LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums




Dunia aombe tu Putin asifanye makosa akabonyeza kitufe, maana US akijibu dunia itakwisha.

Ila Russia akirusha hilo uharibifu wake kama inavoonyesha ni mita 600 upana wake.
 
Umesahau Iran na Pakistan.
 
Hakika umedadavua vyema sana mkuu, mbinu za USA ni kutengeneza kibaraka kwanza, ikumbukwe aliweza kuiharibu USSR, baadaye akaziingiza NATO nchi zilizokua members wa USSR, na sasa anataka kuhitimisha kwa Ukraine. Kwa watu wanaoona mbali hii ni hatari sana kwa ustawi wa Urusi.

Hivi Russia akitengeneza coalition na venezuela pamoja na cuba USA atakubali? Kwa hili Putin anaonewa. Na ipo siku hata nchi za ulaya zitageukwa na USA.
 
Hivi mbona Watanzania huu ugomvi wa Putin na Ukraine mumeuchangamkia na kuunda teams, mnatoleana mapovu baina yenu hata kuzidi wenye ugomvi wao kule.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hata ugomvi wenu na AL SHABAAB tunauchangamkia.
 
Urusi muda huu anashusha kichapo kwa UKRAINE.
Binafsi ningewaomba UKRAINE waweke silaha chini, nchi yao inakuwa uwanja vita. Itakuwa kama BOSNIA sasa.
 
Urusi muda huu anashusha kichapo kwa UKRAINE.
Binafsi ningewaomba UKRAINE waweke silaha chini, nchi yao inakuwa uwanja vita. Itakuwa kama BOSNIA sasa.
Majeshi ya Russia sasa hivi yapo kilomita 13 kutoka Kyiv.

Ni kama kutoka Posta Mpya na Oysterbay pana kilomita 10 hivi.

Weye ongezea hapo hizo kilomita 3 hivi.

Jenerali mmoja wa US mstaafu ameonya kuwa Russia itaua raia wengi sana endapo itachukua Kyiv.

Amesema Russia ni wajuvi wa vita ya mtaa kwa mtaa yaani Urban Warfare.
 
ndio nnchi pekee duniani tunaojua kila jambo tunawatafiti humu nawapiganaji wavita wazuri kabisa nawaitaga #wachambuzihuru

Uchambuzi sawa, ila pitia huu uzi uone watu wanavyotoleana povu mpaka basi, watu wamejiunga kwenye milengo na timu hadi nacheka sana, kunao mpaka wanatukanana humu aisei.
 
Uchambuzi sawa, ila pitia huu uzi uone watu wanavyotoleana povu mpaka basi, watu wamejiunga kwenye milengo na timu hadi nacheka sana, kunao mpaka wanatukanana humu aisei.
Mkuu achana nao hao.

Pata vitu vya uhakika kutoka kwa wachambuzi huru.

Mimi nipo hapa Kibaigwa nafuatilia kwa makini.

🙂
 

Ninachojua na hata ukisoma historia ya Urusi, yeye huwa hajali hata ukiua wanajeshi wake kwa maelfu na malaki, ataendelea kuleta more and more na ndio mbinu alifanya kwa Hittler, Warusi waliuawa zaidi ya milioni 24 na hawakusitisha vita.
Japo simpendi Putin na nawachukia sana hao Warusi kwa hicho wanachkifanya huko, ila Ukraine akubali tu yaishe, maana Putin yupo radhi kurubuni maelfu ya wanajeshi wake ila asiingie aibu ya kushindwa.
 
Unayajua mavi ya kuku!? Basi ulichoandika hapa ni mavi ya kuku.
 
Ukiangalia sana waona kuwa yeye huona matokeo ni muhimu kuliko hali halisi (kwamba watu wengi wauliwa).

Ndo maana hata kule Syria walimwachia Putin awamalize wale waasi walokuwa wakisaidiwa na USA na nchi za magharibi waloitwa Syria Free Army kutaka kumwondoa Asad.

Putin akaenda akamaliza kazi na sasa bado yupo kule.

Venezuela ni hivyohivyo kaenda na yupo kule.

Halikadhalika kule Mali kaingia kwa kuwapeleka Wagner Group wamsaidie kiongozi wa sasa wa Mali na kumlinda dhidi ya uwezekano wa assassination from those guys.
 

Huwa nafuatiilia sana historia ya vita vya pili vya dunia na namna Stalin aliwarubuni Warusi, he literally threw bodies at Hittler, mpaka nchi ikawa na wajane wengi kiasi cha wanaume kuadimika kwa kipindi kirefu, hiyo sio nchi ya kuingia nayo kwenye ugomvi wa kivita.

Marekani pale Vietnam alipoona body county imezidi, aliamua kugeuza kwa aibu, ila kwa Mrusi utaua mpaka utachoka mwenyewe lakini wataedelea kuja. Mrusi wa kawaida huonwa kama mali ghafi ya kutumika na oligarchy.
Japo Ukraine pia ni uzao huo huo, na wao inawezekana wakaamua kufa hadi wa mwisho, sipendi kinachotaka kutokea huko.

Wakae wayaongee, nafuatilia sana commens za Warusi kule Quora, wengi hawataki hii vita.
 
Hata Russia amefunga Facebook na Twitter huko kwake ili raia wake wasijue kinachoendelea

Amefunga sabanu fb na twitter wanafuta update za urusi na wanaruhusu chart ya kuhimiza maandamo urusi na sehwku nyingine hata mimi ningewafuta

Yukraini kipigo kiko pale pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…