Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usicho kielewa!Russia waliwapa silaha watanzania vita ya Idi amini .Na warusi walisomesha watanzania wengi .Kwa hiyo Tanzania wapo loyal kwa mrusi
Hahah hahAtakua kwenye mahandaki ya Dubai wasituchoshe
Haikuwa sahihi kuingia mpaka Uganda ili tumpindue.Usicho kielewa!
mrusi alitaka ku-balance ile vita kwa kuwauzia Uganda ndege vita na kutuuzia sisi unti aircraft misile!
Tuliishiwa heat seaking misile!; ndege za Uganda zikawa zinatamba hadi mchana Mwanza!
Kumwendea Mrusi atupe hizo silaha akadai hard cash au tuingie mikataba migumu!
Kukosa Hekima ya Nyerere kuiomba Algeria na Msumbiji na wakatupa Steller misile!; ile vita ingekuwa ya muda mrefu na kutuweka kwenye hali mbaya!
ICBM-Intercontinental Ballistic Missile. Ni bomu lenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu yaani toka bara moja kwenda bara jingine. Mfano Canada, Amerika Kaskazini Canada hadi Zimbabwe, Afrika.
![]()
Rais Zelensky hajulikani aliko
Inaelezwa kwamba aliko Rais Zelensky ni suala lililowekwa siri baada ya mwenyewe kuwaambia viongozi wa Umoja wa Ulaya kwamba ni mtu wa kwanza katika orodha ya watu wanaolengwa na Urusi.
Japokuwa rais huyo ametoa pendekezo la kutaka mazungumzo na Urusi kuhusu madai muhimu yaliyotakiwa na Moscow, ambayo ni kuitaka Ukraine itangaze kuwa haina upande na itaaachana na dhamira yake ya kutaka kujiunga na NATO.
Urusi kwa upande wake imejibu pendekezo hilo ikisema iko tayari kutuma ujumbe wake nchini Belarus kuyazungumza hayo.
Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri: Mohammed Khelef
DW Kiswahili
Duh tuombe wayamalize tu vita so nzuri kwa wasio na hatia...
Putin anaranda randa mutaani MoscowKwenye vita rais atajulikana je alipo?
Kwani hata Putin anajulika alipo, sembuse Zelensky?
Asante mkuuICBM-Intercontinental Ballistic Missile. Ni bomu lenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu yaani toka bara moja kwenda bara jingine. Mfano Canada, Amerika Kaskazini Canada hadi Zimbabwe, Afrika.
Si Dr.Shika alikuwa anatokea Tanzania? Tunataka Russia apigwe.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kwani watAnzania mnatka apigwe Nani!?
Putin anaranda randa mutaani Moscow
Mwaka 1962 USA walipogundua kuwa USSR walikuwa wanaweka makombora ya nuklia nchini cuba, dunia ilisimama kwa muda wa karibia mwezi mmoja baada ya kutishia kukizamisha kisiwa chote cha cuba endapo mpango huo usingesitishwa. Sasa ebu fikiria kama USSR wasingesitisha huo mpango mambo yangekuwaje?Okay sawa!
Kwahiyo solution ni kwenda kumpiga na kuiharibu nchi ya mwenzie!? Duh
Mpango wa dunia ni kuwaacha Russia wapweke. Maisha yao yatakuwa magumu baada ya 'uyatima' wanaoandaliwa utakaposhika kasi.Nchi nyingi wame cancel Russians planes .
Kwan wao wanawaombea mnavyouana congo na sudan n maeneo mengine africa?? Mbona wao wako busy na issue zao..Mbona waafrika mnapenda kujifanya watu sanaa??afu huruma zenu zinawaumiza kila siku ila hamjifunzi tu.acha wauane acha na wao watoto wao wapate shida acha na wanawake zao wawe wakimbizi acha wafe na njaa kwan ni sisi ndio tumewaletea mabalaa hayo kama wao wanavyotusababishia sisi???Acha ujinga huo. Vita ni mbaya. Waombee mema badala ya kufurahia kana kwamba ni Kariakoo derby
Acha uongo bwana, North Korea wana nini cha kusema ebu angalia South Korea au Japan kisha linganisha hivyo vitu unavyoongelea.Ebu tuache kusikiliza propaganda za US, yaani nchi iwe na uwezo wa kutengeneza nyuklia na kuzi maintains, iweze kutengeneza silaha zake mwenyewe, magari na hata communications system yake na iweze ku survive vikwazo kwa miaka yote then useme Ina uchumi mbovu kulinganisha na nchi inayo export almost kila kitu!?
Unayo nyuma
Kwa vile wewe sio mlengwa naona mods wameuacha uzi wako ujitegemee. Wengi uzi zetu zinaunganishwa na uzi za watu tusiowajua tena bila taarifa au matakwa ya mwenye uzi, kisa tu mod ana chuki binafsi na baadhi yetu. Lile swala la kupunguza comment na Likes ktk uzi zangu naona kidogo wamelipumzisha, sasa wamehamia kwenye kuhamisha uzi zangu kwa watu wengine.URUSI NA UKRAINE;MGOGORO WA MTU NA MDOGO WAKE.
Leo 16:30pm 26/02/2022
Joseph Stalin kiongozi ambae aliifanya Soviet Union(USSR)kuwa na nguvu ya kivita,kiuchumi na kuogopwa duniani,aliunda Warsaw Pact kama muungano wa kiulinzi wa nchi za Ulaya Mashariki mwaka 1955 kama mpinzani wa NATO ambayo iliundwa mwaka 1949 ikiwa ni muungano wa nchi za Ulaya Magharibi .Soviet Union ilijumuisha Russia, Ukraine, Georgia, Belorussia, Uzbekistan, Armenia, Azerbaijan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Moldova, Turkmenistan, Tajikistan, Latvia,Vijana wa miaka ya 80 na 90 mnakumbuka enzi zetu za kupiga charter kwenye kuta "Wasoo" neno hilo lilitokana na nguvu na umaarufu wa iliyokuwa Warsaw Pact.
Warsaw Pact ilijumuisha Soviet Union, Albania, Poland, Czechoslovakia, Hungary, Bulgaria, Romania, and the German Democratic Republic,daima Soviet Union itawakumbuka malegendary V.I Lenin,Joseph Stalin,Nikita Krushchev,Boris Yeltsin na sasa Vladimir Putin,ndani ya Vladimir Putin nayaona mawazo na mitazamo ya Baba wa Soviet Union,Joseph Stalin ambae baada ya kuushinda Ufashisti akawa kiongozi pekee wa watu mwenye kuweza kutatua hatima ya mamilioni ya wananchi,
Kwa muda mfupi aliweza kuigeuza Soviet Union kutoka nchi ya uchumi wa kiwango cha tatu katika nguvu ya viwanda hadi kuwa nchi yenye nguvu kiviwanda,kiuchumi na kivita,
Kwa miongo kadhaa Kremlin imedai mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi zilivunja ahadi ya kutopanua Nato. Madai hayo yanarejelea mazungumzo ya mwaka 1990, kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James A. Baker na kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev,Lakini viongozi wa Magharibi hawakubaliani na kusema hakukuwa na mpango wowote rasmi kuhusu kutopanua Nato hadi Ulaya Mashariki zaidi na kwamba muungano huo unashikilia 'sera ya mlango wazi.' kulingana na Rais wa Urusi Vladimir Putin,ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato (kwa sasa haijatuma maombi ya uanachama), "italeta tishio zaidi kwa Urusi"
uwepo wa Ukraine katika muungano, na uwezekano wa kutumwa kwa makombora yoyote ya masafa marefu yenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi au mifumo ya ulinzi ya makombora, sawa na ile ya Poland na Romania, itakuwa suala la "mstari mwekundu" kwa Moscow.Je unadhani USA yuko tayari kuwekewa silaha nzito nzito na jeshi la kivita la URUSI kwenye nchi jirani kabisa na USA kama Canada,Cuba na Mexico,Ndivyo jinsi ilivyo kidunia kwa Urusi pia yuko sahihi kukataa na kujihami ni mojawapo ya kanuni bora sana za kiuongozi kwa nchi yoyote ile duniani.
Mnamo mwaka 2014, Urusi iliyafadhili kijeshi makundi ya vuguvugu Mashariki mwa Ukraine katika majimbo ya CRIMEA,DONBASS,DONETSK na LUHANSK ambayo wakazi wengi wa majimbo hayo wana asili ya Urusi na wanazungumza Kirusi kwa ufasaha,katika mapambano hayo,Majeshi ya waasi kwa msaada wa Urusi walifanikiwa kuyateka majimbo hayo kutoka kwenye mikono ya Serikali ya Kyiv. Jimbo la CRIMEA liliamua kuitisha kura ya maoni (Referendum) ya kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.Majimbo mawili (Donestk na LUHANSK) yaliendeleza mapambano makali dhidi ya Majeshi ya Ukraine na kuchukua udhibiti KAMILI wa majimbo hayo. Katika Jimbo la DONBASS Majeshi ya Ukraine yalipambana Sana na hivyo waasi kushindwa kuliteka Jimbo Hilo kikamilifu.
Tarehe 24 Desemba 2021, Majeshi ya Urusi yalianza kuingiza mifumo ya Ulinzi wa Anga-ANT AIRCRAFT MISSILES (S-300 na S-400). Ujio wa Mifumo hiyo ya Ulinzi wa Anga ulisababisha DRONES za Ukraine kushindwa kufanya mashambulizi ya Anga. Hali hiyo ilitoa upenyo wa Majeshi ya Urusi na waasi kuchukua udhibiti upya wa majimbo ya DONBASS na LUHANSK,kutokana na Ukraine kutokuwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga (ANT-AIRCRAFT MISSILES) ya Uhakika, Basi Urusi ana nafasi ya kutumia ndege za kivita kushambulia Mifumo yote ya Ukraine ya kulipulia Vifaru Kabla ya vifaru hivyo kuanza kuingia kwenye Ardhi ya Ukraine kwa Urahisi zaidi,kutokana na Ukraine kulijua hili,imeamua kupeleka Mifumo yake ya kulipulia Vifaru karibu na mpaka wa Poland upande wa Magharibi. Makombora haya yanaweza kushambulia vifaru vyote vya Urusi ambavyo vitaingia Ukraine upande wa kaskazini wa Ukraine kutokea Belarus. Je,Urusi ataweza kushambulia kwa ndege za kivita Mifumo hii ya Ukraine ya kulipulia Vifaru ambavyo viko kwenye mpaka wa Poland? Jibu ni Hapana.
Kwasababu Marekani imeonya kwamba, endapo ndege za kivita za Urusi zitakaribia kwenye mipaka ya NATO(Poland ni Mwanachama wa NATO) Basi Marekani hatasita kuzitungua ndege Hizo. Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2017, ndege ya Kivita Ya Urusi iliyokuwa inafanya mission ya kuwashambulia waasi wa ISLAMIC STATE ilitunguliwa na Mifumo ya Anga ya Uturuki ilipokaribia Anga la Uturuki kwenye Mpaka wa Uturuki na Syria. Hili tukio liliharibu uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Uturuki na Urusi.
Kutokana na Uwezo mkubwa wa kijeshi wa Urusi ukilinganisha na Ukraine,bila Shaka Urusi itaibuka kidedea na kuyateka maeneo mengi ya Ukraine Kama itataka hivyo. Ushindi huo wa Urusi hautakuja kwa urahisi,Urusi inaweza kushuhudia kulipuliwa kwa vifaru vyake vingi ambavyo vitaingia kwenye ardhi ya Ukraine kuliko vifaru 140 ambavyo Urusi alivipoteza wakati wa Uvamizi wa nchi ya GEORGIA. Hii ni kutokana na Ukraine kupokea msaada wa Siraha za kulipua vifaru (ANT-TANK MISSILES) Zaidi ya Tani 80 kutoka Uingereza. Mwaka 2014 Ukraine haikuwa na Siraha hizi.
Urusi ilishaonya toka kitambo kwamba haitaruhusu kuona nguvu na ushawishi wa jumuia ya NATO inasogea karibu na mipaka yake,tujipe chemsha bongo kidogo,hivi Cuba pia si ni nchi huru ndugu zangu!?Je nini kilitokea pale Cuba alipotaka kumkaribisha Mrusi kujenga base ya kivita nyumbani kwake kwenye mji wake Mkuu wa Havana,Rais Kennedy akaenda Havana akabomoa kila kitu.
Huwezi ruhusu jirani yako awe na zana kali za kivita tena akisaidiwa na mpinzani wake mkuu kuzikusanya pamoja,Ukraine aondoe wazo lake la kujitanua kijeshi kwa mgongo wa NATO akisaidiwa na USA
La sivyo kaka ake wa Kwanza Russia atampiga kila siku.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.