LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
⚡️ ‘We stand for peace - if they refuse talks, the responsibility will lie entirely with the Ukrainian side' - Head of Russian delegation in Belarus

Moscow’s delegation is waiting for a reply from Ukraine – Russia’s deadline for potential talks ends in one hour (15:00 MSK).

RT
Kwann Eukraine inakataa ofa ya mazungumzo?
 
Tukuache wewe na nani? Ukute hujui hata ubalozi wa Urusi ulipo hapa Tanzania. Unaleta mambo ya mpira ya "sisi Man U tumemnunua XXX"
Hao mabalozi wameoza ila lile jiwe kuu ndio ninalolitumainia toka enzi za Jesus na habari njema
 
Hhahaha..

Mwalimu Nyerere alisemaga upumbavu ni kipaji kuna watu wanazaliwa nacho..

Samahani kama nakukosea Hauna akili mkuu, wewe ni mpumbavu , shuleni watu kama nyie tulikuwa tunawaita shabiki mandazi..

Yani mtu kama wewe ukiwa shabiki wa Yanga unatasema Yanga ni bora kuliko Man city..
Putin amekuwa surprised na jinsi Ukraine walivyopambana kwa uhodari, vifaru vinaungua, vingine vipo abandoned, vijana wadogo wa Kirusi wanakuwa captured lazima awe frustrated.

Above all tunawaombea amani.
 
Jeshi la Marekani 60% yake huwa ni logistics. Vita haipiganwi na anayefyatua risasi mbele peke yake. Kabla yake kuna watu wengi mno wanaodharaulika machoni pa raia, kuna dereva aliyeleta silaha na atayeleta zikiisha (ndio hao wanaoshambuliwa mitaani na maroli yao hapo Kyiv). Kuna medic atakayetibu majeruhi, hawa ni muhimu kuliko anayepigana bila hawa utapoteza wanajeshi hata anayevuja damu mkononi tu na bila hawa hupati morali ya jeshi. Bado hawabebwi wakiumia au kufa, unakuta column ya Urusi inapita inakuta wanajeshi wake barabarani wamekufa au vifaru vimeungua. Marekani huwa inaenda na recovery vehicles kama Hercules kubeba kifaa kilichopigwa kukitoa machoni pa wanajeshi.

Urusi bado ina reli zote kwake na kwa Belarus inaweza zitumia ila ikikutana na kina Finland wenye airforce ya kujitutumua na last year wameagiza F-35s hizo railway facilities zitaharibiwa, mizigo ihamishwe kwenye reli ipite barabarani, columns za malori zipigwe ambush wanajeshi wapigane siku tatu bila supplies wapate njaa wajisalimishe au wafanye retreat. Hivihivi Finland ilipigana na USSR wakatoka kapa
Hongera kwa kuwa mjuvi mzuri wa mbinu za medani, mabeberu wana spy plane zinawakusanyia taarifa za ujasusi ambazo huchakatwa na military elites ambao huandaa mpango mkakati wa ku offense, wengi walitarajia mabeberu waingie in actual fighting bila behind the scene wanapelekeshana puta na putini. Umenikumbusha askari wa amin enzi za vita ya kagera walimdharau mkulima bibi kizee kilichowakuta kesho Simba battalion ikasambaratishwa
 
SmartSelect_20220227-142258_Twitter.jpg
 
Kwann Eukraine inakataa ofa ya mazungumzo?
Hajakataa kuzungumza, walikubaliana wakutane Belarus na Maafisa wa Urusi walishafika huko.. Ukrane wamegoma wanasema hatuweza kujadiliana kwenye nchi ambayo ipo upande wako hivyo itafutwe nchi nyingine isiyoegemea upande wowote.
 
Ndo kukataa boss. Kama anapigwa na anashindwa anatoa wapi kiburi cha kuchagua wapi pa kuzungumzia?
 
Hili swali tangu jana unaliuliza lakini Pro Russia hakuna anaethubutu kukujibu.
Ukraine wanasema Belarus hawako neutral wameruhusu Russia kurusha mizinga toka kwao kwa hiyo wako tayari mji wowote iwe Turkey, Baku au hata Warsaw sababu Belarus imechaguliwa na Russia sio wao wala Belarus. Ndio sababu kuu katoa Rais wa Ukraine kama saa moja lililopita.
 
Wizara ya Mambo ya Nje inataka mazungumzo yafanyike mjini Baku, Azerbaijan au Istanbul, Uturuki au Warsaw, Poland. Wamegoma kufanyia mazungumzo mjini Minsk ambako Belarus inatumika na Urusi kuvamia. Wakubaliane waache vita, maisha yaendelee ila Ukraine isikubaliwe kuingia NATO. Claims za Russia in military view zina mashiko, ila kiraia hazina. Hata US ingefanya hivihivi ila isingewekewa vikwazo.

Wizara ya ulinzi imetangaza kupokea air defence missiles sijui ni MANPADS, ground to air au ni air to air. Inashangaza kuona Urusi ilifeli kuangamiza kabisa jeshi la anga, hilo ndio suala la kwanza Marekani hufanya. Yani bora aachane na boots on ground kama hamiliki anga lako
Iraq alipigwa kwanza defence systems airports armoury. Afu ndio boots on the ground
 
Putin amekuwa surprised na jinsi Ukraine walivyopambana kwa uhodari, vifaru vinaungua, vingine vipo abandoned, vijana wadogo wa Kirusi wanakuwa captured lazima awe frustrated.

Above all tunawaombea amani.
Nusu ya magari ya Vita na vifaru vya Urusi vishateketea ,miundo mbinu imeharibiwa na Ukraine na pia wameshiwa na mafuta na kukimbia mziki ni wanaosupply silaha na mafuta za vifaru
 
Ndo kukataa boss. Kama anapigwa na anashindwa anatoa wapi kiburi cha kuchagua wapi pa kuzungumzia?
Wanasiasa wanatafuta mileage tu hawajali watu kufa kila mtu anatizama maslahi yake ndio maana hata yule Rais aliyepita wa Ukraine naye yuko huko barabarani kutafuta kick za kisiasa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ukraine wanasema Belarus hawako neutral wameruhusu Russia kurusha mizinga toka kwao kwa hiyo wako tayari mji wowote iwe Turkey, Baku au hata Warsaw sababu Belarus imechaguliwa na Russia sio wao wala Belarus. Ndio sababu kuu katoa Rais wa Ukraine kama saa moja lililopita.
Lakini ni ajabu kidogo. Au wewe unaonaje?
 
Back
Top Bottom