Sijaipenda kabisa move hii ya pili.
Urusi imevamia Ukraine kijeshi nchi hiyo kwa kutumia majeshi ya anga,ardhini na nchi kavu.
Wamevamia kutoka Kila upande wa Ukraine.
Wanajeshi wa Urusi walionekana wakiingia mijini kutoka Kila upande.
Urusi imevamia Ukraine yote.
sio Tena majimbo yanayotaka kujitenga ya Donestk na Luhansk.
Jeshi la Urusi limevamia kwa kulenga na kupiga miji mikubwa kama Kiev,mariupol,Kharkiv,Odessa na Kramatorsk.
wenyewe Urusi wanasema wamepigwa sehemu za kijeshi TU na wala hawatashambulia maeneo ya kiraia.
Putin amesema lengo ni kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Ukraine.
Nimeshuhudia kupitia tv jengo moja kubwa nje Kuna askari wa Ukraine wanachoma nyaraka,mtangazaji anasema huenda ni jengo la Kijasusi. Helkopta za Urusi zimaonekana kutawala katika miji iliyovamiwa.
Karibu Mkuu wa NATO akijibu maswali amatanabahisha kuwa NATO haitapeleka wanajeshi wake. Marekani imelaaani na rais wa Marekani anaiombea kwa Mungu Ukraine katika kipindi hiki kigumu.
Waziri Mkuu wa UK amesema vikwazo vikali vitaongezwa.
Putin anasema hii ni Special operation yake ni kwa ajili ya "kui "neutrilize country's military capacity," kuiodhiofisha kijeshi Ukraine.
Rais wa Beralus amesema majeshi yake hayajaingia Ukraine kuongozana na Urusi ila yakihitajika yataingia.
Aisee hii Dunia haiko swa kabisa. Ukweli ni kwamba majeshi ya Urusi yanajipigia TU Kila yanapotaka
NATO wamemtosa Ukraine, Stoltenberg karibu Mkuu wa NATO anasema NATO jukumu lake ni kulinda Wanachama wake haitaingiza jeshi. Sasa sijui walipokua wanasogeza majeshi sijui walikua wanafikiria nini.sijui walipeleka ili kupiga picha!
Marekani kamtosa Ukraine,
Uingereza kamtosa ukraine.
Kusema kweli kutoka moyoni huruma imeniingia sikupenda move hii ya pili.