Mkuu haya madini,bado natamani "kitabu"
Please....
Ha ha ha happpana Mkuu, kweli ase me sio mwandishi mzuri, basi tu hizo mambo huwa zinajazana kwa kifua zikipata mwanya zinatoka kama hivyo katika reply kadha wa kadha za rafiki zangu hapa JF...
Nimerudia kuisoma kwa mara nyingine, Mwamba hapo kwenye mafuta ya kujipaka naamini hujaitamka holela. Kuna kitu, kama hutojali unaweza kushare, nimewaza ulimaanisha nini nimekosa majibu.
We nae mdadisi eishiii 😂
Of course sikulitamka bahati mbaya, Kivipi? Ni hivi, kwanza nianze kwa kujipambanua mie sio medical specialist. Nitakachokueleza ni kile nachokijua so far katika ufatiliaji wangu wa issue za Afya kwa ujumla.
Mafuta kawaida yametengenezwa kwa ajili ya ngozi nadhani hili linafahamika wala halihitaji maelezo mengi. Ukiichukua kopo la mafuta ya kujipaka utakuta maelezo yapo hapo yakikuambia au kukuhusia kuhusu kuyaweka mbali na watoto. Kwanini mtoto? Kwasababu mtoto anaweza kuyaweka mdomoni.
Ok now tuachane na huyo mtoto turudi kwako mtu mzima. Nadhani ushawahi osha vyombo katika ukuaji wako kama hujawahi basi we mtoto wa kishua.
Na najua pia Katika osha osha ya vyombo ushawahi kuosha bakuli la mchuzi wa nyama au sufuria lililokuwa na mafuta.
Katika uoshaji wako bila kutumia maji ya moto nadhani wajua hali ya sufuria au bakuli itakavyokua.... Kwamba yale mafuta huwa hayatoki.
Sasa hali hiyo unakutana nayo baada ya kujipaka mafuta ukifika wakati wa kula. Most katika sie hasa tunaopaka mafuta mazito kisha tunanawa maji ya baridi huwa tunabaki na yale mafuta mkononi.
Ambayo later "tunayafinyanga" kwenye tonge la ugali tunaweka mdomoni. Hii ni continuously kwenye daily routine.
Again kwa mkeo sijui mchepko wako huko. Katoka zake kujipodoa mkononi kajaa kila aina ya mkorogo na kwasababu akishayapaka hayaonekani basi ajisuuza vidole kisha anamlisha mtoto, Je Unajua anamlisha vingapi wakati huo 😆😆😆?
Ni wachache sana ambao hutumia maji ya moto wakati wa kunawa kabla ya kula ili kusafisha mikono vizuri.
Sasa hii daily consumption ya Petroleum products "indirectly" mwilini tushajiuliza ina madhara gani? Kwanini ni sie tu tunaojiita modern world ndio tunakumbwa na haya magonjwa ya ajab ajab?
Ha ha au basi tu, maana kuyaeleza haya itakuwa kama tunatishana hivi, so tuyaache tu.