Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Back and forth

1. Demilitarization
Labda haujui nini maana ya demilitarization. Unasema demilitarization ni mpaka uiteke nchi uiweke chini ya himaya yako!? Aisee!!!

Acc to encyclopedia of social and behavioral sciences
Demilitarization ni "dismantling or demobilization of a military, and the eventual destruction of military equipment, the destruction of weapons and explosives, and the incineration and destruction of chemical and biological weapons."

Hayo yote hayawezi kufikiwa mpaka kwanza uiteke nchi uiweke chini ya himaya yako!? Mnastaajabisha. Yaani kupiga makambi ya jeshi, kuharibu masilaha na miundombinu ya kijeshi ni mpaka uiteke kwanza nchi!?

2. Unasema hata Russia kuna manazi!? Unaweza kunitajia kitengo cha manazi kilichopo ndani ya jeshi la russia au serikalini!? Kuwepo na nazi mmoja au mia moja urusi sio shida, shida ni pale nchi kama nchi inawatambua na wanapewa nyadhifa mbali mbali jeshini na serikalini na wakifanya unyama kwa binadamu wengine wananyamaziwa.

Hii nimeipata wikipedia tu hapo
"The Azov Special Operations Detachment or Azov regiment or Azov battalion, is a neo-Nazi unit of the National Guard of Ukraine based in Mariupol in the coastal region of the Sea of Azov." Key word NEO-NAZI!

(Kama kipo kitengo kama cha Azov urusi au israeli au nchi yeyote nitafurahi ukikitaja.)

Hao ndio putin alikuwa na lengo la kuwafurumisha kutoka ukraine. Nadhani umejionea jinsi makao yao hapo mariupol yalivyodondokea mikononi mwa urusi. Mpk sasa mariupol ipo chini ya urusi. Baadhi ya makamanda wa Azov wameuawa na wengine wamekamatwa nafkiri baada ya vita watahukumiwa.

3. Jamaa unazingua. Unashughulishwa na petty issues sana. Sasa urusi kuvamia kutoka juu sijui chini ndio inahusiana vipi na Russia kuwasaidia warusi wa Ukraine!? Kwa hiyo ulitaka mpaka russia wapitie wapi ndio wawe wanatoa msaada kwa ndugu zao!? Kitendo tu cha kulipunguza nguvu jeshi la ukraine kupitia airstrikes na kuongezea fronts nyingine za vita ni relief kwa watu wa donbass. Mwanzoni ukraine walikuwa wanapigana na dpr na lpr tu sasa hivi wnapigana na jeshi pia la russia. Kwanza hiyo ya kuingilia juu na chini ni strategy tu ili walizunguke vizuri eneo la mshariki (donbass).

Russian forces are trying to encircle Ukraine's army in the east, moving in from the north, east and south. "This is a big territory to control, and I think we shouldn't underestimate the geographical complexities of this," says Tracey German, professor in conflict and security at King's College London.

Helping chechen speaking in RF, anayeweza na aende kuwasaidia [emoji1787]. Btw wachechen mbn wapo gudi urusi. Kadyrov ni lt gen wa jeshi la urusi. Sasa ukawasaidie kwani wanakufa kama wadonbass.

4. Ukraine haitajiunga NATO. haijalishi ni wanapangiwa au wanapnga wenyewe. Mikataba sijui agreements zitatajwa vifungu ibara na blah blah kibao ila bottom line Ukraine haitajiunga na NATO. ita uonevu au nini lkn ndio hivyo. Hilo lengo limetimia

"Ukraine’s president, Volodymyr Zelenskiy has acknowledged that Ukraine will not become a Nato member, in a significant concession on a day when Kyiv was pounded by Russian shells and missiles and the invading force tightened its grip on the capital."

Kwanza ulikiwa unapinga kwamba hayo sio malengo ya operation ya kijeshi inayofanywa na Russia huko Ukraine au!?




Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hayo ndio yalikuwa malengo Yao au unawasemea wewe?

Huyo Zelensky sio kibaraka wa west?

Special operation bado inaendelea na Mariupol inaanguka huko mikononi mwa Vikosi vya Urusi.

Regime change itawezekana tu, baada ya Urusi kutimiza malengo yake,
Yapi hata Mimi sijui

Kumbuka kwa mbinu zao za kivita wapo sahihi kipindi hiki kuliko mwanzo.
 
Acha upopoma komred,

Kikundi Gani kilifanya na kuratubu maidan revolution kule Ukraine?

Unajua kwa nini Zelensky alivyoingia madarakani alikuwa tofauti na huyu wa Leo?

Kwa neo Nazi na Manationalist wameikamata serikari pale kiev?

Kwa nini useme kikundi kidogo? Wakati ndio wenye sauti?
 
Jinsi unavyoandika unaweza kuangalia ramani miaka bila kuona kitu. Odessa iko mashariki mwa Ukraine?? -- Tofauti kati ya juu na chini, kushoto na kulia kwenye ramani umeshasikia?

Menginevyo: Hadi sasa Putin aliamua kuua hasa Waukraine katika maeneo penye wasemaji wengi wa Kirusi.
Mji wa Kharkiv penye asilimia kubwa kidogo cha Waukraine wa Kirusi unajitetea kwa nguvu zote- ushirikiano wa wakazi wote.
Luhansk na Donetsk watu walipigia kura pro-Ukraine kabla ya kuvamiwa na Urusi - kila kitu baadaye mbele ya bunduki ya Warusi. Krimea labda (?) tofati - Donbass hapana.
 
Urusi tunaishangaa kwa vile inapigana kutokea nyumbani inavuka mpaka wa ardhini, bado inatokea Donbass ambako ina umiliki na bado inatokea Belarus na misafara ya silaha.

Marekani ilienda Vietnam kwa kuandaa logistics kali za gharama, kuvuka majini na kupiga air drops za masafa marefu kwenye terrain wasiyo familiar nayo, weather tofauti na mazingira tofauti ambayo hata silaha zilikuwa zinafeli nyingine. Na huu uzi hatuzungumzii Marekani nyuzi zipo ambazo tulishasema udhaifu wa Marekani ilipoenda Vietnam.
Afghanistan Marekani haijatoka kwa kupigwa, imetoka kwa kukaa miaka 20 na hakuna hatma ya operation yao kwahiyo wakaona hakuna economic benefit wanapata na hakuna security threat watakuwa nayo endapo Taliban itarudi madarakani. Ukisoma objectives zao zilikuwa ni nini, ni kubadilisha regime, kuweka mpya na kuipa training. Yote wamefanya kwa miaka 20, kama walitoka ikabadilika hilo ni jambo lingine ambalo halikuwa kwenye objectives zao.

Marekani haijawahi pigana na jirani tangu karne ya 19. Russia sasa ndio analazimika kupigana nao. Russia yuko anapigana na jirani ambaye siri za jeshi karibia zote anajua, silaha nyingi anajua walitengeneza wote, ramani anazo, kambi na strategies baadhi wanajuana. Makamanda wa Russia na wa Ukraine wote kabla ya 1991 walikuwa wanatumikia jeshi moja, wengine walienda vyuo vilevile na wengine Russians waliwahi kuwa stationed Ukraine, na Ukrainians waliwahi kuwa stationed Russia. Yet, superpower hajapata gain ya maana. Hatushangai sana kutoipiga Ukraine, tunashangaa zaidi mpaka leo hakuna kilomita za mraba kadhaa za kuonyesha kwamba wameteka. Yani hata Mariupol uliopo mpakani ambao Ukraine inasuasua kupeleka reserve na supplies, wanajeshi hawajawa relieved ila bado superpower hajauteka completely
 
Pengine NATO/NAZI ndio hydra (joking [emoji1787])
Kwenye picha zao za holywood Captain America na Winter soldier nimeona habari kama hizi unazoziashiria hapa

Kwanza (hydra) walianza kama Nazi baadae wakaja kama S.H.I.E
L.D (nato)

"Cut off one head, two more shall take its place. Hail HYDRA!"


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mapinduzi ya MAidan walifanya wananchi. Baadaye walikuwa na uchaguzi huru mara mbili.
Unajua matokeo?? Hapana hujui. Nikusaidie: Chama cha Svoboda (penye wafuasi wa itikadi wa Bandera) ilishuka nchini na chini hadi kufikia 2% pekee na mbunge 1 (mmoja). Wapi neonazi nje ya propaganda ya Urusi - na labda kati ya hizi asilimia 2??)
Onyesha mfano jinsi gani chama chenye asilimia 2 inakamata serikali??? Imekataliwa.
Tukijadili sehemu ya 2%: kwenye msingi gani unadai ni wengi au muhimu???
Eleza Bwana!
 
Kawaida yenu kukataa hata meli si mlisema imewaka moto. Sasa unabishana na wasuruhishi?
 
Ukikadiria ukubwa wa Ukraine kutoka kule Magharibi, hutaweza bisha au kukataa kuwa Bado Odessa ipo mashariki.

Sijajua unachobisha, lugha yao ni kirusi.
 
Kama ni kweli Ukraine wamepiga ile meli Ukraine itapigwa na kitu kizito kichwani ni kitu cha muda tu.

Hii itapelekea Russia kutumia nguvu zaidi au wanaweza kutoka kwenye OP mode wakaswitch kwenye War Mode.
Mrusi wa Mchambawima huyo
 
Kwahiyo video ya meli kuonekana kwenye mitandao ndio meli inaweza kupigwa. Ungejaribu kuhusisha rules of engagement usingeandika hiki. Mara kibao meli zinakuwa illuminated na hakuna issue inatokea. Kurekodi picha mbona Marekani wanafanya kwa satellites zao wanaonesha hata gari lako lililopaki sembuse meli, tena hapo wanatumia civilian satellites hizo za military hatuna access nazo.

Meli ya Marekani iliyopigwa na Yemens ilikuwa flagship? Hata Israel iliwahi shambuliwa meli yao na Hezbollah na haikuzama. Tofauti inakuja kwamba wale hawakujulikana kama wana anti ship missiles ila Ukraine ni taifa sio the so called magaidi. Na hizi Neptune AShM zilipozinduliwa mwaka jana Warusi walifanya analysis wakasema hamna kitu. There must be preparedness maana capabilities za adui zinajulikana fika, sasa kama preparation ndio ilikuwa hivi basi kuna tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…