Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

1. Demilitalization inafanyikaje bila uvamizi ambao ndio wamefanya. Na inafanyikaje bila incapacitation of Ukrainian forces ambayo ndio unakataa eti hawana mpango wa kuiteka Ukraine. Bila kuiteka utadhibiti vipi jeshi lao na kuzuia counter offensive zao. Lazima uteke nchi majeshi yao yasisumbue ndio uwaambie cha kufanya na wafuate. Russia mpaka sasa siku 50 hana territorial gains za maana za kuonyesha.

2. Denazification ya Ukraine ni upuuzi. Wapi duniani uliona mashabiki wa Nazi wanavamiwa na jeshi la nchi nyingine. Tukitafuta Nazis Russia yenyewe tunawakuta. Nchi nyingine dunia hii zina Nazi sympathizers hata hiyo Israel yenyewe, dunia nzima haiwezi pigana kisa watu wachache mamia.

3. Helping Russian speakers in Donbass kivipi na Russia imevamia kutokea Belarus mpakani Kaskazini na kutokea Kusini miji ya Mariupol, wakati Russia speaking territories zipo Mashariki. Na isitoshe zipo under independent authorities zinazoshirikiana na Russia. Hapo si wangepeleka majeshi Donbass wakamaliza tena hapo wasingepata upinzani kutoka Ukraine.

Vipi ikifanyika 'helping Chechen speakers in Russian Federation'

4. Waizuie Ukraine kujiunga NATO wakati mkataba wao 1991 ulikuwa Russia kutoivamia Ukraine na Ukraine kuteketeza silaha za nyuklia. Mwaka 2014 Russia ilivamia Crimea, kisha ikavamia Donetsk na Luhansk. Sasa unazuiaje Ukraine kuamua inavyotaka.

Nadhani nishakujibu
Back and forth

1. Demilitarization
Labda haujui nini maana ya demilitarization. Unasema demilitarization ni mpaka uiteke nchi uiweke chini ya himaya yako!? Aisee!!!

Acc to encyclopedia of social and behavioral sciences
Demilitarization ni "dismantling or demobilization of a military, and the eventual destruction of military equipment, the destruction of weapons and explosives, and the incineration and destruction of chemical and biological weapons."

Hayo yote hayawezi kufikiwa mpaka kwanza uiteke nchi uiweke chini ya himaya yako!? Mnastaajabisha. Yaani kupiga makambi ya jeshi, kuharibu masilaha na miundombinu ya kijeshi ni mpaka uiteke kwanza nchi!?

2. Unasema hata Russia kuna manazi!? Unaweza kunitajia kitengo cha manazi kilichopo ndani ya jeshi la russia au serikalini!? Kuwepo na nazi mmoja au mia moja urusi sio shida, shida ni pale nchi kama nchi inawatambua na wanapewa nyadhifa mbali mbali jeshini na serikalini na wakifanya unyama kwa binadamu wengine wananyamaziwa.

Hii nimeipata wikipedia tu hapo
"The Azov Special Operations Detachment or Azov regiment or Azov battalion, is a neo-Nazi unit of the National Guard of Ukraine based in Mariupol in the coastal region of the Sea of Azov." Key word NEO-NAZI!

(Kama kipo kitengo kama cha Azov urusi au israeli au nchi yeyote nitafurahi ukikitaja.)

Hao ndio putin alikuwa na lengo la kuwafurumisha kutoka ukraine. Nadhani umejionea jinsi makao yao hapo mariupol yalivyodondokea mikononi mwa urusi. Mpk sasa mariupol ipo chini ya urusi. Baadhi ya makamanda wa Azov wameuawa na wengine wamekamatwa nafkiri baada ya vita watahukumiwa.

3. Jamaa unazingua. Unashughulishwa na petty issues sana. Sasa urusi kuvamia kutoka juu sijui chini ndio inahusiana vipi na Russia kuwasaidia warusi wa Ukraine!? Kwa hiyo ulitaka mpaka russia wapitie wapi ndio wawe wanatoa msaada kwa ndugu zao!? Kitendo tu cha kulipunguza nguvu jeshi la ukraine kupitia airstrikes na kuongezea fronts nyingine za vita ni relief kwa watu wa donbass. Mwanzoni ukraine walikuwa wanapigana na dpr na lpr tu sasa hivi wnapigana na jeshi pia la russia. Kwanza hiyo ya kuingilia juu na chini ni strategy tu ili walizunguke vizuri eneo la mshariki (donbass).

Russian forces are trying to encircle Ukraine's army in the east, moving in from the north, east and south. "This is a big territory to control, and I think we shouldn't underestimate the geographical complexities of this," says Tracey German, professor in conflict and security at King's College London.

Helping chechen speaking in RF, anayeweza na aende kuwasaidia [emoji1787]. Btw wachechen mbn wapo gudi urusi. Kadyrov ni lt gen wa jeshi la urusi. Sasa ukawasaidie kwani wanakufa kama wadonbass.

4. Ukraine haitajiunga NATO. haijalishi ni wanapangiwa au wanapnga wenyewe. Mikataba sijui agreements zitatajwa vifungu ibara na blah blah kibao ila bottom line Ukraine haitajiunga na NATO. ita uonevu au nini lkn ndio hivyo. Hilo lengo limetimia

"Ukraine’s president, Volodymyr Zelenskiy has acknowledged that Ukraine will not become a Nato member, in a significant concession on a day when Kyiv was pounded by Russian shells and missiles and the invading force tightened its grip on the capital."

Kwanza ulikiwa unapinga kwamba hayo sio malengo ya operation ya kijeshi inayofanywa na Russia huko Ukraine au!?




Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Additionally, mpaka sasa Zelensky is outshining Putin. Putin si alitaka regime change, iko wapi?
Putin anashindwa nini kumkamata Zelensky, ni kwamba hajaweza. Zelensky si anazurula mitaani Kyiv tena last time akiwa na Boris Johnson. Au unasema Russia wanafurahia vifaru vyao kupigwa, ndege na tena meli.

Bila kuiteka Ukraine hao Russia watafanyaje. Si imegoma kujisalimisha na kuweka silaha chini. The next kama Ukraine ingetekwa ni kumfungulia mashtaka Zelensky au kumuua na kubadilisha katiba ioneshe marufuku kujiunga NATO na kubadilisha serikali. Pro Russia wanajua hili waziwazi.

Kuitawala baada ya kuiteka si ni kuweka kibaraka. Hili haliumizi akili hata maana washafanya hivi before
Hayo ndio yalikuwa malengo Yao au unawasemea wewe?

Huyo Zelensky sio kibaraka wa west?

Special operation bado inaendelea na Mariupol inaanguka huko mikononi mwa Vikosi vya Urusi.

Regime change itawezekana tu, baada ya Urusi kutimiza malengo yake,
Yapi hata Mimi sijui

Kumbuka kwa mbinu zao za kivita wapo sahihi kipindi hiki kuliko mwanzo.
 
WW2 Wanazi hawakupigwa bure from nowhere. Walivamia nchi kuanzia Poland, France, UK, USSR na kushambulia misafara ya meli za Marekani ndio maana walipigwa. The same way na Russia alivyovamia Ukraine.

Nazi waliua Wayahudi na watu wengine kibao. Walifanya atrocities wakajenga concentration camps na machafu mengi, ila mara nyingi hawakuwa wezi kwa vile nchi yao ilikuwa inajiweza kiuchumi na haikuwa inajibrag bure kwahiyo hawakuwa washamba na vitu vya kigeni tofauti na hawa wanaoiba hata washing machines na magari.

Nazi kilikuwa chama tawala cha Ujerumani chenye jeshi, makao makuu, ofisi, wafanyakazi, maofisa na sera. Ukivamia unajua unaenda kupigana na nani na yuko wapi na una sababu za msingi nilizotaja.

Hasira za Urusi ni Nazis hao kuleta upinzani mkali kwenye war on Donbass, ndio fighters wenye spirit kubwa na wala hawako incorporated kwenye jeshi la Ukraine na hawapandishwi vyeo wala maslahi kama wanajeshi. Na kingine ni sababu tu za kuvamia zisizo na msingi. Kwani Ukraine jeshi lake ni Nazi, kwahiyo Russia akitokea mamia wavuta bangi basi tuseme nchi nzima mamilioni ni wavuta bangi.

Nazi Germany ilikuwepo since early 1930s na ikaisha 1945 baada ya kuvuruga usalama wa dunia. Nazi wa Ukraine wamefanya nini? Hata Ujerumani wapo Nazi sympathizers huwa wanafungwa magerezani kwahiyo Russia ivamie Ujerumani?
Acha upopoma komred,

Kikundi Gani kilifanya na kuratubu maidan revolution kule Ukraine?

Unajua kwa nini Zelensky alivyoingia madarakani alikuwa tofauti na huyu wa Leo?

Kwa neo Nazi na Manationalist wameikamata serikari pale kiev?

Kwa nini useme kikundi kidogo? Wakati ndio wenye sauti?
 
Inaonyesha hata ramani ya Ukraine yenyewe huijui komredi.

Mariupol kwa maelezo yako haipo Mashariki?

Kweli nimeamini kweli walifaa waliokuita mzee wa google, hata hili hujui?

Ukraine ni nchi iliyogawanyika kati ya Mashariki na Magharibi,

Ambapo Mashariki wamejaa hao Russia speaking na Ukrainians language huko Magharibi.

Mariupol ipo mashariki mpaka Odessa na ndio lengo la Urusi kwa Sasa.

Angalia hiyo ramani halafu useme google imenipeleka kushoto.
Halafu Crimea walipiga kura kuchagua ambao majority walitaka kujiunga na shirikisho la Urusi, acha uongo.
Lughansk na Donetsk walisema hawaitambui serikari iliyopo kiev na kuhold referendum.
Jinsi unavyoandika unaweza kuangalia ramani miaka bila kuona kitu. Odessa iko mashariki mwa Ukraine?? -- Tofauti kati ya juu na chini, kushoto na kulia kwenye ramani umeshasikia?
1650052785559.png

Menginevyo: Hadi sasa Putin aliamua kuua hasa Waukraine katika maeneo penye wasemaji wengi wa Kirusi.
Mji wa Kharkiv penye asilimia kubwa kidogo cha Waukraine wa Kirusi unajitetea kwa nguvu zote- ushirikiano wa wakazi wote.
Luhansk na Donetsk watu walipigia kura pro-Ukraine kabla ya kuvamiwa na Urusi - kila kitu baadaye mbele ya bunduki ya Warusi. Krimea labda (?) tofati - Donbass hapana.
 
Kabla ya kuinanga Urusi kushindwa vita ambavyo havijamaliza hata miezi miwili na wala havijaisha, inange Marekani kwanza aliyo iliyopigana kwa zaidi ya miaka 8 na nchi maskini kuliko hata Tz kipindi hicho ya Vietnam na kushindwa vibaya sana.

Huitaji kuvaa miwani kujua ya kwamba vita inakuwa ngumu kutokana na Ukraine kupokea silaha kutoka nchi magharibi tofauti na hapo hii vita ingekuwa imeisha zamani.
Hata Marekani kushindwa kwake Vietnam ni kutokana na Usoviet kuingilia vita kwa kuipatia silaha Vietnam kama ambavyo Marekani anafanya sasa hivi ndani ya Ukraine, tofati na hapo Marekani angeshinda vita pengine ndani ya mwezi tu.

Urusi iliikimbia Afghanistan kwa sababu ya Marekani kuwapatia mjahidini silaha na Marekani kaikimbia Afghanistan kwa sababu ya Urusi kuwapa Taribali silaha.


Ukifuatilia vita ya Iraq Urusi haikuingilia kabisa kwa sababu ilikuwa dhaifu na ilikuwa na hali mbaya sana kiuchumi Marekani alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na Iraq kutokuwa na msaada wowote kutoka nje.
Hata ukifuatilia vita ambavyo ameshinda Urusi ni ile ambayo Marekani haijaingilia.

Kwa hiyo msitake kuishusha sana Urusi maana kapigana vita nyingi na kashinda.
Urusi tunaishangaa kwa vile inapigana kutokea nyumbani inavuka mpaka wa ardhini, bado inatokea Donbass ambako ina umiliki na bado inatokea Belarus na misafara ya silaha.

Marekani ilienda Vietnam kwa kuandaa logistics kali za gharama, kuvuka majini na kupiga air drops za masafa marefu kwenye terrain wasiyo familiar nayo, weather tofauti na mazingira tofauti ambayo hata silaha zilikuwa zinafeli nyingine. Na huu uzi hatuzungumzii Marekani nyuzi zipo ambazo tulishasema udhaifu wa Marekani ilipoenda Vietnam.
Afghanistan Marekani haijatoka kwa kupigwa, imetoka kwa kukaa miaka 20 na hakuna hatma ya operation yao kwahiyo wakaona hakuna economic benefit wanapata na hakuna security threat watakuwa nayo endapo Taliban itarudi madarakani. Ukisoma objectives zao zilikuwa ni nini, ni kubadilisha regime, kuweka mpya na kuipa training. Yote wamefanya kwa miaka 20, kama walitoka ikabadilika hilo ni jambo lingine ambalo halikuwa kwenye objectives zao.

Marekani haijawahi pigana na jirani tangu karne ya 19. Russia sasa ndio analazimika kupigana nao. Russia yuko anapigana na jirani ambaye siri za jeshi karibia zote anajua, silaha nyingi anajua walitengeneza wote, ramani anazo, kambi na strategies baadhi wanajuana. Makamanda wa Russia na wa Ukraine wote kabla ya 1991 walikuwa wanatumikia jeshi moja, wengine walienda vyuo vilevile na wengine Russians waliwahi kuwa stationed Ukraine, na Ukrainians waliwahi kuwa stationed Russia. Yet, superpower hajapata gain ya maana. Hatushangai sana kutoipiga Ukraine, tunashangaa zaidi mpaka leo hakuna kilomita za mraba kadhaa za kuonyesha kwamba wameteka. Yani hata Mariupol uliopo mpakani ambao Ukraine inasuasua kupeleka reserve na supplies, wanajeshi hawajawa relieved ila bado superpower hajauteka completely
 
Hadi kufikia tareh 24 Feb media zao zote zilikuwa zikiwatambua kama Nazis ndani ya Ukraine, kiasi kwamba toka mwaka jana Japan alikuwa kaliweka hili kundi la Azov ndani ya list yao ya vikundi vya kigaidi duniani.

But any1 who fight with Russia kwenye sura za magharibi ni mtakatifu no matter iweje, That's why unaeza ona vyombo vya habari hivo hivo vikabadili jina kutoka Nazis hadi "Far right", Japan nae akawatoa kwenye list na ombi la radhi juu uku akiahidi haitojirudia.

Na hiyo utaona matukio ya kinyama yanayofanywa na Ukraine na hao Azov yakiwa Praised kwenye social network na vyombo vyao vya habari kama yule dada akimchinja POW wa Russia the same ISIS tactics ila hakisemwi kitu.

Anyway nikuache na maswali haya ya nyongeza...
1. Kwanini logo ya NATO ina resemble ile logo ya Nazi?

2. Kwanini jengo la NATO, pale makao makuu... Ukilizoom kutokea juu lina shape ya NAZI?

3. Kwanini war criminals wa kinazi wamekuja kuhodhi uongozi wa juu ndani ya NATO???
Ntawataja wachache ambao unaeza kuwatafta kamaa mfano tu
[emoji298]Adolf Heusinger from Nazi tena huyu alikuwa chief of Staff wa Hitler to the Chairman of NATO military committee...

[emoji298]Hans Speidel from Nazi General to Supreme Commander of NATO's Ground Force kwa Central Europe enzi hizo.

[emoji298]Johannes Steinhoff huyu mpaka alitunukiwa Knight Cross ya Iron Across ambayo ni Highest Nazi military award ya kipindi hicho ila nae akaja kusave as Chairman of NATO military committee!

[emoji298] Johann von Kielmansegg huyu General Staff officer wa kinazi akaja kua NATO's Commander in Chief of Allied Forces Central Europe...

Na wengineo kuendelea kuwataja ntaifanya kuwa ndefu.

4. Sasa unaeza kuitizama hiyo list ilivo ndefu na nafasi walizoshikiria ndani ya NATO na hakika itakupa walau ule mwangaza tu wakujua kwanini NATO wako after Russia.

Kwasabab wale kwa nafasi zao walizokuwa nazo ndani ya NAZI army na nafasi walizoshika ndani ya NATO sizani kama naeza kushawishika kua zile Ideology ziliishia uko uko... Bali zimeendelezwa kizazi na kizazi.

5. Kisha rudi kujiuliza mengine tena, haya makundi ya kinazi ndani ya Ukraine yamekuwa trained na Maafisa kutoka nchi zilizo Umoja wa NATO, Je kama Europe really wako against Nazi, ilikuaje wakawa wanawa-train kijeshi... Walikuwa wanatrain kijeshi wafuzu against nani baadae???

6. Itizame vizuri hii picha... View attachment 2188841Soma hayo maandishi Ajab ni kua, hiyo Logo iliyopo kifuani ya Nazi inafanana na Jengo lao la HQ... Je is it a coincidence? Designer ama architecture wa hilo jengo, logo yao... Kwamba Alifanya kwa bahati mbaya? View attachment 2188800
Pengine NATO/NAZI ndio hydra (joking [emoji1787])
Kwenye picha zao za holywood Captain America na Winter soldier nimeona habari kama hizi unazoziashiria hapa

Kwanza (hydra) walianza kama Nazi baadae wakaja kama S.H.I.E
L.D (nato)

"Cut off one head, two more shall take its place. Hail HYDRA!"


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Acha upopoma komred,

Kikundi Gani kilifanya na kuratubu maidan revolution kule Ukraine?

Unajua kwa nini Zelensky alivyoingia madarakani alikuwa tofauti na huyu wa Leo?

Kwa neo Nazi na Manationalist wameikamata serikari pale kiev?

Kwa nini useme kikundi kidogo? Wakati ndio wenye sauti?
Mapinduzi ya MAidan walifanya wananchi. Baadaye walikuwa na uchaguzi huru mara mbili.
Unajua matokeo?? Hapana hujui. Nikusaidie: Chama cha Svoboda (penye wafuasi wa itikadi wa Bandera) ilishuka nchini na chini hadi kufikia 2% pekee na mbunge 1 (mmoja). Wapi neonazi nje ya propaganda ya Urusi - na labda kati ya hizi asilimia 2??)
Onyesha mfano jinsi gani chama chenye asilimia 2 inakamata serikali??? Imekataliwa.
Tukijadili sehemu ya 2%: kwenye msingi gani unadai ni wengi au muhimu???
Eleza Bwana!
 
Putin alitaka regime change wapi!? Alikuambia!? Ushahidi!? Mbona mnapenda kuzusha!?
We unafikiri regime change ni mpaka uiteke nchi!? Yaani urisk maisha ya maelf ya wanajeshi wako na military infrastructures, eqps n tools kisa regime change, kweli!? Regime change inaweza kufanyika kirahisi tu kwa njia mbali mbali km coup, sabotaging elections, assassination, internal conflicts etc. etc. Sio lzm urisk vita huko ni kuua rungu kwa mende.

A matter of who outshines who is purely subjective. Kwako wewe putin amekuwa outshined na Zelensky. Your opinion. Kila mtu anajudge kivyake.
Kuzunguka kila mahali unaomba msaada, kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya mpinzani wako, maelf ya wanajeshi wako kujisalimisha kwa adui, kupoteza sehemu ya ardhi ya nchi yako, etc. Etc. That doesn't sound like shining to me!

Kuweka kibaraka mahali/nchi fulani ni lazima kwanza uiteke hiyo nchi!? Bagosha!!

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Kawaida yenu kukataa hata meli si mlisema imewaka moto. Sasa unabishana na wasuruhishi?
IMG_20220415_231350.jpg
 
Jinsi unavyoandika unaweza kuangalia ramani miaka bila kuona kitu. Odessa iko mashariki mwa Ukraine?? -- Tofauti kati ya juu na chini, kushoto na kulia kwenye ramani umeshasikia?
View attachment 2188914
Menginevyo: Hadi sasa Putin aliamua kuua hasa Waukraine katika maeneo penye wasemaji wengi wa Kirusi.
Mji wa Kharkiv penye asilimia kubwa kidogo cha Waukraine wa Kirusi unajitetea kwa nguvu zote- ushirikiano wa wakazi wote.
Luhansk na Donetsk watu walipigia kura pro-Ukraine kabla ya kuvamiwa na Urusi - kila kitu baadaye mbele ya bunduki ya Warusi. Krimea labda (?) tofati - Donbass hapana.
Ukikadiria ukubwa wa Ukraine kutoka kule Magharibi, hutaweza bisha au kukataa kuwa Bado Odessa ipo mashariki.

Sijajua unachobisha, lugha yao ni kirusi.
Screenshot_20220415-231540.jpg
FB_IMG_1645827449382.jpg
 
Kama ni kweli Ukraine wamepiga ile meli Ukraine itapigwa na kitu kizito kichwani ni kitu cha muda tu.

Hii itapelekea Russia kutumia nguvu zaidi au wanaweza kutoka kwenye OP mode wakaswitch kwenye War Mode.
Mrusi wa Mchambawima huyo
 
Mkuu kuna meli ya Marekani ilisha wahi kupingwa kombora na magaidi ikiwa pwani ya Yemen sema wao haikuwazama waliwahi kuzima moto ila iliharibiwa vibaya sana unazungumziaje hilo?

Haya mameli ya Marekani unayo yasifu kila siku drone za Iran huwa zinapaa juu ya hayo mameli na hayaoni chochote wana shutuka video inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiyaonesha hayo mameli yananyo fanya kazi mpaka Marekani ilirazimika kuipiga mkwara Iran ili iache hiyo tabia.
Kwahiyo video ya meli kuonekana kwenye mitandao ndio meli inaweza kupigwa. Ungejaribu kuhusisha rules of engagement usingeandika hiki. Mara kibao meli zinakuwa illuminated na hakuna issue inatokea. Kurekodi picha mbona Marekani wanafanya kwa satellites zao wanaonesha hata gari lako lililopaki sembuse meli, tena hapo wanatumia civilian satellites hizo za military hatuna access nazo.

Meli ya Marekani iliyopigwa na Yemens ilikuwa flagship? Hata Israel iliwahi shambuliwa meli yao na Hezbollah na haikuzama. Tofauti inakuja kwamba wale hawakujulikana kama wana anti ship missiles ila Ukraine ni taifa sio the so called magaidi. Na hizi Neptune AShM zilipozinduliwa mwaka jana Warusi walifanya analysis wakasema hamna kitu. There must be preparedness maana capabilities za adui zinajulikana fika, sasa kama preparation ndio ilikuwa hivi basi kuna tatizo
 
Back
Top Bottom