LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mkuu naomba unipe mtazamo wako bila kuegemea upande maana ww ni mtu mwenye uelewa mkubwa sana hasa hasa kwenye nasuala ya kijeshi.

(1)hivi mkuu unadhani ni kwann Urusi imeamua kutumia njia hii ya kufanya ambush kwenye miji mingi kwa wakati mmoja? je hili halilipunguzi ufanisi?

(2)kuna coment moja nimesoma ulikuwa una sema ya kwamba wanajeshi wengi wa Urusi walio tumwa Ukraine si wazoefu wa vita, ni kweli kabisa hata mm hilo nimeliona maana wengi ni vijana wadogo ,sasa swali langu kwann atumie wanajeshi wasio na uzoefu wa kimapambano au ali idharau Ukraine?

(3)kwa kiasi kikubwa silaha nyingi anazo tumia Urusi ni za kizamani je kwann atumii silaha zake zenye uwezo wa hali ya juu ili ashinde vita haraka?

(4) Urusi inaonekana kupata kigugumizi kutumia nguvu hasa za angani una dhani ni kwann? Maana nakumbuka kipindi Urusi ana ishambulia Allepo yale mashambulizi yalikuwa makali sana ,Iwapo hayo mashambulizi angekuwa ana kumbana nayo Ukraine sidhani kama angeweza ingeweza kuhimili.

Mwisho mtazamo wangu inaonekana wanajeshi wengi wa Urusi sio wazuri kwenye mapigano ya mjini maana sehemu za wazi wamepita kirahisi ila mjini inaonekana wana sumbuka sana.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Ni ushabiki wa ajabu, Ukraine inabomobolewa halafu mtu anasema Urusi haimuezi Ukraine. Kitu ambacho nchi za magharibi na Marekani hazipendi ni vita ambayo Adui anao uwezo wa kupiga majengo ndani ya Nchi zao. Marekani na hata NATO wanaufahamu uwezo wa Russia, N.Korea na China kijeshi. Wanafahamu kuwa Russia haiko peke yake pia.
 
Marekani na nchi za magharibi zilishangazwa na uwezo wa Russia pale Syria kwa Bw Asad. Majeshi ya magharibi yalisambaratishwa kama watoto, baada ya pale kila nchi ikaomba kununua silaha na mifumo ya ulinzi kutoka Russia
 
Hadi sasa,ni miji gani ambayo Russia wanaweza sema wana control 100% kutokana na hii vita ukiacha kule Dombass na Crimea ambazo hazikuwa chini ya Ukraine wakati vita inaanza?...
Kharkov ambao ni mji wa pili kwa ukubwa uko chini ya majeshi ya Urusi hadi sasa baada ya mapigano ya usiku na leo asubuhi. Bado kuna pockets chache za Ukraine
 
Empty head unazani Usa akiingia kuna ambacho uyo basha wako ata fanya?? Ilo ni biti la mtu anae jua majibu amna nchi inayo ingia ingia tu vitani kwa sababu ya nchi nyingin
Huna unachojua, omba ufundishwe. Urusi ana resources nyingi sana ambazo sio tu Marekani anazihitaji na kuzitumia, ila nchi kibao ulimwenguni, ikiwemo gas na wheat. Urusi kingekua ni kinchi tu cha kawaida ambacho hakina nguvu Marekani angekua kashakipiga siku nyingi, akajimilikishe resources kama anavyofanya kwenye mafuta Uarabuni. Nini kinamzuia kwenda kupigana na Urusi? Anaishia kuweka vikwazo tu na kutoa msaada wa silaha. Urusi taifa kubwa kijana. Anaeona alililotoa Putin ni biti mbona maelekezo yapo wazi, aingie tu front kumsaidia Ukraine, majibu atayapata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasihi wasalimu amri, vinginevyo itailazimisha Urusi itumie silaha kubwa zaidi kuiharibu nchi na mahandaki walimojifisha
 
Nakwambia na amini kwamba USA hatopeleka JESHI kupigana na URUSI. BIDEN aliwahi kumwambia mwandishi wa habari. "URUSI SIO KIKUNDI CHA KIGAIDI, NI MOJA YA MAJESHI MAKUBWA DUNIANI. HIVYO KUINGIA VITANI NI KUBET NA LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA."
Marekani aende kupigana na urusi ili apate nini , tuanzie hapo kwanza
 
Angalie jinsi URUSI walivyo hatari. Hiki kipigo ni takatifu
Your browser is not able to display this video.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Marekani ana uchumi mkubwa, haya mwambie akavamie NORTH KOREA kama uchumi ndio unapigana. Uchumi ungekuwa unapigana USA asingekimbia AFIGHANSTAN. Akili unaziacha wapi wewe?
Sasa maisha ni vita tu au unahisi vikwazo vilivyowekwa ni vya kivita. Vikwazo vya kiuchumi, North Korea hana shobo na mtu na hayuko UN wala huwa hatoi tamko lolote lisilomuhusu. Usimletee kiherehere, vita wapigane Warusi alafu umtaje North Korea
 
Ukraine ishasema inapigana defensive war na silaha zote inazopewa ni defensive wala sio offensive. Ukraine haijaingia kuvamia Urusi wala haina uwezo huo.

Urusi mpaka sasa wana mji mmoja mkubwa wa Kharkiv ambao uko mpakani nao. Hapo watakuja wanasogea taratibu kwa sababu mji upo mpakani wanavusha supplies wanapiga kwa 'kuambukiza'. Hawana uwezo wa kupiga kwa stretching mpaka sasa, hawana flexibility.

Kwenye ramani: K- Kharkiv mpakani na Russia
C- mashambulizi kutoka Crimea
D- Donetsk na Luhansk regions
Hapo Kaskazini kutokea Belarus ndio wanapigana kuichukua Kyiv ambayo iko karibu tu na Belarus ila ndio concentration ya Ukraine ilipo.

Bila Russia kutumia Belarus sasa hivi tungekuwa tunawacheka. Haki ya Mungu hili sio jeshi la kukutana na vichaa kama Poland
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…