LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hizi taarifa za media yaani ni mwendo wa kuvuruga akili zetu tu. Maana ninachokisomo naona kinaenda tofauti na tunayopata kutoja kwa jamaa zetu waliopo Ukraine na Russia. Kuna taarifa zingine kwenye Media ni Propaganda
 
Hizi taarifa za media yaani ni mwendo wa kuvuruga akili zetu tu. Maana ninachokisomo naona kinaenda tofauti na tunayopata kutoja kwa jamaa zetu waliopo Ukraine na Russia. Kuna taarifa zingine kwenye Media ni Propaganda
Ila nakumbuka wiki mbili zilizo pita waafrika walipo Urusi na Ukraine tulipo wauliza kwamba nini kinaendelea huko ? Kwani vyombo vya Habari vinatuhabalisha habari za kushitua sana huko .

Majibu mengi yalidai mambo Ni shwari tu hakuna tatizo
 
Nimejaribu kuwafuatilia kwa muda humu nimeona wazi watu wengi wanaongozwa na mapenzi binafsi juu ya upande fulan hasa hawa wanaojionyesha NI PRO USA+NATO...unakuta mtu anakwambia eti siku ya tano leo mbona urusi hajaiteka kiyv(ambayo ndio mji mkuu wa ukraine)....HEBU WATOE HISTORY NI LINI NA WAPI MAREKANI WANAOMPIGIA CHAPUO HAPA AMEWAI SHINDA VITA KWA SIKU TANO???..wote tunafahamu humu mwaka 1950 mmarekani alishindwa vita dhidi ya taifa dhaifu kabisa la vietnam vita ile aliyopigana zaid ya miaka 4 na hakutoboa...unakuta mtu anakwambia mbona huyo putin kashindwa kuifanya ukrain majivu...ukweli ni kwamba URUSI HATAKI UKRAINE KUJIUNGA NA NATO NANDICHO ANAPINGA UTANUZI WA UMOJA WA NATO KUINGIZA WANACHAMA WAPYA KINYUME NA MAKUBALIANO AMBAYO AFISA WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE YA RUSSIA ALIINGIA NA NATO 1992...YOTE HII MRUSI AKIWA ANA WASIWASI KUWA WANAWEZA MFANYIA MASTERPLAN WAKAIGAWA ZAIDI RUSSIA KAMA ILIVYOTOKEA KWA USSR HUKO AWALI. na kiuhalisia mji wa kyiv hauna waasi huo mji upo mikononi mwa serikali kwa miaka mingi...mikoa ya ukraine ambayo ilikuwa inawaasi wanaopingana na serikali ya ukraine ni miwili tu LUHANSK NA DONETSK ambayo russia alishasign hati ya kuitambua kama nchi huru na ndio mikoa ya kwanza kuitwaa kabla ya kuingia hapo kyiv tokea usiku wa tarehe: 26 kuamkia tarehe:27...na lengo la urusi si kutake over all the ukraine country ni kumega mikoa hiyo iliyokuwa inakaliwa na waasi na pia kumdhoofisha ukraine ili aachane na mikakati ya kujinga na nato...na mpaka sasa mikoa hiyo ya luhansk na donetsk imeshachukuliwa kutoka mikononi mwa ukraine na

Hadi ile tareh:25 mwezi huu rais wa ukraine aliomba msaada kutoka kwa wajumbe 27 wa nato na wote hawakuwa na dhamira ya msaada na kutoa jibu la moja kwa moja wataisaidia vipi ukraine na kitu icho ndo kimefanya rais wa ukraine kukataa msaada aliotak kupewa na biden kutoka kwenye simu aliyopokea tareh:27 asubuhi kutoka kwa biden...na kwa kitendo icho TAYARI KIMEONYESHA DHAMIRA YA RAIS HUYO KUWA HATAKUWA TAYARI KUJIUNGA TENA NA NATO MARA BAADA YA MZOZO HUU KUISHA MAANA AMEGUNDUA NI WANAFIKI NA NDIOMAANA "ALIANZA KUHIMIZA VITA HII TUTASHINDA NA KILA RAIA WA KIUME UKRAINE WA UMRI KUANZIA MIAKA 18 HADI 60 ASHIKE SILAHA KUIPAMBANIA NCHI YAO WENYEWE"...na ukweli ndo huo marekani na washirika wake wa nato ni wanafiki maana inakuwaje mtu mnayemhimiza ajiunge nanyie nato anavamiwa hadi Mikoa yake ya mipakani LUHANSK NA DONETSK inachukuliwa na amewaomba msaada hamkurespond na baadae ndo mnajifanya kumpigia simu na kumwambia mumsaidie financial wakati mtu anapigwa?...iyo itamsadia nin??...nandio maana rais wa ukraine akakataa hadharani kwenye akaunti yake ya insta hii ilimfanya marekani+nato waonekane hawana nia ya kuisave ukraine...na hatua hii ndo imepelekea USA kujinasibu kuwa itawasaidia ukraine ANTI-AIRCRAFT MISSILE STINGER ...huku nato walikutana kwa dharura na kukubaliana kuongeza SEVERE ECONOMIC SUNCTIONS KWA URUSI NA MAKAMPUNI YAKE....kitu ambacho hata korea kaskazin waliwekewa hivyo vikwazo miaka nenda rudi na bado wanasurvive freshy tu...sikatai itamdhohofisha putin kiuchumi lakini haitofanya lengo lake alitakalo kukamilika kiuhalisia that guy is a COWARD...yaan haogopi ivyo vikwazo na bila shaka alisha asses iyo risk kabla ya kuianza iyo vita hivyo alishacalculate wapi nato watakimbilia before.

UKITAKA KUJUA NATO+USA NI WANAFIKI RAIS WA UKRAINE ALIPOST HII.

IKIWA RAIS WA TURKEY BWANA EDORGAN ANAWEKA WAZI KUWA NATO WANAMFELISHA UKRAINE WEWE NI NANI HUMU JF kuwasifu nato na marekani kama msaada wa ukraine kwenye hii battle???

Ifahamike kuwa russia hajafanya full scale invasion kwa ukraine kama alivyofanya pale syria dhidi ya waasi wa asadi...angefanya ivyo maana ake angetumia kila silaha aliyonayo na ukraine isingekuwa salama hadi ivi sasa...maana inafahamika wazi kiuwezo wa kijeshi Ukraine bado sana kwa russia kwa msiojua labda.

Nato hawana meno direct dhidi ya mgogoro huu...ukilinganisha na madhara ambayo anayapata ukraine!...mitizamo ya watu walio wengi WALITAZAMIA KUMSAIDIA UKRAINE DIRECT KWA KUTUMA ARMED-TROOPS ZIKAMPIGE MRUSI PALE UKRAINE LAKINI CHAKUSHANGAZA KILA ANAYEJITOKEZA KUSAIDIA AKIWEMO CANADA NA UINGEREZA ANATOA MSAADA WA SILAHA KITU AMBACHO SIO GENUINELY KWENYE FIELD OF WAR MAANA WHAT IF WANAJESH WA UKRAINE HAWANA 100% EFFICIENCY YA KUTUMIA HIZO SILAHA ZA MISAADA MAANA HAWAKUWA WAKITRAIN NAZO TOKEA HAPO AWALI NA ZIMEKUJA WAKATI HUU KAMA MSAADA.



Watu waliowengi PRO USA+NATO WANATAZAMIA AIBU AMBAYO ATAIPATA RUSSIA ASIPOWIN HII VITA...WANASHINDWA KUJUA RUSSIA AMESHAPATA 80% YA MALENGO YAKE YAANI AMESHATWAA MIKOA YA LUHANSK NA DONETSK iliyokuwa inashikiliwa na waasi waliyoipinga serikali ya ukraine kama alivyofanya hivyo huko nyuma kwenye rasi ya Crimea iliyokuwa sehemu ya ukraine 2014 na hivisasa ni urusi...kilichobaki ni ukraine kutokubali kuingia NATO tu.

Tokea jana zipo taarifa kutoka kwa rais wa ukraine kuwa kuna mazungumzo kati ya ukraine na maafisa wa urusi yatakayofanyika mpakani mwa jirani yao Belarus...ikumbukwe mkutano huu haujaitishwa na urusi...ni rais wa belarus ndo amefanya juhudi hizi kuwakutanisha majirani zake.

Japo rais mwenyew wa ukraine anasema hana imani kama maongez hayo yatazaa matunda...beleive it makubaluano hayo yanaweza kuwa na kifungu cha kumlimit yeye ukraine kwa maandishi kwamba hatojiunga nato siku za usoni wala hapo miaka ya baadae...sasa itakuwa ni juu yake kukubali au kukataa na kufanya vifo vya watu wasio na hatia viendelee kutokea nchini kwake.
 
umesema ww ni waziri wa wapi wa mambo ya nje?
 

Kwako wewe neno "large" unalielewa vipi, ndani ya siku nne uue watu 352 kwa kuwapiga mabomu ndani ya makazi yao, hiyo unaona sio large?
 
Wapo kwenye Mpaka wa Ukraine na Beralue mbona mnataka kupotosha? Ukraine iligoma kwenda Belarus Kama Putin alivyopendekeza awali.

Hata hivyo nashangaa,hivi Kabla ya Vita si huyo huyo Putin aliyekataa kwamba hazungumzi na Ukraine Bali anataka kuwekeana Mikataba na USA? Na akapeleka Mapendekezo yake na Masharti Kule Marekani ambayo yote yalipigwa Chini?

Viongozi wengi walitiririka kwenda Moscow kumtaka asiivamie Ukraine Bali atumie Diplomasia lakini akaamua Kuvamia.

Leo amekubali kukutana na Ukraine,Kweli Ushujaa ni Mhimu hata Kama uko dhaifu kiasi gani.
 
Russia imesema kwa muda mrefu haitaki kuona Ukraine yatumiwa kuwa kichaka cha NATO na Marekani.

Kumbuka mafahali wawili huwezi kuwaweka zizi moja.

Russia hataki Marekani asogee karibu kupitia mgongo wa Ukraine.

Ukraine ingeruhusiwa kuingia NATO basi ingepewa Air defence systems za kuzuia mashambulizi ya Russia na Russia ingekuwa haina uwezo wa kuzishambulia nchi zote majirani na ingevamiwa.

Ndo maana Russia ikaiwahi Crimea na sasa yaitaka Ukraine.

Poland, Latvia na Romania ndio majirani pakee ambao Russia hana shida nao kwa upande wao magharibi na kusini magharibi.

Estonia ambako vipo vikosi vya majeshi ya UK na wengine nao Russia hana shida nao.

Russia haitaki kuona NATO na Marekani upande wa mashariki na kusini mashariki hadi bahari nyeusi.
 
Kwaio na wewe unaiamini io tovuti kwa kila kitu.? Yani mzaliwa wa chato burigi akatambuliwe jina na mkenya wa kisumu huko kiraisi raisi tu.? Maiti zinaungua moto hovyo uo utambuzi wanatumia njia gani kuwatambua.? Au ndio unaamini propaganda za kua warusi 5000+ wameuwawa na ao kiev.? Unaamini data za kiev au urusi ambae hajatangaza hata idadi ya wanajeshi walioko huko wala walio kufa.?

Punguza kua mjuaji ktk mambo ya wanaume.
 
Leo vita imesimama kupisha majadiliano ,kama majadiliano wasipopatana kesho vita itaendelea,na misaada ya kijeshi inazidi kumiminika kwa ukraine kutoka member wa nato
sijui sana mambo yavita yanaendaje ila kwanilichoexperience ndani ya siku 3 hizi urusi nikama wanaattack sana usiku kukipambazuka hawafanyi heavy millitary operation yeyote zaidi yakumove kutoka eneo moja nakusonga mbele....nadhani leo wanaweza wakashambulia zaidi usiku kama maafikiano hayatafikiwa kwasababu jana usiku pia walishambulia sana licha ya ukraine kukubali kufanya mazungumzo
 
Watu mnaishabikia sana Russia na kusahau kuwa hiyo Russia inasapotiwa ki maneno na Ukraine inasapotiwa kivitendo.
Msitegemee kuona washirika wake wakijiingiza ktk hiyo Vita ya kipuuzi.
Rejeleeni mgogoro wa Russia na Georgia ulianza km huu wa Ukraine mara Russia akapoteza kwa Georgia na hamtoamini hi itajirudia Tena.
Ht uwe na nguvu vipi ukipingwa na mataifa ya Ulaya pamoja na America ushapoteza.
 
umeandika 🚮🚮🚮🚮 kanywe maji ulale
 
Kwenye media hii vita urusi anachezea kichapo kweli kweli ila kwenye uwanja wa vita ukraine maji yamemfika shingoni
View attachment 2134045
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hii vita mitandaoni URUSI askari wanauawa kama M23. Ila sasa wenyewe UKRAINE muda wote wanaomba msaada wa vifaa, askari na hata kugawa silaha kwa Raia wao, wafungwa nk. URUSI wameteka miji kibao ya UKRAINE lkn huku ndani wanasema wamepigwa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Anachotaka kufanya urusi Kwa akili yako ni sahihi ??? Huwezi kumchagulia ex wako Bwana wa kuishi naye 😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…