Nimeifata hiyo link nimekutana na hii comment ya mdau mmoja hivii... Nimecheka tu
View attachment 2207810Eti now I know why alien land only in US [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] akiwa na maana Russia hakuna mdudu wa kutua kwenye anga hiyo.
Ila Warusi washenzi sana aisee,waliwahi kuKipiga chombo Cha alien na wakakikamata.
Pia watu wengi hawajui ujasusi wa wa Urusi.
Nilisoma mahali KGB na majasusi wengine wa Urusi walifuatilia taarifa na nyendo za aliens na wakajua ainabalimbali za aliens.
Kuna Alliens wakorofi Adui wa binadamu kuna Alliens wapole yaani rafiki wa binadamu.
Watu wengi wanajua Kuna Area 51 lakini watu wengi sana hawajui kuwa Kuna eneo la Urusi la Siri Zaid kuliko Area 51, huko tafiti zote za silaha,mbinu za jeshi na ujasusi na mengineyo zinafanyika.
Eneo linaitwa "Kapustin Yar".
Pia watu wengi sana hawajui Urusi ndio mwanzilishi wa kwenda anga za mbali na ndio nchi ya kwanza duniani kupeleka binadamu anga za mabali.
Watu wengi sana hawajui kuwa Urusi ndio alieunda sehemu muhimu sana ya International Space Station ISS na kuwakaribisha akina USA na wachovu wengine.
Lakini kabla ya ISS watu wengi hawajui kuwa Urusi ilikua na Space Station yake peke yake iliyokadiriwa kukaa angani miaka 11 lakini ikakaa miaka 13.
Hii ilikua ikiitwa MIR.
Watu wengi sana hawajui kuwa baada ya Urusi kufanikiwa kupeleka binadamu anga za mbali ,iliwachukua USA miaka kumi nao kupeleka mtu "mwezini".
Watu wengi sana hawajui kuwa ni Urusi pekee wanaweza kumpeleka mtu akakaa angani mwaka mzima,USA na wenzake hawawezi kumpeleka mtu akakaa mwaka mzima,wao mwisho wiki mbili TU au sidhani kama mwezi anaweza kumaliza.,
Watu wengi hawajui kuwa binadamu wa kwanza kwenda kutalii Anga za juu kabisa alikwenda kupitia Urusi na chombo Cha Urusi.
Huyu alikua Ni bilionea wa kimarekani Bw Denis TIto.
Aliomba NASA ,NASA wakamwambia wao hawawezi kwani unaweza ukatokea uharibifu kwenye ISS,hivyo wakamshauri asafiri kupitia Urusi.
Warusi wakampiga USD million 40.
Binadamu wa pili mtalii alikua ni Tajiri wa South Afrika nae alienda anga za juu kupitia Urusi.
Soyuzi imefanya kazi hii sana. 😥😥