LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Usizidishe chumvi mzee
Mwisho wa siku ni Russia ataondoka ukrain kwa aibu
 
We unaongea nini kuna nchi yenye technologia na inteligencia kama Russia?

Teknolojia na Intelejensia kweli anavyo lakini sio kwa kiwango cha kushindana na wakubwa wenzie kama USA, UK , Israeli nk..

toka kuanguka kwa USSR, nguvu ya KGB ilipungua, uwezo wa kiteknolojia ulipungua kutokana na matatizo ya kiuchumi na mabadiriko ya siasa za kidunia... USSR enzi za kudai uhuru kwa mataifa ya Africa alikuwa na ushawishi sana Africa, Uarabuni na America ya kusini... maana mataifa mengi yaliamini kwenye ujamaa....Akili ya kibepari ilivyoingia kila mahala duniani Mrusi alipoteza ushawishi na baadala yake USA na allies wake wakakaa kila mahala..

Nguvu ya intelejensia ya Russia imebaki ndani ya mipaka ya Russia, wakati nguvu ya kiintelejensi ya USA ipo mpaka kwenye mdomo wa Russia..
 
Naacho omba ni Uncle Sam aingilie kati
Hawezi!

Kwa sababu kila mtu anajua consequences zitakazotokea. Njia pekee ambayo ni salama ni Ukraine akubaliane na masharti ya Mrusi, awe neutral.
 
Hivi alimaanisha nini kwenye mstari mwekundu
 
Katika vita yoyote majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kutakuwa na propaganda nyingi na uzushi mwingi sana wakati huu. Na watu watayasambaza bila kupata ushahidi wake. Mwisho wa siku ni kueneza uzushi kwa faida ya pande husika. Hii vita bado mbichi, ngoja tuone!
 
Huna lolote unalojua , aheri ukojoe ulale
 
Kuna mdau mmoja kasema PUTIN ana ule usela wa 80's 😂
 
Ukraine naye asidharauliwe jamani, hajawashangaza tu? Russia akitumia silaha kubwa za kuifuta Ukraine isiwepo hawezi kuachwa salama pia. Raia wake watamsumbua, Dunia itamsumbua na ikiwezekana anaweza uwawa na wenzake huko huko ambao hatakubaliana nao. Hii vita dunia inamuhurumia Ukrain, na Warusi wanamuhurumia Ukraine. Ni vita vya Puttin kwa ajili ya manufaa kijeshi si kijamii.
 
Kwa jinsi watu na mataifa mengi kupiga kelele kuhusu uonevu wa Russia , naona kamavile ile kauli kanafanya kazi ." SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU"

Mungu amesikia ndio maana Putin haamini kinachotokea.
 
Mji Mkuu upi huo ambapo Russia yupo? Embu nitajie Mji Mkubwa wowote wa Ukraine ulio under Russia controls
Maletopol ulitekwa jana na Russia.

Huo mji unao sema ya kwamba umelejeshwa kwa Ukraine bado hakuna udhibitisho hata BBC wameripoti hivyo ya kwamba hakuna udhibitisho wowote unao unesha ya kwamba mji huo umerudi Miko noni mwa Ukraine.

Hivi mna tumia vigezo gani mpaka mnasema eti Urusi kashindwa na Ukraine.

Urusi huko Ukraine hapambani na vilema bali anapambana na watu wenye mafunzo na silaha kama yeye kwahiyo usitegemee mteremko.
Kwa hiyo nyinyi mlitaka Ukraine itekwe kwa siku mbili tu ? Unadhani vita ni kucheza ngoma?

Ukraine ni suala la muda tu itatekwa na Russia, anacho fanya Ukraine ana jitutumua tu kama Saddam alivyo jitutumua kwa miezi miwili na propaganda kibao lakini mwisho wa siku USA ikaiteka Iraq.
Mpaka sasa zaidi ya asilia 60 ya wanajeshi waliokuwa mpakani bado hawajaingia vitani wenda hii ni mbinu ya Russia kutuma hicho kikosi cha kwanza kama chambo ili kulipunguza nguvu jeshi la Ukraine alafu badae afanye ambushi ya nguvu kumbwa.

Usitegemee Urusi kutoa wanajeshi wake kabla ya lengo lake kutimia.

Aidha Ukraine ikubali kujiondoa kwenye mchato wa kutafuta uanacha kwenye NATO aidha itekwe.





Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Kwa jinsi watu na mataifa mengi kupiga kelele kuhusu uonevu wa Russia , naona kamavile ile kauli kanafanya kazi ." SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU"

Mungu amesikia ndio maana Putin haamini kinachotokea.
UK imekiri kuwa imeisaidia Ukraine Silaha, Ujerumani imempatia Rockets lakini hawawezi kupeleka Troops zao kwasababu NATO wataingia na itasababisha vita kuu ya 3 ya dunia (WWIII)

Kwahiyo kwasasa Urusi haipigani na Ukraine peke yake.
 
Putin hakujiandaa na hii vita, amekurupuka tu, sidhani kama wamefanya tathmini sahihi kwenye muda na kila stage ya vita.
Sasa haya ni mawazo yako!
Wachambuzi wanasema Russia bado wanawahitaji raia wa Ukraine, ile nchi bado ipo na ni jirani yao na itabakia kuwa hivyo. Hakutakuwa na sababu ya kufanya uvamizi mkubwa kama alivyofanya Syria. Akifanya uvamizi wa namna hiyo atatengeneza adui mwengine mkubwa wa kizazi na kizazi ambaye ni jirani na ni mazingira hatari kwa usalama wa nchi ya Russia.

Kimkakati inambidi adili na wanajeshi tu baada ya amiri jeshi mkuu wa nchi ya Ukraine kukataa makubaliano waliyoyapendekeza. Na ndiyo maana akaanza na kupunguza nguvu ya jeshi la Ukraine kwa kushambulia base za kijeshi na maghala ya kuhifadhia silaha pamoja na viwanda vinavyojihusisha na utengenezaji wa silaha. Lengo no kupunguza nguvu za jeshi la Ukraine.

Operation inayofuata ndiyo hiyo ambayo anayoifanya sasa hivi na ni operation ngumu ambayo ni urban warfare. Ikiwa ni kuiondoa serikali ambayo kwake anaiona ni hatarishi. Kwa kuzuia uharibifu mkubwa wachambuzi wanasema ameingia na silaha za nyuma si za kisasa.
Urban warfare ni ngumu na ugumu wa hapa si kwamba Russia hana uzoefu. Ugumu wa hapa ni mnapambana kwenye makazi ya watu ambao ni raia, ambao sheria za kivita zinawalinda. Shambulio lolote dhidi yao ni uhalifu wa kivita kwa sababu umeshambulia wasiyostahiki. Na huu ni mtego kwa Russia, majeshi ya Ukraine yanajificha kwenye makazi/majengo ya makazi ya raia.
Kuna suala hapa umelisahau. Russia lengo la hii vita ni kulinda usalama wa nchi yake. Sote tunafahamu NATO ikiwa mlangoni kwake ni hatari. Ukraine pia inakuwa kijeshi ikiwa NATO na ikijijengea na uwezo wa kutengeneza mabomu ya nyuklia hatoweza kumdhibiti. NATO wanalijua hili na wanajua kuwa Ukraine ni kete muhimu dhidi ya Russia.

Naam; Ukraine ni nchi huru ina wajibu wa kufanya maamuzi yake lakini ni hatari kufanya maamuzi yatakayo hatarisha usalama wa nchi jirani yako. Russia anachofanya ni kumdhibiti Ukraine mapema. Ikiwa Russia mkakati huu utafeli wachambuzi wanasema itamlazimu alazimishe mazingira. Nayo ni kutunisha msuli wake. Akifanya hivyo maangamivu ya Syria miji kuwa gofu yatahamia Ukraine. Na Ukraine itaumia.

Russia inacheza mahesabu hapa! ni mahesabu yanayohitaji umakini wa hali ya juu. Atakayeumia zaidi ni Ukraine ikiwa akikaza msuli.
 
Kwani hao NATO na Marekani hawana Nuclear?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…