Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Usipende kupotosha....maji shingoni ni Ukraine ambapo majeshi ya Russia yanasonga mbele huko Donbass ...ndiyo maana Kuna kikao kizito Cha nchi za NATO na EU huko ulaya...waziri wa ulinzi wa Ukraine naye amealikwa ...wamekutana kuhakikisha kuwa Russia inazuiwa kuichukua Donbass...you have to read news between the lines...Lavrov amesema hivyo kwa kuwa Sasa ni wazi Russia haipambani Tena na Ukraine Bali na NATO...na katika mazingira haya lolote linaweza kutokea likihusisha nuclear weapons...
 
Asante, ila naona tofauti ambayo si ndogo.
Kwanza sijapinga upanuzi wa himaya ya Urusi (kuna faida gani kupinga historia??) lakini ninasema: maarifa ya mataifa ya Ulaya na Urusi inatosha kuona kwamba wanaona Urusi kama tishio, na wana sababu nzuri.

Pili nilidokeza hali halisi kwamba Urusi ilipanusha himaya yake kwa njia ya vita na uvamizi wa kijeshi.

Tatu ninaona upanuzi wa NATO haikutokea kwa njia ya uvamizi wala vita bali kwa njia ya maazimio ya nchi zilizopata uhuru zikaamua vile kwa hiari yao.

Je unakubali nchi ina haki ya kuamua ushirikiano wake ya wengine au la? Je DRC ilikuwa na haki kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki? Je Sudan Kusini ilikuwa na haki hiyo??
Mataifa ya Ulaya pamoja Urusi yalikubaliana mwaka 1975 kila nchi ina haki kuchagua siasa yake. (Helsinki Accords)
 
Yanasogea kweli?? Hadi sasa hatujaona mabadiliko makubwa.
 
Hivi punde kuhusu mzozo wa Urusi na Ukraine
  • Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa anasukuma kwa suluhu nchini Ukraine
  • Vikosi vya Urusi vyakamata jengo la baraza la jiji la Kherson
  • Urusi inaitaka Marekani kuacha kuipatia Ukraine silaha
  • Rais wa Uturuki Erdogan asisitiza mchakato wa Istanbul katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa UNGuterres kumaliza mzozo wa Ukraine
xhtxs.cn/tY9
 
Aise, yaani ww! Naomba utuambie,nan muazilishi wa NATO?
 
Hawa watu usiangalie wanayosema, angalia wanayotenda, na kwa sasa wanayotenda ni kumshambulia Urusi ingawa mdomoni wanatamka wanaloona ni muhimu kutamkwa.
Wanakuwa kama watoto wadogo wanaodanganywa kununuliwa gari kisha anaachwa nyumbani,mzazi akirudi jioni mtoto hata hakumbuki tena kuulizia ahadi yake.Watu wanapeleka rundo la silaha kila kukicha bado unasema watajitoa NATO,hata Putin mwenyewe hii kauli ya 'watajitoa NATO hawezi kuiamini hata kidogo.
 
Nikiona jinsi gani marais wa nchi mbalimbali na sasa mawaziri wa Marekani wanaingia na kutoka Ukraine jinsi wanavyotaka, sioni kwamba jeshi la anga la Urusi linathibiti anga la Ukraine.
Nilisita kuamini taarifa kwamba marubani Warusi wanaogopa kuzura juu ya Ukraine kwa sababu bado kuna roketi za SAM ambazo walishindwa kuharibu (maana najua kila upande unasambaza propaganda yake).

Sasa Ujerumani iliamua kuimarisha ulinzi wa anga wa Ukraine kwa kutuma vifaru vyake vya Gepard ambazo zinalenga ndege na roketi.
Kwa hiyo uwezo wa Urusi kuendelea na mashambulio kutoka anga utategemea idadi ya roketi zake zilizobaki...
 
Aisee huko Ukraine kunawaka Moto saa hizi...Nchi 40 za NATO na EU zinakutana huko Uholanzi kujaribu kuokoa jahazi...fuatilieni manbo kwenye field..
[emoji3][emoji3][emoji3] tuko mwezi wa tatu sasa,hizi kauli zilishakuwa ni ngonjera tu
 
Wanajua kutumia media. Media kwao ni weapon.
 
Kumekucha wapendwa .

....haya wale ma pro NATO mko mtaa gani ....leo niko full full .....masnonda ...

Tsh....

NYAMIZI

Coco reborn

Mwanamkwiki sijui nimepatia hilo jina

bibie jonnah

naskia MOSCOW imezingirwa ..........[emoji3][emoji3][emoji3]

Alafu coco rebon wacha kukimbia vita ukae humu tukuoneshe namna warussia huwa hatupendagi ufamba....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…