Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Cuba haikuvamiwa na US. Mfano wako haufananii.
Cuba haikuvamiwa na US kwa sababu ya busara za viongozi wa kipindi hicho..watu waliweka utu mbele, NATO wakaondoa makombora yao Turkey na USSR wakaondoa makombora yao Cuba..win win situation...

Viongozi wa kizazi hiki wamechangia huu mgogoro....hakuna anaekubali kukaa chini na kuongea na mwenzake, kibaya zaidi Western countries wanaishawishi na kuichochea Ukraine kukataa maridhiano...Unajua ni kitu gani kingefuata kama USSR ingeendelea na mpango wa kuweka makombora Cuba..US wangekiharibu kabisa hicho kisiwa..labda na kusababisha World war
 
Watu wanatafuta ugali wa watoto wao hawacheki na kima.
Russia we ndio mwanaume tunaekutegemea kwa sasa uwachallenge mazoea yamezidi.
Principle yao ile ile that, Arm every one and let them kill each other... Lau kama wangeijua history basi wasingeshududu upuuzi wanaouropoka sasa hivi.

They don't know who is in control, some think it's US regime, thou actually it's those who are behind US regime, that're Western elites. My dear, tell them hii ndio ramani ya US baada ya kupokea uhuru wao kutoka kwa "British".

800px-United_States_evolution.gif

Na hii chini ni US tunayoiona hivi sasa
united_states.jpg


Je, wanafaham safari ya hilo eneo hadi kufikia hii US tunayoiona leo ilivyokua mmmh? Hii Calif, Nevada, Utah, Arizona, New Mexico na Texas wanajua zilivyochukuliwa kutoka Mexico ya wakati huo?

Wanajua sababu kubwa ya Ugonvi uliopo kati yake US na Mexico hadi leo ikafika kitendo hadi Trump kutaka kujenga Ukuta kwenye mpaka wake yeye na jirani yake? Ni Drug Traffic au sio? He he he 😂

US ni taifa chotara, Ethnic yake ni mchanganyiko kwasababu lilikuwa shamba la utumwa, enzi hizo watumwa kutoka sehem tofauti duniani walikuwa wakipelekwa huko kutumikishwa kwenye mashamba ya wakoloni hawa wazungu wanaowashobokea mbaka leo.

Je baada ya Uhuru wanajua kile white supremacists walichokifanya kwa wahindi wekundu? Ok tufanye walikuwa hawajazaliwa, Je wanakifaham ambacho wameendelea kuwafanyia watu weusi hadi leo hii?

Again wanajua ni nani aliye'sanifu WW1 na WW2? Na lengo lake hasa lilikuwa ni nini? Baada ya kufanikisha alichokusudia ama kwa wale wanaofikiri walipewa uhuru bure, washawahi kujiuliza Isingekua kuyumba kwa uchumi kwa mataifa tawala hapo Ulaya baada ya WW2 wanajua wangekuwa na hali gani hivi sasa?

Baada ya kuvunjika kwq USSR, taifa lilobaki likichuana na US kiuchumi alikuwa Japan, wanaweza kutwambia huko kufreeze kwa Uchumi wa Japan hadi leo ni nini?

Tutumie number ieleweke, Japan GDP in 1991 ilikuwa $3.6T, 2000 ilikuwa $4.9T na last year was $5.2T. Upande wa China 1991 ilikuwa $384B, 2000 ilikuwa $1.21T na last year was $17.7T. So unaweza kuona how jina dictator linavyozaliwa na kuingia katika matumizi?

If that exponential growth of Chinese Economy was due to dictatorship na hiyo
stagnant of Economy ya Japan was due to democracy, Huh bas that's fantastic indeed.

Sogea afrika kwetu, Libya GDP in 1990 was $28.9B, kufikia 2000 ilikua $38.2B, na one year before NATO hawajachafua hali ya hewa ilikua $74.8B, lakini leo hii miaka 11 imepita tangu wamtoe yule wanayemuita Dictator na Libya GDP ni $51B, Mind you hii ni nchi tajiri wa Mafuta Afrika. Can you tell the difference under given two ideology?

Ok tuhame huko, Ingekuaje kwe huu mgogoro uliopo yeye na jiran yake US huyu Mexico, Russia na China waanze kumpatia Mexico silaha za kujilinda nae US atafeel vipi? Je, Hiyo nayo ni democracy?

Je, wanafaham kama J. F. Kennedy aliuliwa kwa mlengwa ule ule pale alipotaka kulitoa taifa lake kwenye mikono ya "wahuni"😂 mmmh?, Kama walifanya kwa kiongozi aliyepo madarakani kwenye taifa hilo hilo watashindwa kwenye mataifa mengine yanayoenda kinyume nae?

Usichoke tuendelee, Israel ni rafiki mshirika wa United State. Oh! Tizama hii picha revoultion yake ya wizi wa ardhi wa kutoka kwa wapalestine.

palestine_map.gif


As you can see hapo, hizo annexation anazozifanya Israel ni Copy ya aliyoifanya US miaka hiyo, Je hiyo nayo ni democracy, if not? Did you ever hear them condemn Israel juu ya anachokifanya? Did they ever told them ku-abide na democracy?

Hapo hapo tuwashtaki UN (Umoja wa mchongo huu) kwenye hiyo picha juu, utaona Illustration ya pili ya mipaa ni ile iliyowekwa na UN mnamo 1947, je mipaka hiyo ndio iliyopo sasa? 1947 hadi leo ni miaka 75. Ni kweli UN hawajaliona hilo ila la Crimea ndio waliloliona? Ulishawahi kusikia kuna taifa limempa vikwazo Israel?

Haiishii hapo tu... Saudia Arabia, Qatar, UAE hawa nao ni washirika wakubwa wa mmarekani. Their rulling system sio democracy but Ufalme ambao familia moja inatawala milele. Refer to democracy kua ni serikali ya watu, for the people to the people... Kwanini hawa hawaguswi kelele zipo Russia na China?

Yah, Simply because sio threat kwenye interest zao na wala sio Issue za demokrasia hapo.

Canada, Australia, New Zealand na Nchi zingine nyingi tu hapo Caribbean bado ziko under British Influence. Hizo nchi zina waziri mkuu tu kama kiongozi wa serikali lakini kiongozi wa nchi/Top Official ni Mfalme ama Queen wa Uiengereza. Kwanini hizo Nchi kubwa kama hizo zinabaki chini ya familia moja (Royal family) badala ya kupewa full sovereignty if kweli wanamaanisha wanayoyazungumza?

Wanatumia kigezo kipi kudai sehem flan kuna udikteta na sehem flan kuna democracy? Kwani Putin na Xin wamejichagua wenyewe? Kwanini kila anayepingana nao hafai?

Em turudi hapa Afrika, kuna nchi mbili hadi leo toka uhuru zimetawaliwa na Marais wawili tu. Anza na Cameroon kwa Paul Biya kisha njoo Equatorial Guinea kwa Teodoro Obiyang. Ushawah kusikia kuna Mzungu anapiga kelele au kuweka vikwazo kwenye nchi hizo kwasababu ya udikteta?

Kombe la CAF mwaka huu limefanyikia Cameroon, je Taasisi za michezo, Taasisi za haki za binadam umezisikia zikipinga kufanyika michezo hiyo kwenye hizo nchi ambazo hazina democracy?

Nakudokeze kidogo, Equatorial Guinea ni nchi yenye utajiri wa Mafuta, wanaochimba mafuta hayo nchini hapo ni ExxonMobil, Marathon Oil Corp, Noble Energy na Kosmos Energy. Zote hizo ni Kampuni za Marekani

Swali, Ikawaje anayejiita father of democracy akaenda kuwekeza (na sio kuwekeza pale wanaiba tu) kwenye nchi ya udikteta. Ambayo Kiongozi wake huyo Obiyang kafungua account zaidi ya 60 kwenye bank 1 US anakopokea malipo ya Mafuta hayo? So unaona aina ya viongozi wanaopendwa na hawa watu wala sio kelele za Democracy ama Udikteta?

Leo hii China sometimes na Korea, wanaigiza movies nyingi tumeziona kama sehem ya kuwafundishia kizazi chao namna walivyotawaliwa na Mjapan... Jinsi walivyosota na namna walivyojikomboa? Ujue kwanini? Wanalinda Historia, asiyejua anakotoka hawezi jua anakoelekea.

Je hivi leo sisi weusi tunaweza igiza Movies kama hizo kufundisha kizazi chetu tulikotoka na namna tulivojikomboa au ndio tutawachorea picha za nyani tuwaambie tumetokana na nyani na huko ndiko babu zao walikotoka hivo wakirushiwa ndizi wasishangae...?

Kwao there is so no such a thing as World peace kwenye ajenda zao bali creating chaos, Arm everyone then wanakaa pembeni muuane vizuri. Hawa ndio wako msitari wa mbele kutuambia Dini flani hivi ni mbaya kwasababu ilienezwa kwa nguvu, ubabe na upanga...

If that's true, sasa wanatakaje tuamini na hii democracy ni nzuri inayoenezwa kwa Chaos na mauaji ya watu kiasi hicho maeneo ambayo hawakubaliani na mfumo wao huo?

If really democracy ni uhuru wa kila jamii, rika ama kundi kufanya itakalo. Kwanini wanaopenda tofauti na wanachokihitaji wawe wabaya ilhali wanahubiri "freedom" kwa kila kundi kufanya wapendalo?

Na kwanini dada mkuu akimbilie Europe na Asia kueneza itikadi zake, kwani jiran zake hapo Mexico, Latin and South America hawaoni?

Anyway, niishie hapo tu. Hata kwa hayo machache najua sijapoteza mda wangu kuyaandika coz am talking with mtu anayejielewa 😂... Mdau kama Mdau, hatare sana.

Namaliza na hili kwa kuliandika kwa Herufi kubwa... wanaojua hongereni na kwasio jua tunawajuza kulikubali au kulikataa ni uhuru wenu pia, ni kwamba KILA MZALENDO, na ANAYETANGULIZA MASLAHI YA TAIFA LAKE KWANZA KABLA YA KILA KITU, MBELE YA BEPARI NI DICTATOR tu.

Dictator ana Umimi, hajadiliani na mtu. Anachokiangalia ni maslah yake tu na watu wanaomzunguka... Mzalendo ni yule anayetanguliza maslah ya taifa lake, jamii yake, Amejawa usisi sio umimi. Yupo radhi wakati wowote kutetea maslahi ya walio wengi na sio kikundi kichache au ya kwake binafs.

Na ukiizingatia hiyo tafsiri utagundua ule upande wanaodai wana democracy ndio hawa madictator na huu upande unaodaiwa kua udikteta ni ule upande uliojaa wazalendo tupu.
 
Rasmi, Ukraine imeanza Kupokea Makombora hatari ya harpoon ambayo yatakuwa na uwezo wa kupiga hadi Moscow.

Urusi itegemee Upinzani mzito kwenye Mapigano baada ya Ukraine Kupokea Makombora haya.

Je, tutarajie Ukraine kuanza kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi.

______________


Ukraine yaanza kupokea makombora hatari ya Harpoon kukabiliana na Urusi

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksii Reznikov amesema Ukraine imeanza kupokea makombora ya kivita aina ya Harpoon kutoka Denmark na ndege za zisizo na rubani kutoka Marekani.

"Ulinzi wa pwani wa nchi yetu hautaimarishwa tu na makombora ya Harpoon - yatatumiwa na timu zilizofunzwa za Ukraine," Reznikov aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Reznikov alisema usambazaji wa makombora ya Harpoon ni matokeo ya ushirikiano kati ya nchi kadhaa.

Ukraine imekuwa ikiomba silaha za kisasa zaidi lakini hadi sasa misaada mingi imekuwa katika mifumo ya masafa mafupi kama vile silaha za kukinga vifaru.

Marekani inazingatia ombi kutoka Ukraine kuipatia Kyiv silaha nzito za masafa marefu lakini bado haijafikia uamuzi wa mwisho.

Chanzo REUTERS, Aljazeera, BBC

Hapa Chini ni kombora la harpoon [emoji116]View attachment 2243356
Sio kweli bro acha Fix. Harpoon Missiles na Standard Missiles (SM-6) Ni Anti-Ship and Ant-Submarines Missiles. Kazi Yake Ni Kulipua Meli na Nyambizi za Kijeshi umbali wa Kilometa 120. Makombora yenye Uwezo wa Kufika Moscow Ni ATAMCS Missiles ambazo Zinarushwa kutoka kwenye Multiple Lunch Rocket System(MLRS) zenye Uwezo wa Kufika Mile 200 Sawa na 320Km. Hizo Katu Marekani hawezi kuzipeleka Ukraine,Mark My Words.
 
Hoja ya kujiunga NATO inakufa hivi,
1.Ukraine haijwahi kutangaza inataka kujiunga NATO. Sio kwenye uvamizi huu au ule uliofanywa mwaka 2014 na Russia. Hakuna rekodi ya kiongozi yeyote wa Ukraine kusema au kuandika Ukraine inataka kujiunga NATO. Finland ambayo ina mpaka mkubwa na Urusi kuliko Ukraine imepeleka maombi rasmi ya kujiunga NATO na mpaka sasa hakuna hata bomu moja lilirushwa Helsinki.

2.Hoja ya Unazi nacho ni kichaka dhaifu mno kwa Putin kwa sababu Zelenskyy mwenywe ni Myahudi na hadi babu zake waliuwawa kwenye Holocaust, ni kituko kufikiria mtu wa aina hiyo anaweza kuwa na mafungamano au ku support watu wa aina hiyo.

Hakuna ushahidi wa hao wanazi kama walikuwepo na pia hata kama kweli walikuwepo Ukraine au sehemu nyingine Ulaya walikuwa kitisho kivipi kwa usalama wa Russia. Na je hao wanazi ndio waliosababisha aivamie nchi nzima?!

3.Hakuna ushahidi wowote wa biolabs, Russia wenyewe hawajaisema hii sababu na hito hizo biolabs haieleweki ni kitu gani kwa nyie Pro-Russia mna demka tu kuielezea hii conspiracy ya biolabs na mambo mengine ya mnayohusisha nayo huu uvamizi kama ushoga.


4.Hii sababu ya nne wachambuzi wengi ndio wanaamini ni sababu kubwa ya Putin kuivamia Ukraine.
Eti kwa sababu anaamini Ukraine sio nchi kamili. Pia ana ndoto yake ya muda mrefu ya USSR ya kale na kuanza kujenga umoja wa aina ile kuizunguka Russia

Hii ndio sababu kubwa japo ni ya hila, ina uongo mkubwa ndani yake na ni ya kipambavu.

Kila nchi ikianzisha vita kudai sehemu inayodai ilikuwa yake kijiografia huko zamani katika historia au kulazimisha miunganiko kwa nguvu za kijeshi huu ulimwengu hautakalika tena. Utakuwa uwanja wa fujo tupu, hiyo inafanya uvamizi wa Putin kwa sababu hii kuwa haramu na unaopaswa kulaaniwa na mtu yeyote mwenye akili.
Sababu zote.
 
Unataka kuniambia kwenye hizi Abram crew walipona?.kama walipona basi hao watu walikuwa wa chuma
Haya madude yanapunguza sana vifo na majeruhi ila kuyahudumia ni gharama kubwa Sana.

Vile vifaru vya 'Abrams' vina uwezo wa kuhimili shambulizi na crew wakibaki hai, ila vina teknolojia ya juu kuviendesha, huenda ndio maana Marekani hawezi kuipa Ukraine.
images%20(40).jpeg
images%20(38).jpeg
images%20(39).jpeg
 
Mkuu usilete vitu ambavyo haviendani na mada plz, watanzania wengi walimchukia jiwe sio kwasbb walipenda wazungu sanaa hapana jiwe was a homicidal dictator, lakini katina development model yake hakuiweka wazi hata hivyo asinge kufa na natural death Wazingu wangemfanyia chochote aahindwe tu, US na EU sio wezio, wenyewe wanata tubaki na hi underdevelopment level,...... US hajawahi kutowa msaada wa $40bn kwa nchi yoyote Africa, lakini kwa hi Ukuraini ametoa zaidi ya hiyo ndani ya mda mfupi........kuepo kwa US na umoja wa Uleya sahau maendeleo ya Africa,
Jamani msilete mijadala isiyo na tija kwenye uzi huu...ninavyofahamu Mimi uzi huu ni wa Russia-Ukraine war...Sasa hii eti sijui Watanzania wengi walimchukia JPM na kwamba eti alikuwa a homicidal dictator inatoka wapi hi?! Is it true kwamba eti Watanzania wengi walimchukia JPM??!!! Na is it true that eti JPM alikuwa a homicidal dictator?!?!

Let us focus our debate kwenye vita vya Russia-Ukraine....
Isije kuwa Kuna baadhi wametumwa to divert our attention on/from what is going on in Ukraine...
 
Tukutane field!!!
====
Hivi mmeishasahau kilichowatokea US, France na UK kule Syria? Walijifanya kumshambulia Syria kwa missiles kutoka kwenye manoari na merikebu zao eti katumia silaha za kemikali kumbe ni wale wahuni wa White helmets ndiyo wamefanya igizo!

Wote kwa Pamoja walipanga kurusha zaidi ya missiles 250. Lakini zilizofanikiwa kurusha ni Karibu 110 na na Karibu zote zikidakwa na mitambo ya ulinzi wa anga wa Syria zikiwemo S-300. Wataalamu wanasema zile 250-110 missiles ambazo zilimisfire, inasemakana Russian electronic warfare technologies zilihusika kati hilo. Kumbuka Russia ana kituo cha kijeshi Magharibi mwa Syria muda mrefu. Tukio hili lilitokea 2018!

Kwa hiyo, hivi vitu vya range isiyozidi 300km sidhani kama vitamsumbua Russia.
Hii habari yako Ni ya kweli japo umeileta kiushabiki.kwanza Kati ya Makombora 110 yaliyorushwa na Manowari ya Marekani,Ni Makombora 30 TU yaliyotunguliwa,80 yalitua na kuharibu ghala la Silaha la Syria.

Swali langu kwako

Trump alipotangaza kuwa Marekani itashambulia Kambi za Jeshi la Syria ambalo lilihusika na Matumizi ya Silaha za Sumu,Urusi ilitoa onyo kuwa Endapo Marekani itaishambulia Syria Basi Urusi itashambulia Kule ambako Makombora hayo ya Marekani yatakuwa yametokea. Sasa tueleze,Je,baada ya Meli ya Marekani kushambulia huko Syria,Urusi aliishambulia hiyo Meli ya Marekani?
 
Cuba haikuvamiwa na US kwa sababu ya busara za viongozi wa kipindi hicho..watu waliweka utu mbele, NATO wakaondoa makombora yao Turkey na USSR wakaondoa makombora yao Cuba..win win situation...

Viongozi wa kizazi hiki wamechangia huu mgogoro....hakuna anaekubali kukaa chini na kuongea na mwenzake, kibaya zaidi Western countries wanaishawishi na kuichochea Ukraine kukataa maridhiano...Unajua ni kitu gani kingefuata kama USSR ingeendelea na mpango wa kuweka makombora Cuba..US wangekiharibu kabisa hicho kisiwa..labda na kusababisha World war
Mgogoro wa Cuba hakuanza na wala haukuwa unahusu makombora ya Marekani barani Ulaya. Huo mgogoro chanzo chake ni ugomvi kati ya Castro na US kufikia uhasama wa juu. Castro ndiye aliyeenda kumuomba Khruhschev wa USSR kweka makomba kisiwani kwake na sio kinyume chake.
 
Cuba haikuvamiwa na US kwa sababu ya busara za viongozi wa kipindi hicho..watu waliweka utu mbele, NATO wakaondoa makombora yao Turkey na USSR wakaondoa makombora yao Cuba..win win situation...

Viongozi wa kizazi hiki wamechangia huu mgogoro....hakuna anaekubali kukaa chini na kuongea na mwenzake, kibaya zaidi Western countries wanaishawishi na kuichochea Ukraine kukataa maridhiano...Unajua ni kitu gani kingefuata kama USSR ingeendelea na mpango wa kuweka makombora Cuba..US wangekiharibu kabisa hicho kisiwa..labda na kusababisha World war
Wapi Western countries wanachochea Ukraine kukataa maridhiano?. Kinyume chake US hata kabla ya vita walitoa tahadhari kuwa Urusi inataka kuvamia Ukraine, lakini Putin akasema huo ni uwongo. US aka share intelligence info kwa siri na China ili iishawishi Urusi isivamie lakini China walivyo wapuuzi na yenyewe ikasema uongo na wakaambia Urusi eti US wanasema mnataka kuvamia Ukraine.
 
Mkuu javelin ndio iliyomuhamisha Mrusi mji wa Kyiv ndio mana mpaka leo Kyiv heshima imetawala, US amesharudisha ubalozi wake na watoto wameanza kucheza na kupiga picha picha kwenye kwenye masalio ya vifaru vya russia vilivyochachagwa ni hiyo javeline na stinger

Kwamba huko anakokamata maeneo mrusi Javelin haziwezi kwenda ili zimuondoe kabisa? Hadithi nuingine bana.
 
Urusi kama alikuwa anataka tu kuwasaidia wanaojitenga angeingia maeno yao waliokuwa wanataka kujitenga sio nchi nzima kama alivyofanya.

Hicho kinachoitwa kutaka kujitenga kwa maeneo ya Mashariki ya Ukraine ni propaganda ya Russia tu iliyoanza mwaka 2014 baada ya Rais Yanukovych ambaye alikuwa ni Pro-Russia alipoondolewa madarakani kwa maandamano ya raia nchi nzima baada ya kukataa kusaini mkataba wa biashara na EU uliopitishwa na bunge la Ukraine. Hicho ndicho kilichomuuma Putin kupoteza puppet wake muhimu Kyiv na akaanza kufanya vurugu Crimea na maeneo mengine ya Ukraine kisha akaingiza majeshi huko na sababu kubwa ya kushindwa kuzuiwa wakati huo ni serikali ya dhaifu ya Ukraine

Baada ya hapo EU na USA waliwekeza pesa nyingu na utaalamu kuijenga serikali ya Ukraine na jeshi lake, Putin ameona Ukraine ikizidi kuimarika hataweza tena kuifanya koloni lake ndio maana akaivamia nchi nzima wakati huu kwa lengo la kuweka tena Puppet wake Kyiv, aliposhindwa lengo kuu akahamishia nguvu mashariki ili aigawe hiyo nchi asitoke mikono mitupu.
Tuanzia na Cuba crisis ile ya base ya Russia hebu tutoe tongotongo. Why it was an issue iwapo Cuba a sovereign state alikuwa anaweza kumchagua yeyote awe mshirika wake kama leo Ukraine anavyotaka kuingia NATO na Europe?
Halafu je nchi kuomba kujitenga na kusaidiwa ni mara ya kwanza mfano South Sudam etc.
Nchi ikiwa na kiongozi dikiteta kwa mujibu wako je ni mbaya kuwasaidia wananchi kama Libya? Je zile tuhuma za NAzi na utesaji wa watu Donbas ni za kupikwa na Russia sio za kweli?
 
Wapi Western countries wanachochea Ukraine kukataa maridhiano?. Kinyume chake US hata kabla ya vita walitoa tahadhari kuwa Urusi inataka kuvamia Ukraine, lakini Putin akasema huo ni uwongo. US aka share intelligence info kwa siri na China ili iishawishi Urusi isivamie lakini China walivyo wapuuzi na yenyewe ikasema uongo na wakaambia Urusi eti US wanasema mnataka kuvamia Ukraine.
Kabla ya vita hii....Huyo kiongozi wa Urusi aliainisha mambo ambayo kwao Urusi ni Redline.....Offcourse demand zilikua kali sana lkn ulikua mwanzo wa kukaa chini ns kunegotiate, Ukraine kupewa silaha na kumjenga kwa maneno kuwa asikubali na kuchochoe mgogoro tu.......
Waziri wa mambo ya nje wa UK anasema kabisa hakuna kuongea..ni kutoa silaha na lazima Urus washindwe..Kiongozi pekee aliyejitahidi ni Macron kidogo na Erdogan...nao wamekosa support..wengine wote hamna kitu

Asili ya huu mgogoro ni hao hao WESTERN powers na Maidan revolution 2014...waliratibu kumtoa madarakani Yanukovich...raisi aliyechaguliwa kihalali kabisa...kwa sanduku la kura kabisa..kisa tu alikua mtu wa east na alipendelea zaidi ukaribu na watu wa Urusi...
 
Aya yako ya mwisho imejaribu kuelezea ukweli ila kizandiki na kwa shingo upande.

Sema wazi sababu za Yanukovych kuondolewa madarakani mwaka 2014 kwa maandamano nchi nzima na raia wake ni yeye kukataa kusaini mkataba wa biashara na Umoja wa Ulaya uliopitishwa na BUNGE la Ukraine kwa sababu ya presha ya Russia aliyekuwa mfadhili wake mkubwa na maslahi yake binafsi ya kibiashara.
Kabla ya vita hii....Huyo kiongozi wa Urusi aliainisha mambo ambayo kwao Urusi ni Redline.....Offcourse demand zilikua kali sana lkn ulikua mwanzo wa kukaa chini ns kunegotiate, Ukraine kupewa silaha na kumjenga kwa maneno kuwa asikubali na kuchochoe mgogoro tu.......
Waziri wa mambo ya nje wa UK anasema kabisa hakuna kuongea..ni kutoa silaha na lazima Urus washindwe..Kiongozi pekee aliyejitahidi ni Macron kidogo na Erdogan...nao wamekosa support..wengine wote hamna kitu

Asili ya huu mgogoro ni hao hao WESTERN powers na Maidan revolution 2014...waliratibu kumtoa madarakani Yanukovich...raisi aliyechaguliwa kihalali kabisa...kwa sanduku la kura kabisa..kisa tu alikua mtu wa east na alipendelea zaidi ukaribu na watu wa Urusi...
 
Back
Top Bottom