LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Huwezi kujifunga kwenye minyororo ya historia,huyo Russia angetaka hicho anachodai asingeruhusu Nchi zilizokuwa sehemu ya federations ziwe Republics.

Kwa kuruhusu tuu hilo hana haki tena na anachodai.Ndio maana sasa ameamua kupandikiza watu kwenye majingo yanayojitenga,anatumia njia ile ile walioyotumia west so vita ya nini sasa.
Unajua muda mwengine Mtanzania anaweza akang'ang'ania kitu sana hata kwenye nchi yake anaona kama ni uzalendo. Au akang'ang'ania kitu sana hata asichokijua akaona yupo sahihi kumbe suala ni elimu ndogo.

Kingine hatuna utaratibu wa kuwa wasikilizaji wa mambo tusiyoyajua ili tufahamu kwa mapana. Sisi kila kitu tunazungumza tu.

Tunashindwa kutofautisha kati ya mawazo ya mtu na ukweli uliyosemwa na mtu juu ya suala fulani. Mawazo ni haki ya mtu na yataheshimiwa ila kuyarasimisha mawazo ndiyo yawe ukweli ni kuukosea ukweli ukweli.

Nakushauri tusome Mzee.
 
Lakini mm mkuu naona hatua ya Ujerumani kupeleka silaha Ukraine ni mbaya maana ninahofia wenda Urusi ika lazimika kuanza kutumia nguvu kubwa sana kitu ambacho kitasababisha maafa makubwa kwa Ukraine ikageuka Siyria ya Ulaya.
Maana nikikumbuka yale mashambulizi ya anga yaliyo fanywa na Urusi kule Allepo na pata hofu.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Wala usipate hofu,si ni majuzi tu hapa mlikuwa mnasema hii ni special operations itachukua chini ya masaa 24 tu na Ukraine atakuwa keshachakazwa.
 
Mkuu unajishushia heshima kwa kutoelewa vitu vidogo. Sijui una elimu gani, ila angalia miaka 1980-90s URUSI alipeleka BASE yake ya kijeshi NCHINI CUBA, ulitokea mzozo kama huu wa leo. Hii ina maana kwamba, UKRINE hana adui katika ukanda huu, ila URUSI ana maadui ukanda huu ambao ni NATO. hivyo walikubaliana na NATO kuwa kuwe na ukomo wa nchi fulani kuwa NATO, ambapo hizi majirani na RUSSIA zisiwe NATO, leo hii UKRAINE anataka kuungwa NATO huoni ni UGOMVI?? Nchi kama, FINLAND mbona wametulia na hawataki kuwa NATO??
Kwenye huu mzozo URUSI yuko sahihi na wapenda haki watasimama na URUSI.
Achana na suala la elimu yangu. Twende taratibu mahaba weka pembeni.

Unasema makubaliano ya kutokuungwa NATO kwa nchi jirani na Urusi yalikuwa ni makubaliano ya NATO na Urusi si ndo?
 
Nani kasema anataka kupeleka silaha kwenye majimbo yaliyojitangaza huru?

Kisingizio cha Russia ni kwamba hayo majimbo wakazi wake wengi wanaongea ki Russia so wananyanyaswa na Ukraine.

Lakini sidhani kama ni kweli wananyanyaswa, ukweli ni kwamba ni sehemu ya ku destabilise Ukraine na kuharibu ku push NATO nje zaidi ya mipaka ya Russia.
Soma tena maelezo ya Colonel Macgregor wa jeshi la Marekani, yaonekana umekimbilia kujibu kabla hujaelewa alichozungumza Macgregor.
 
Hata mm hili jambo nimewambia watu wengi lakini wamekomaza vichwa Ukraine akiendeleza ukaidi atageuka kuwa Syriya ya Ulaya.
Nikikumbuka Aleppo ulivyo teketezwa ndani ya wiki moja nawaonea huruma raia wa Ukraine.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Muda ni Mwalimu mzuri. Watajifunza kwa matendo tu. Ila Urusi akifikia huko watambadili jina watamuita mnyama hana utu.
 
Shukrani mkuu. Sijui utapataje notification ila huu uzi tangu vita ianze nipo humu na uzuri niko likizo. Hata fainali ya Liverpool vs Chelsea nimeenda ila nikatoka maana niko busy na vita. Tangu jana sijatembelea uzi mwingine, chanzo cha kuja JF ni mambo ya kimataifa
Mkuu wengi tunakufuatilia.
Just to acknowledge sio huyo jamaa tu.
 
Achana na suala la elimu yangu. Twende taratibu mahaba weka pembeni.

Unasema makubaliano ya kutokuungwa NATO kwa nchi jirani na Urusi yalikuwa ni makubaliano ya NATO na Urusi si ndo?
Ukianza nao taratibu hawaji tena,maana wanajua fika unakotaka kumpeleka hawezi chomoka,hawa ndiyo pro Russia sasa,wakati mwingine unaamua kwenda nao kwa style yao ya story za vijiweni tu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nmesoma heading TU,
Ila nadhani Ni kwasababu ya Ile kesi ya mbowe ya ugaidi ambayo KINGAI na wenzake wameleta mashahidu wa kuchonga
(Utani[emoji4])
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Hii vita tayari Ukraine keshapata discipline ya kutosha, vita ikipiganwa kwenye ardhi yako ni majanga matupu kwako. Miundombinu, na mali nyingi zateketezwa. Hapa dege kubwa duniani la mizigo limeteketezwa tayari

 
Wale wazee wa vita ya dunia irudiwee irudiwee. Wakat ndio umefika muanze kuandaa mishale na mapanga
Usisahau kuwakumbusha kujipaka ufuta! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji125][emoji125][emoji125][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Sasa kwa mfano Putin akawahi akatupia hilo Bomu katika Makao Makuu ya jeshi lako huo muda wa wewe kuanza kuji organize utautoa wapi?
Kwani mabomu ya Nuclear yanawekwa Makao Makuu ya Jeshi,unajua Marekani ana kambi ngapi za Kijeshi Dunia nzima?
 
Hapa ni mjadala wa dini au vita?

Hujui urusi alishawahi pigana vita na hao chechinia unaowaita waislam na aliwapukutisha sana!

Risasi haina dini punguza ujinga
Chai, URUSI kuna waislamu 10% Chechen ni Waislam tupu kama hujui.
 
Haya Sasa, habari ndiyo hiyo kwenye hiyo clip...
Wamekimbia na kuacha kila kitu, masikini vijana wana wazazi na familia zao Russia, halafu huyu msela mavi mjinga sana anawaswaga kwenye vita ya kipuuzi....

 
Lakini mm mkuu naona hatua ya Ujerumani kupeleka silaha Ukraine ni mbaya maana ninahofia wenda Urusi ika lazimika kuanza kutumia nguvu kubwa sana kitu ambacho kitasababisha maafa makubwa kwa Ukraine ikageuka Siyria ya Ulaya.
Maana nikikumbuka yale mashambulizi ya anga yaliyo fanywa na Urusi kule Allepo na pata hofu.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
Wakati Russia inafanya Yale mashambulizi pale Allepp ilikua na inamiliki anga lote la Syria bila upinzani wowote ule toka Kwa ISIS lakini sasa Hali NI tofauti maana Ukraine Wana air defense na nyingine ni man pads (zile zinabebwa tu begani) na bado Ujerumani na nchi nyingine zinatuma hizo manpads Kwa maelfu kwenda Ukraine. Hivyo si Rahisi Kwa Russia kufanya kampeni ya Syria ndani ya Ukraine. Labda warushe makombora mbali na anga la Ukraine.
 
Una akili sawa? Yaan NATO watangaze kupeleke vikosi afu wewe ucheke??
Kwan NATO wamesema wanapeleka Nuclear weapons? Alafu Kwan hizo silaha anazo yeye tu wenzie hawana? Hizo ni dalili za kupagawa Kwa Putini
 
Ukraine wanavibweka sana nadhani Putin huko alipo anajutia sana.

 
Back
Top Bottom