Kidokezo cha asubuh [emoji847]
Mtizamo wangu mwingine kuhusu hii operation ya Russia. Kama Russia angeipeleka speed na kuimaliza mapema (Na huu uwezo anao) basi isingeleta hata ile walau a fraction of harm kwenye uchumi wa hili kundi la Western wakiongozwa na kiranja wao US...
Ukiwaangalia wale "International Community" kila uchao ni majanga kwao, wanapoteza ushawishi na gharama nyingi za vifaa wanazo'jaza ukraine zikiishia kuharibiwa.
Nchi karib zote za Ulaya sasa zinakumbwa na janga la Inflation, Viwanda vingi vinafungwa, Idadi kubwa ya watu wakipoteza ajira kupitia "reactions" zinazofanywa na Viongozi wao wenyewe.
Ukirejea nyuma kwenye Annexation of Crimea, ilikuwa Military Operation ambayo ilifanyika kwa kasi mno, ndani ya siku 7 za mwanzo teari walikuwa wameshabadili uongozi uliokuepo... mwezi mmoja na siku 6 tu. Crimea ilikuwa rasmi ndani ya Russia OFFICIALLY..
Aftermath ni Russia kuondolewa G8 na Mfulululizo wa International Sanctions kuanza kuandamwa... Ndani ya vile vikwazo upande wa EU na Western kwa ujumla hawakua na cha kupoteza...
Hivi kama hii OP ingeisha haraka tungejuaje madudu yaliyojaa kwenye vichwa vya hawa viumbe ase?
Round hii mambo yamekuwa tofauti, look like Russia imeingia imejipanga kikamilifu ikijua nini kitatokea kwa uingiaji wao ndani ya Ukraine. Inaonesha kabisa wazi kua mbali na Denazification waliyoitamka ni kama vile wako na harakati za kuibomoa hii Empire of Lies.
Kwasababu uwezo wa kuisambaratisha Ukraine wanao, tena mkubwa mno but they choose to be soft dhidi yao. Hawa Western wanairefusha wakihisi wanamkomoa Russia ila uhalisia ni kua wanajimaliza wenyewe huku wakizidi kumnufaisha Russia.
Em tuangalie upande mmoja tu wa nishati... tuambizane nani anayefaidika sana kwa bei ya Nishati kua juu? Mnunuzi au Muuzaji? Kama ni Muuzaji je atataka bei iwahi kushuka chini? Je hii haileti majibu ya kwanini Russia anafanya makusudi kuipeleka Operation Polepole [emoji23]?
EU na US imekua ikitolewa taarifa karib kila siku kuhusu kuporomoka kwa uchumi kwenye nchi hizo. Wote twajua uchumi ni shughuli za kibinadam. Ambazo msingi wake mkuu ni nishati. Matumizi ya nishati yanapoathiriwa basi shughuli zote zinaathirika. Na hili wanafanya kujikaanga wenyewe kwa "sufuria" walilopewa na Russia bila kuambiwa kazi ya sufuria n nn [emoji847]
Nasema hivyo kwasababu na nyie ni mashahidi, Russia alikuwa na uwezo wa kuziharibu all doors upande wa west Ukraine wanakopitishia Silaha. But ajab akaziacha ziendelee kuingia...
Anao uwezo wa kuharibu mifumo yote ya mawasiliano ndani ya Ukraine ili kupoteza connection kwa frontline kutoka kwenye Command Post zao... Anao uwezo wa kuharib Supply chain ya jeshi zima ila kayaacha kama yalivyo huku akienda veeeery slow na naendelea kusema ni makusudi sio kwamba hawezi kuharakisha.
Hapa Russia Vs Ukraine is actually a front in the greater proxy war between China and US, na hii z what few people understand. THE NEW WORLD vs THE OLD WORLD... no wonder Biden alikuwa anadai kua vitu vinaenda badilika.. kua tunaenda kwenye NEW WORLD ORDER ambayo wao wanataka kutake the Lead...
Na ni maoni yangu kua Russia asingeifanya hii Operation kama asingekuwa na Full back up, full support kutoka kwa China na wenzie hasa kwenye Issue za kiuchumi.