Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Ukraine ni nchi huru nayo ina haki ya kujilinda na Russia kama anaiona ni tishio kwake.Sasa haya ni mawazo yako!
Wachambuzi wanasema Russia bado wanawahitaji raia wa Ukraine, ile nchi bado ipo na ni jirani yao na itabakia kuwa hivyo. Hakutakuwa na sababu ya kufanya uvamizi mkubwa kama alivyofanya Syria. Akifanya uvamizi wa namna hiyo atatengeneza adui mwengine mkubwa wa kizazi na kizazi ambaye ni jirani na ni mazingira hatari kwa usalama wa nchi ya Russia.
Kimkakati inambidi adili na wanajeshi tu baada ya amiri jeshi mkuu wa nchi ya Ukraine kukataa makubaliano waliyoyapendekeza. Na ndiyo maana akaanza na kupunguza nguvu ya jeshi la Ukraine kwa kushambulia base za kijeshi na maghala ya kuhifadhia silaha pamoja na viwanda vinavyojihusisha na utengenezaji wa silaha. Lengo no kupunguza nguvu za jeshi la Ukraine.
Operation inayofuata ndiyo hiyo ambayo anayoifanya sasa hivi na ni operation ngumu ambayo ni urban warfare. Ikiwa ni kuiondoa serikali ambayo kwake anaiona ni hatarishi. Kwa kuzuia uharibifu mkubwa wachambuzi wanasema ameingia na silaha za nyuma si za kisasa.
Urban warfare ni ngumu na ugumu wa hapa si kwamba Russia hana uzoefu. Ugumu wa hapa ni mnapambana kwenye makazi ya watu ambao ni raia, ambao sheria za kivita zinawalinda. Shambulio lolote dhidi yao ni uhalifu wa kivita kwa sababu umeshambulia wasiyostahiki. Na huu ni mtego kwa Russia, majeshi ya Ukraine yanajificha kwenye makazi/majengo ya makazi ya raia.
Kuna suala hapa umelisahau. Russia lengo la hii vita ni kulinda usalama wa nchi yake. Sote tunafahamu NATO ikiwa mlangoni kwake ni hatari. Ukraine pia inakuwa kijeshi ikiwa NATO na ikijijengea na uwezo wa kutengeneza mabomu ya nyuklia hatoweza kumdhibiti. NATO wanalijua hili na wanajua kuwa Ukraine ni kete muhimu dhidi ya Russia.
Naam; Ukraine ni nchi huru ina wajibu wa kufanya maamuzi yake lakini ni hatari kufanya maamuzi yatakayo hatarisha usalama wa nchi jirani yako. Russia anachofanya ni kumdhibiti Ukraine mapema. Ikiwa Russia mkakati huu utafeli wachambuzi wanasema itamlazimu alazimishe mazingira. Nayo ni kutunisha msuli wake. Akifanya hivyo maangamivu ya Syria miji kuwa gofu yatahamia Ukraine. Na Ukraine itaumia.
Russia inacheza mahesabu hapa! ni mahesabu yanayohitaji umakini wa hali ya juu. Atakayeumia zaidi ni Ukraine ikiwa akikaza msuli.
Yaani ihalalishwe Russia kuivamia Ukraine sababu Russia inajilinda na NATO kwa kuingilia uhuru wa taifa ambalo lenyewe pia linajilinda na Russia?