LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Kwa hiki kinachoendelea hivi sasa kati ya Ukraine na Russia nadhani kama Rais wa Marekani angekuwa Donald Trump saa hizi Russia ingekuwa imeshafutika kwenye uso wa dunia hii
 
Mbona Hammas wanafanya hivyo hivyo lakini Israel akishambulia mnasema anaua Raia?

Hivi unafikili ingelikuwa na Ukraine inashambulia ndani ya Moscow kwa Makombora hao Raia wa Ukraine wangelionewa Huruma? Warusi wangelipiga BOMB CLUSTERS Kama zile za Syria.
 
Unajua maana ya Warmonger? Tuanzie hapo kwanza
 
Hawa wabaguzi wa Ukraine wanawazuia waafrika kupanda treni kutoroka mapigano kwenda Poland.

Kinachosikitisha zaidi wanawazuia hadi wanawake na watoto tena wajawazito kisa tu rangi zao za mwili.

Acha tu Putin awaanyooshe. Wengi msiojua tangu Putin angie madarakani Urusi Kaleta mabadiliko makubwa sana kwa watu weusi waishio Urusi kwa kuweka sheria za kuheshimiwa na haki.

WayUkrain wabaguzi sana. Acha wanyooshwe tu.
 
mbona poland, Deutschland, Netherlands, turkey, wametoa msaada ya fedha na silaha kwa kyiv hawajafanywa chochote mpaka muda huu

Inategemea na msaada upi, wa bidadam n.k. lakinii sio msaada wa jeshi, wajaribu waone.
 
Maelezo mazuri unaeleweka.
 
Formula ni ile ile booby trap....wanaingia kwenye target wanavuja damu.
Tuwaombee tu watu wa ukraine ila kwa ninavyowajua warusi, si watu wa kukubali kushindwa kabisa wapo tayari wafe hata milioni ila lengo lao litimie.

We fikilia wamepeleka wanajeshi wengi kuzunguka mji mkuu wa Kiev ila bado wanaona haitoshi.CNN imeriport muda sio mrefu kuwa kuna convoy ya magari ya kijeshi kama 60 yakielekea mji mkuu. yapo kilimeter kama 6 kutoka mji mkuu.

Wakati uwo uwo msafara wa wanajeshi kutoka Chechen upo kam kilometer 30 ukielekea Kiev.tuombe Mungu jaman maana ninachokiona mbele sio kizuri kabisa naomba waelewane wamalize hii vita
 
Sasa kwa mfano Putin akawahi akatupia hilo Bomu katika Makao Makuu ya jeshi lako huo muda wa wewe kuanza kuji organize utautoa wapi?
Ngoja nikusaidie tu.

Kurusha Kombora la Nyuklia kutoka Russia Hadi Marekani itachukua dakika 30 kufika Marekani.

NUCLEAR BASED SILOS (Siraha za Nyuklia za Marekani zilizoko Chini ya Ardhi) Mfano,ATLAS MISSILES,TITAN MISSILE na MINUTEMAN MISSILES Zinaweza kufyatuliwa ndani ya Dakika 5 TU na kuanza Safari ya kuelekea Urusi. Kwahiyo,Makombola ya Urusi na Marekani yatapishana angani Kila Moja yakienda kumaliza kazi iliyotumwa. Baada ya Dakika 30 hakutakuwa na Kitu kinachoitwa Urusi Wala Marekani kwenye Uso wa Dunia. Wingu kubwa la Mionzi(NUCLEAR FALLOUT) na Vumbi litatanda angani Dunia nzima na kuzuia kabisa mwanga wa Jua kufika kwenye Uso wa Dunia. Mimea yote itakufa kwa kukosa mwanga wa jua kwa ajili ya Photosynthesis. Kwa Vile Mimea ndio hutoa Oxygen kwa ajili ya Wanyama akiwemo binadamu Basi Oxygen itapotea yote, Wanyama wote watakufa kwa kukosa Hewa. Matajiri ambao wataweza kupata Artificial Oxygen kwa kutembea na Portable Respirators nao wataanza Kufa kwa CANCER mbali mbali kutokana na Mionzi ya NYUKLIA (Radiations) kuanza kufanya IONIZATION na Kutafuna TISSUE za Miili yao.

Kwahiyo ndugu yangu ukiona mtu anashabikia Matumizi ya Siraha za Nyuklia kisa TU upande wake anaoushabikia ndio ushinde ujue ni Rayman hajui lolote kabisa. Ndio maana ni Mara chache Sana Mimi kuwajibu watu hao japo nina majibu mazuri kabisa.
 
Russian state TV: manuari zetu pekee zinaweza ku launch zaidi ya 500 nuclear warheads, ambayo tunawahakikishia kuiharibu US na NATO kwa uzuri tu. Kanunini yetu ni rahisi tu "kwanini Tunahitaji Dunia wakati yenyewe hitaki Russia IWEPO"?




Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Ukifikiria kama hivi basi utaingia kwenye matatizo kama yaliyomkuta Ukraine. Russia haitaji uwe mshirika wake. Anachohitaji ni usalama wa nchi yake; lielewe dhumuni na mantiki ya Russia. Na hakuna anayepinga kama Russia naye kijeshi ni mkubwa kama huyu mkubwa aliye na ushawishi.

Nimejaribu kuirejea historia lengo ni kupata kujua endapo ukiwa kwenye nafasi kama ya Ukraine uishi vipi! Historia inatufunza kwa Cuba baada ya kumkaribisha Soviet aweke makombora yake. Cuba ni pua na mdomo na US. US kwake ikawa ni tishio. Alichokifanya aliwapiga vikwazo Cuba. Haikutosha akajaribu kufanya mapinduzi ila yakashindwa.

Huyu ni mwenye nguvu ya kijeshi na ushawishi alitumia nyenzo zake. Mwenye nguvu ya kijeshi peke yake unafikiri atatumia nguvu ipi?

Kingine umezungimzia vikwazo kwa Mrusi tambua ya kwamba havitomuathiri peke yake. Kwa namna moja na nyengine vita athiri na wengine kwa sababu: Russia ndiyo nchi ya 3 duniani (kama sijakosea) inayozalisha mafuta kwa wingi baada ya mashariki ya kati. Russia naye ni mzalishaji mkubwa wa ngano duniani. Russia ni miongini mwa nchi zinazozalisha gesi kwa wingi duniani.

India, Misri, China n.k zinategemea ngano ya kutoka Russia. Misri inatumia takribani $ billion kadhaa kununua ngano Russia. Bara la ulaya wanategemea gesi kutoka Russia kwa % kubwa. Kuna nchi nyengine zinategemea kwa 100% gesi ya Russia zipo Ulaya na huku wanataka kumtoa kwenye mfumo wa SWIFT hayo malipo mtayafanya kwa njia gani? Ukraine yenyewe inategemea gesi ya Russia.

UK anatumia sana anga ya Russia kwenda New Zealand, Australia n.k Russia naye kampiga vikwazo vya kutotumia anga yake. Ina maana UK ata-change route ambayo itakuwa ni ndefu sana (hapa gharama za mafuta zitaongezeka) itasababisha gharama kwa mteja kuwa juu sana.

Hivyo haya masuala ni mapana. Russia wataathirika ila Russia hatoathirika peke yake. Unampiga vikwazo huku unategemea gesi kutoka kwake naye akiongeza gharama za mauzo ya gesi mtafanyaje?

Nafikiri kwa kiasi fulani tumeelewana?
 
Kama kuna mpango wa kufanya siege warfare, maana yake kuna uwezekano mkubwa sana wa kuongezeka kwa vifo vya raia endapo wataamua ku-react hapo baadaye. Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi kuthibitisha suala hilo.
Una maanisha nn mkuu sija kuelewa.

Sent from my TECNO BB4 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…