Ilikua USSR na sio UrusiHahaha ukisema Russian Federation hawaelewi pia unapoitaja urusi hawaelewi wanadhani urusi ni nchi 2 au moja kama Tanzania. JAMANI,URUSI NI MUUNGANO WA NCHI 23 AMBAZO ZIKAUDA URUSI KAMA ILIVYO KWA USA. Na Ukraine ilikuwa miongoni mwa izo nchi kabla ya kujitenga.
Nadhani inatosha.
Kama Urusi ingejikita kuyatwaa hayo maeneo ya Ukraine mashariki toka awali huenda wangeshayatwaa na wasingeangukia kwenye fedhedha waliyonayo hivi sasa hasa baada ya kushindwa kuiteka Kyiv.View attachment 2232150
kamanda wa kikosi cha Azov akiwa dhoful hal.Wale makamanda wa awali walifanya njama na Urusi na kukimbia
Kamanda mkuu wa kuilinda Azovstal Denys Prokopenko ambaye alibaki kwenye mahandaki baada ya kundi kubwa la askari wake kujisalimisha nae ametoa tamko rasmi la kukataza upinzani wa aina yoyote dhidi ya jeshi la Urusi akitoa sababu ili kuokoa maisha na kulinda siha za waliobaki hai.Wakati huo huo amesema wamo katika juhudi za kuwatoa wenzao ambao ni maiti ili wakazikwe.
Kwa upande mwengine jeshi la Ukraine limetangaza kuwa jeshi la Urusi limesonga mbele kwa kasi katika mipaka yote ya jimbo la la mashariki la Donest.Kauli hiyo inaenda sambamba na msemaji wa jeshi la Urusi ambaye muda mfupi uliopita amesema jeshi lake liko karibu kabisa kulidhibiti eneo lote la Luhansk huko huko mashariki ya Ukraine ambalo kwa wiki mbili sasa limekuwa kitovu cha mapigano makali.
Dawa ya drones imepatikana Kieve ipo mdomoni sasaKama Urusi ingejikita kuyatwaa hayo maeneo ya Ukraine mashariki toka awali huenda wangeshayatwaa na wasingeangukia kwenye fedhedha waliyonayo hivi sasa hasa baada ya kushindwa kuiteka Kyiv.
lee van cliff idawa
Habari kama hii, wanafiki BBC huwezi kuona wakitangaza.[emoji298][emoji298][emoji298]ITALY (Genoa). Demonstrations by Italians against NATO. https://t.co/Rx6zuhYuZI
Taarifa za muda mchache uliopita zinaonyesha hali inazidi kuwa mbaya kwa jeshi la Urusi, kwa sasa ina upungufu mkubwa wa wapiganaji, kutokana na wanajeshi wengi wa Urusi kuuawa kwenye Vita ya Ukraine, hali hiyo imepelekea Bunge la Urusi kujadili mswada utakao waruhusu wazee na Raia wa Kigeni kujiunga na Jeshi kwa ajili ya Vita ya Ukraine. Hii ni fedhea kwa Jeshi la Urusi ambayo inajinasibu kuwa na Jeshi kubwa duniani.
Safari hii lazima Putin Afundishwe adabu na ndo kwaanza mapema kabisa hadi November nazani akili itakuwa imemkaa sawa.
________________________________________
Bunge la Russia linatarajiwa kujadili mswada utakaoruhusu raia wenye umri wa zaidi ya miaka 40 na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo wenye umri wa kuanzia miaka 30 kujiunga na jeshi.
Hatua hii ni ya Russia kuimarisha mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, baada ya kupoteza wanajeshi kadhaa katika vita vinavyoendelea.
Taarifa iliyoandikwa kwenye wavuti wa habari za serikali ya Russia, Duma, imesema kwamba hatua hiyo ni ya dharura, inayolenga kutumia ujuzi wa watu wazee wenye uwezo wa kivita.
Kwa sasa, wanajeshi wenye umri wa kati ya miaka 18 na 40 ndio wanaoruhusiwa kujiunga na jeshi la Russia.
Russia imepata pigo kubwa sana kwa kupoteza wanajeshi na silaha katika vita vya siku 86 sasa, ambapo Ukraine umefanikiwa kuwashawishi raia wake kupigana na kupinga uvamizi wa Russia.
Japo Russia imedhibithi Mariupol, imeshindwa kufikia malengo yake katika vita hivyo pamoja na kushindwa kudhibithi Donbas, mashariki mwa Ukraine.
Wakati huo huo, waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu amesema kwamba Russia imeanda kuunda vikosi 12 vya jeshi katika sehemu za magharibi, kwa matayarisho ya kile ametaja kama vitisho vinavyoongezeka katika sehemu hiyo, akisema vinatokana na Finland na Sweden kuomba kuwa wanachama wa NATO.View attachment 2232267
Sio hivyo tu,wamezuia wanaume chini ya miaka 60 kutoka nchini Ili wapambane,Sasa wakishushiwa moto wanalialia kuwa ni Civilians!!!!Tupe update za uwanja wa vita.sio kutuletea ngonjela.unashangaa vipi kwa WARUSI wakati yule bwana yeye alitangaza kuwa mtu yoyote yule akitaji kushika silaha kwa ajili ya jeshi la UKRAINE anapewa nauli ya kufika UKRAINE na uraia juu