanya watu sanaa??afu huruma zenu zinawaumiza kila siku ila hamjifunzi tu.acha wauane acha na wao watoto wao wapate shida acha na wanawake zao wawe wakimbizi acha wafe na njaa kwan ni sisi ndio tumewaletea mabalaa hayo kama wao wanavyotusababishia sisi???
 
Acha uongo bwana, North Korea wana nini cha kusema ebu angalia South Korea au Japan kisha linganisha hivyo vitu unavyoongelea.

Tuongee tu ukweli bila ushabik, hiyo North Korea kama wasingekuwa na huo mfumo wa utawala walionao sasa leo hii wangekuwa wapi kiuchumi,

Acheni propaganda za kwenye vijiwe vya kahawa bwana.
 
Hilda Newton kama ni wewe kweli watake radhi wanaume na jamii nzima ya Watanzania

Kama mwanasiasa unayejinasibu umetukosea sana. Kwetu tulio waumini wa imani yake mwanaume ni heshma. Ukimdharau mwanaume umemdharau aliyempa mamlaka

Hilda unaweza kuwa sahihi kwa wanaume unaowajua wewe ila wengine ambao tuna wanaume wa shoka viongozi wetu, watoto wetu wa kiume, kaka zetu, waume zetu. baba zetu wakituhadithia walivyoenda vitani uganda umetukosea mno kuipigania nchi umetukosea sana




MUNGU Ibariki Tanzania
 
Kwa vile wewe sio mlengwa naona mods wameuacha uzi wako ujitegemee. Wengi uzi zetu zinaunganishwa na uzi za watu tusiowajua tena bila taarifa au matakwa ya mwenye uzi, kisa tu mod ana chuki binafsi na baadhi yetu. Lile swala la kupunguza comment na Likes ktk uzi zangu naona kidogo wamelipumzisha, sasa wamehamia kwenye kuhamisha uzi zangu kwa watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…