RTI
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 2,422
- 7,173
Ww jamaa acha kutufanya mazuzu humu.Kwa Poland sidhani. Wameshajenga bandari kubwa la gesi kwenye pwani, pia wameshajenga bomba la gesi kwenda Norwei. Hawatakosa gesi.
Bulgaria sijui, nadhani huko Warusi wanalenga kutenganisha vyama vinavyobeba serikali. Tuone.
Ujerumani ambayo ilitegemea sana Warusi imeshapunguza mafuta ya Urusi kutoka asilimia 35 ya mahitaji yake kabla ya vita hadi asilimia 12 tu sasa, hadi mwisho wa mwaka wanataka kuiacha kabisa. Gesi bado, lakini hata kama Putin angesimamisha pia gesi ya Ujerumani wanayo akiba ili wadumu mwaka 1 na katika kipindi hiki wanaamini watapata mbadala.
Ila Putin atatafakari mara tatu kabla ya kuzamisha gesi ya Ujerumani maana hana mteja mbadala, mabomba ya kwenda China hayatoshi hata kidogo, mpaka kujenga atahitaji miaka , atapoteza pesa nyingi.
Maana umekuwa ukiongea mambo kana kwamba ww pekee ndio mfuatiaji wa mambo yanavyo enda duniani.
Nimesha kwambia na ninarudia kukwambia hayo maneno ya sijui kupuguza utegemezi wa mafuta na gesi ya Urusi ni ya kisiasa tu lakini kiuchumi haliwezekani kwa haraka kama ww unavyo taka kutuaminisha.
Mpaka sasa hakuna kiwango chochote cha mafuta kwenda kwenye nchi za magharibi kilicho pungua bali kimeongezeka zaidi ya aslimia 20.
Hiyo Poland unayo isema itaanza kulazimika kununu gesi ya Urusi kupitia nchi nyingine kama Ujerumani tena kwa bei kubwa.
Marekani kapiga marufuku mafuta ya Urusi lakini marufuku hiyo imebaki kwenye makaratasi tu ila utekelezaji wake umekuwa ni mgumu bado meli za mafuta ya Urusi linaendelea kutia nanga kwenye bandari za Marekani.