Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kwanza fahamu Cuban missile Crisis ilitokea wakati wa vita baridi kati ya West na USSR, haikubuka tu kwa sababu Cuba ilikuwa inajichagulia rafiki.

Pili fahamu huo mgogoro ulikuwa unahusisha silaha za nyuklia, USSR ilikuwa inataka kwenda kuweka silaha za nyuklia mikononi mwa wakomunisti walikokuwa na ugomvi mkubwa na Majirani zao US.

Tatu katika huu mgogoro wa makombora Marekani haikupeleka majeshi yake kuivamia Cuba ila deal na USSR moja kwa moja, makabuliano yalifikiwa kati yake na USSR.

Baada ya maelezo haya yote. Swali lako linuhusianaje na Urusi kuivamia Ukraine??
Tuanzia na Cuba crisis ile ya base ya Russiq hebu tutoe tongotongo. Why it was an issue iwapo Cuba a sovereign state alikuwa anaweza kumchagua yeyote awe mshirika wake?
 
So ni mambo ya kawaida tu kuwa na hofu na inaruhusiwa kuchukua hatua kujilinda. Kwani unaweza kumpangia Ukraine eti asiweke siraha za Nuklia akishakuwa mnato?
 
Very good! Naona unajileta,weka makubaliano hayo Kati ya US na USSR,na ni kwanini US ihangaike na hayo makubaliano ikiwa iliona ilichotaka kufanya USSR sio tishio?
 
Kama utakuwa umefanikiwa kumaliza kidato cha nne utakuwa ulifundushwa overpopulation kwenye somo la Geography.

China baada ya kuona population yao inaongezeka kwa kasi huku kasi ya maendeleo ikiwa ndogo waliweka sera ya mtoto mmoja mwaka 1980 "one child policy". Walipaswa wawe na sera ya population muda mrefu kabla ya 1980 ili kuepuka sera kama hiyo ila walipokuja kushtuka ongezeko la kasi la population yao litakuwa tatizo kubwa likiendelea ndipo wakaja na hiyo sera ambayo ilitekelezwa kwa ukatili mkubwa sana.

South Sudan ni taifa changa lilitoka vitani muda sio mrefu na bado sasa hivi wanapigana wenyewe kwa wenyewe.
Kwa hiyo kuna mahusiano chanya makubwa kati ya population na resource utilisation?. China wamewezaje sasa au why South Sudan wamefeli?.
 
Ni kuvuana nguo kwa kweli

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Cuba haikuvamiwa na US. Mfano wako haufananii.
 
Kwani Ukrane imevamiwa na Urusi kwa sababu gani?

1.Kwa sababu ilitaka kujiunga NATO?
2.Kwa sababu kuna wanazi na kufanya denazification kama Putin alivyodai?
3.Kwa sababu ya biolabs?
4.Kwa sababu ilikuwa sehemu ya Russia kama vilaza wengi wanavyoamini?

Ukijibu hili swali ndio nitaweza kulielewa na kulijibu swali lako.
So ni mambo ya kawaida tu kuwa na hofu na inaruhusiwa kuchukua hatua kujilinda. Kwani unaweza kumpangia Ukraine eti asiweke siraha za Nuklia akishakuwa mnato?
 
🇵🇰 | On Saturday Pakistan decided to directly import two m metric tonnes of wheat from Russia while dropping a barter trade plan, as it also approved Rs160 billion supplementary grants to ensure an uninterrupted supply of food, fuel & electricity. 🌾🇷🇺
 
Hayo maneno na tuhuma za jumla havina mashiko, leta mfano mmoja mmoja tuuchambue na tuone kama unafanana na hata unakaribiana na uvamizi wa Russia kwa majirani zake kama Ukraine.
Huu ndio ujuha mwenyewe kutaka kutetea uvamizi wa Marekani uonekane ni halali ila wa Urusi ni haramu.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa hakuna taifa lenye haki ya kulivamia taifa lingine kwa sababu yeyote ile zaidi ya kujibu shambulizi baada ya mipaka yake kushambiliwa.

Uvamizi unao fanywa na Marekani na Urusi kwenye nchi za watu wote ni haramu ila kwenye masilahi ya mataifa makubwa sheria za kimataifa huwa hazina nafasi.

Kwa hiyo usijitoe akili.
 
My point is hao wazungu wameiunderdevelep Africa kwa kubeba strong, health na elite people from Africa kwenda kuendeleza kwao huku kwetu wakiacha watu dhaifu,wanawake na watoto na puppets wao.
Hivyo basii biashara ya utumwa imetukwamisha sisi watoto wa Africa na nadhani hadi mpaka sasa madhara bado yapo watu hawajiamini kama wanaweza.
 
Sababu zote.
 
MRAPs za Urusi zote zile kina Typhoon na wenzake zina limitations. MRAPs nyingi zimeundwa kuzuia milipuko isiyozidi 6kg of TNT. Kuna nchi ya Ulaya nadhani ni Uingereza inayo aina moja mpya ya MRAP ni very expensive inazidi hata their most advanced MBT. MRAPs hazijatengenezwa kutoharibika ila lengo lake ni kuzuia wanajeshi waliomo ndani kufa gari likikanyaga mine au kushambuliwa. Ziko protected against mines na blast shockwaves, chassis yake pale chini iko V-shaped inasambaza shockwaves pembeni na walioko ndani hawajigongi pembeni au kuvuja damu puani. Hivi vifaru vya Urusi unavyoona vinalipuka turret na kuruka juu hata kama crew haijafa yote ila anayetoka pale hasikii tena na atakufa kwa shocks alizopata.

Israel kuna kampuni sikumbuki kama ni Rafael Defense ina teknolojia mpya ya chassis za MRAP inauza, kuna consortium ya Spain na wazungu wenzake ndio wako kwenye mchakato wa kununua ila gharama kubwa.
 
Kwa hiyo tukiwa na mtoto mmoja afrika tuatendelea?. Achana na mambo ya kupangiwa maisha eti zaa mmoja sijui upate maendeleo. Ndio maana sasa mpo na sera ya kutoa mimba.
 
Wala hakuna mtu anayeichukia nchi nyingine...Unachukiaje nchi kwa mfano??Nchi ina vitu vingi sana au variables nyingi sana....watafanya vizuri kwenye hiki, watazingua kwenye kingine....kama kwenye ngazi ya familia tu...kuna utofauti..sembuse mataifa ambayo kuna mamilioni ya watu.....Hivyo huwezi kugeneralize kuchukia nchi, labda kama upo irrational...

Again....Afrika tutapiga hatua kama tutakuwa na competent leaders tu...kama ulivyosema hapo...lazima tuwe na maslayi yetu.....Viongozi wanatoka kwenye jamii zetu..kuanzia ngazi ya familia, mashuleni n.k..kama wewe kwa mtazamo wako huo..KUWA U.S na WESTERN Europe ndo kama miungu....hatuwezi kutengeneza hicho ulichokiongea hapo..

Hakuna chakula cha bure duniani..AFRIKA HATUWEZI KUTEGEMEA U.S, CHINA, EUROPE, RUSSIA etc kwa ajili ya maendeleo yetu....Tunapaswa tujisimamie sie na tuwe na malengo au maono..na interests zetu ambazo zitatuongoza kwenye maamuzi mbalimbali hasa linapokuja suala la kudeal na mstaifa ya nje.......
 
Haya madude yanapunguza sana vifo na majeruhi ila kuyahudumia ni gharama kubwa Sana.

Vile vifaru vya 'Abrams' vina uwezo wa kuhimili shambulizi na crew wakibaki hai, ila vina teknolojia ya juu kuviendesha, huenda ndio maana Marekani hawezi kuipa Ukraine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…