Omary - Msamalia
JF-Expert Member
- Jan 19, 2020
- 2,077
- 4,525
Pro Russia hivi Putin analipuaga Silaha Gani hii mizinga inaitwa M777
Huyo ndio Putin sasa Wa magharibi wakiwaza hivi yeye anakuja vile, jamaa anajua kuwapiga chenga za mwili.Victory Day Parade ndio imeisha dakika chache zilizopita, ilitumia kama dakika 50 hivi. Haikuwa na mambo mengi, silaha sio nyingi, wanajeshi kwenye parade sio wengi, manjonjo kiasi. Angani ndege na helikopta hazijapita wanasema hakukuwa na hali nzuri sana ya hewa.
Putin hajasema lolote la kutishia kama wengi walivyotarajia, alitoa hotuba ya kawaida ila kaitaja Marekani directly. Silaha kama MSTA self propelled howitzer, Bumerang APC, T14 Armata na T34 zilikuwepo.
Ni maadhimisho ya kawaida zaidi tangu nianze kuyatazama 2015
Ni kibano kwa kwenda mbele anapewa👇Huyo ndio Putin sasa Wa magharibi wakiwaza hivi yeye anakuja vile, jamaa anajua kuwapiga chenga za mwili.
Mapuuzi ya NATO cheki yanavyoweka habari na picha za kipropaganda
Hawa wataliwa haraka harakaFinland yuko tayari sasa kujiunga NATO na kajitayarisha kwa uvamizi wowote kutoka Russia 👇
View attachment 2217883
Na Ukr mlisema hivyo hivyo ila hadi sasa mnalia Lia.Hawa wataliwa haraka haraka
umeeleza fact kabisa mkuu,Ila kumbuka Russia anaijua mipango Yao yote ya wamagharibi,thus why unaona kila wakija na hiki jamaa anategua ,kirahisi!! ninachokiona mm uliyoeleza nikweli ndo lengo la US ,Ila US huwa hawezi kukamilisha mpango wake mpaka apate kampani na watu wa kumjoini ,Ila awamu hii imekuwa tofauti ,mataifa rafiki na US yameshtuka huu mchezo wa US ,na Kama unavyoona hawako tayari Kama mwanzo kumunga mkono kwenye mipango yake ,ambayo kimsingi haina faida zaidi ya kuleta giza kwa mataifa. mfano German alikataa bila kuficha hayuko tayari kuunga mkono vikwazo vya katazo la kununua mafuta ya russia ,kwa dalili hizi Basi US awamu hii ata feli Sana kukamilisha mpango wake dhidi ya russia .Kuna huyu Mzee mmoja anaitwa E. Michael Jones, American Author katika mahujiano yake na Kituo cha habari cha Press TV ya Iran anasema kwamba namnukuu
"the United States believes a long, exhausting war in Ukraine will lead to the collapse of Russia in the same way that the Afghanistan war led to the collapse of the Soviet Union and that's why they don't negotiate with the Russians."
View attachment 2217828
Ukiizingatia hiyo kauli, inatupa majibu kadhaa ya maswali ambayo huwa tunajiuliza kila siku. Miongoni katika hilo ni lile kuhusu kua kwanini US hawataki wamalizane kwa diplomasia anaendelea kukoleza moto hapo Ukraine.
Kiasi nakubaliana na mawazo yake ingawa kuna kitu kingine mie najarib kukiona. Naitizama Afghanistan kama Kaburi la empires. Kila empire iliyopigana hapo Afghanistan huwa hazina maisha marefu. Na hii naiona iko reflected hata kwa US.
Historia inatwambia USSR ilipigana na Afghanistan toka 1979 hadi 1989... Na miaka miwili baadae USSR ilivunjika. Katika hiyo Vita USSR ilishindwa na hao Mujahedeen wa hapo Afghanistan.
View attachment 2217833
Kinachofurahisha hapa ni kua LIST ya nchi zilizokuwa mgongoni kwa hawa Mujahedeen inashangaza sana... Ni US na mashost zake.... Kama ilivo sasa kwa Ukraine.
View attachment 2217839
View attachment 2217841
Ni hiki kipindi media za Magharibi zilikuwa zikimtangaza Osama bin Laden kama shujaa...
View attachment 2217845
Na walio kua nyuma ya hayo mapigano yote ni US...
View attachment 2217847
Maajabu hayakuishia hapo tu... Miaka kama 12 baadae, 2001 US na team yake wakaingia Afghanistan kupigana na kikundi walichokua wanakipa support awali.
View attachment 2217855
View attachment 2217857
View attachment 2217859
List ni ndefu mno ila matokeo ya hiyo Vita ni Wataleban kujinyakulia ushindi...
View attachment 2217873
[emoji847]
View attachment 2217877
Sasa em tizameni hiyo list yoooote kuisoma mpk inakera ya Nchi zilizoshiriki kupigana na hao wataleban kwa miaka karibia 20 yet wamekosa ushindi. Leo Russia ana miezi miwili anaitwa dhaifu [emoji23].
Last year wakati US na team yake wanatangaza mwisho wa chokochoko lao hapo Afghanistan kuna Dr mmoja hivi akanambia... Galip enzi za USSR ulikuwa mtoto, sasa shuhudia kudondoka kwa empire nyingine duniani kwa macho yako... Nikamuuliza kwanini....
Afghanistan imekuwa Grave yard of empires na ukiutizama mwenendo wa Western unakoelekea ndiko... Time will tell soon or later ka ni kweli au Laa [emoji848]
Sasa aliyemsimamisha Hitler ya ujerumani ni nani!!?Mrusi kelele tu hana huo ubavu ajaribu apigwe nyie mnawaona kama wanaiweza dunia ahahah. Alikuwepo mwanaume hitler huyo putin mweupe tu. Nipo Manzese kwa mfuga mbwa.
Kwenye G7 ujerumani yupo? Kama yupo hakuna vikwazo hapo
Hamna kitu apa takataka tuUchambuzi: Putin sasa anakabiliwa na aina tofauti tu za kushindwa vita:
Mafanikio ya kijeshi ya kigeni ya Putin kote ulimwenguni baada ya 2008 yalipatikana kwa kutumia vitengo vidogo vya vikosi vya wasomi, mamluki, na vikundi vya wanamgambo wa ndani pamoja na jeshi la anga la Urusi.
Hii iliipa Moscow faida kubwa kwa gharama ya chini wakati wa kuingilia kati huko Georgia, Nagorno-Karabakh, Syria, Libya, Mali na mara mbili nchini Ukraine mwaka wa 2014, kwanza katika kunyakua Crimea kinyume cha sheria na kisha kuunda majimbo yaliyojitangaza ya Urusi huko Luhansk na Donetsk.
Katika kila hali, Urusi ilisonga haraka na kwa ukatili kwa njia ambazo ulimwengu wa magharibi haukuweza kukabiliana isipokuwa kupitia sheria za vikwazo zilizohitimu - hakuna kitu ambacho kingeweza kubadili ukweli. Putin alikuwa hodari katika kuunda "ukweli mpya juu ya ardhi".
Mnamo Februari alijaribu tena kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo nchini Ukraine - kunyakua mamlaka ya kiserikali ndani ya saa 72 katika nchi ya watu milioni 45 inayomiliki eneo la pili kubwa la ardhi barani Ulaya.
Ilikuwa kamari ya kustaajabisha na isiyojali na ilishindikana kabisa katika wiki ya kwanza muhimu.
Putin sasa ana maamuzi machache lakini kuendelea mbele ili kufanya vita hii kuwa kubwa zaidi ama kubwa zaidi nchini Ukraine au kubwa zaidi kwa kusonga mbele zaidi ya mipaka yake.
Kuongezeka kunajengwa katika hali ya sasa na Ulaya imefikia wakati hatari sana katika historia yake ya hivi karibuni.
Baada ya kushindwa na Mpango A wa kukamata serikali ya Kyiv kabla ya majeshi ya Rais Zelensky, au ulimwengu wa nje, haujaweza kuguswa, Moscow ilibadilisha Mpango B. Hii ilikuwa mbinu ya kijeshi ya "manouvrist" zaidi ya kuzunguka Kyiv na kuhamia Ukraine nyingine.
miji ya Chernihiv, Sumy, Kharkiv, Donetsk, Mariupol na Mykolaiv na kuzima upinzani wa Kiukreni kwa silaha wakati Kyiv yenyewe ingetishiwa kusalitiwa au kuharibiwa.
Hili nalo lilishindikana. Kherson ndio jiji kuu pekee lililokuwa chini ya udhibiti wa Urusi na tangu wakati huo limeendelea kupinga utawala wa Urusi.
Ukweli ni kwamba vikosi vya Urusi vilikuwa vidogo sana kutawala nchi kubwa kama hiyo; walifanya vibaya sana kwa sababu mbalimbali, waliongozwa vibaya na kutawanywa kuzunguka pande nne tofauti, kutoka Kyiv hadi Mykolaiv, bila kamanda mkuu.
Nani atasoma makamasi yakoInaendelea...
Jeshi la Kiukreni lililodhamiria na lililofunzwa vyema ambalo lilipigana nao hadi kusimama katika maonyesho ya kawaida ya "ulinzi wenye nguvu" - bila kushikilia mstari lakini badala yake kuwapiga washambuliaji katika maeneo ya hatari zaidi.
Kwa kuchanganyikiwa, Urusi sasa imehamia "plan C", ambayo ni kuachana na Kyiv na kaskazini, badala yake kuelekeza nguvu zake zote kwa mashambulizi makubwa katika eneo la Donbas na kusini mwa Ukraine, pengine hadi bandari ya Odesa kusini magharibi kwa ufanisi kuzuia nchi.
Hii ndiyo kampeni tunayoiona sasa ikichezwa mashariki karibu na Izyum na Popasne, Kurulka na Brazhkivka.
Vikosi vya Urusi vinajaribu kuzingira Operesheni ya Vikosi vya Pamoja vya Ukraine, (JFO) karibu 40% ya jeshi lake ambalo limechimbwa kinyume na "jamhuri" zilizojitenga za Luhansk na Donetsk tangu 2014.
Malengo muhimu ya Urusi ni kuchukua Sloyansk na, mbele kidogo. kusini, Kramatorsk. Zote ni sehemu muhimu za kimkakati za udhibiti wa eneo zima la Donbas.
Na vita vimehamia katika awamu tofauti ya kijeshi, mapambano katika nchi iliyo wazi zaidi, wakati wa hali ya hewa bora, na vifaru, askari wa miguu walio na mitambo na zaidi ya yote, silaha - iliyoundwa kuharibu safu za ulinzi za wapinzani kabla ya vikosi vya silaha kuingia.