LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Kwa jinsi ilivyo its better akae na urusi atafute suluhu kuliko kuruhusu nchi yake kugeuka uwanja wa vita,
Malaki ya raia watapoteza maisha na miundombinu itaharibika na haitarudi kuwa kama zamani tena
Its better to die as a free man than to live on your knees.
 
Hiki kizazi cha akina Hitler Bora kingekufa WWII,Sijui Li Putin kwa nini halikufa.

Wanaleta kero kwenye modern world.Ikiwezekana wataalamu wa usalama watafute namna ya kuliua hili jamaa Ili Dunia ipumue.
 
Ndio ukweli huo,kwa nini uwazuie former Soviet states kuamua marafiki wanaotaka?
Kwa nini USA wahujumu Wasovieti? Wao hawana haki ya kuwa na mfumo tofauti wa kisiasa? USA ndiyo iliratibu 100% anguko la USSR. Maumivu hayo wengine yangali kumkichwa!

Hongo za USA zinazotiririka kwenda Ukraine huzioni? Umeshajiuliza kwa nini?
 
Walisema hivyo toka mwanzo ila alichofanya Putin ni ku take hiyo advantage.

Ina maana kwa sasa hawataruhusu Nchi yeyote ya Eastern Europe kujisogeza na NATO..

So njia yeyote ya wao kuwa safe ni ku build uwezo wao wenyewe kijeshi Ili baadae wakichagua upande waweze kukabiliana na Russia,jambo ambalo ni gumu.
 
Kwa nini USA wahujumu Wasovieti? Wao hawana haki ya kuwa na mfumo tofauti wa kisiasa? USA ndiyo iliratibu 100% anguko la USSR. Maumivu hayo wengine yangali kumkichwa!

Hongo za USA zinazotiririka kwenda Ukraine huzioni? Umeshajiuliza kwa nini?
Sio kuhujumu,bali ni mbinu za kutafuta resources zaidi kwa akili,hawakutumia Jeshi and so ni wajibu wa Russia kutumia mbinu zinazokubalika kwenye Dunia iliyostaarabika.
 
Hivi Tanzania idadi ya wanajeshi jwtz ni wangapi?
Kwa hali kama hizi ,ni bora kuwa independent kwenye masuala ya Uchumi,hukawii kuwa umeolewa na aidha China, US au Russia.

Pili AU iwe na treaty kama ya NATO maana huko tuendako mivutano itazidi hasa kadiri China anavyopata nguvu.
 
Huku kwetu tanzania naona kila mtu kawa mshangiliaji wa kusifu urusi kuwa mbabe.

sawa ni mbabe ila unafahamu mzozo wa vita vya pili vya dunia ulianzaje.

Hii ni historia ambayo inaweza kutokea na kwa nini mataifa makubwa yamebaki kukemea na sio kuunga mkono.

Urusi bado inatafuta njia ya kurudisha maeneo yake iliyopoteza kwa kuvunjika umoja wa USSR.kuvinjika kwakwe ni moja ambalo taifa tunalitegemea labda linaweza kuipa nguvu ukrain ni USA akifatiwa na washirika wake.

katiba taarifa ambazo watu wengi wanaziipuzia kuwa urusi alishaandaa kila target ya nchi yoyote itakayo taka kuungilia jambo lolote.

na kama hizi nchi zitaingilia basi ile sinema inayo itwa Terminal ikionesha kila nchi ikilusha kombora ndio itakuwa mwanzo wa vita vya tatu kwenye dunia.

sisi tunaoshangilia hata dawa kufikisha vijijini ngumu embu tujitafakari kuomba amani ya dunia.

kutokufikia na uchumi kuyumba wa dunia na vita ambazo kila kona zimetawala
 
Ndiyo maana kirefu cha JF ni JESHI la kwenye FINGERTIPS!
 
We ndo Mungu?

Usishirikishe Imani kwenye vitu visivyo na uhusiano. Wakati Nato wanaipiga Iraq, Iran, Syria ulikua wapi kutabili?
 
Mrusi hajawahi pigana vita ya maana akashinda, alipigwa Afghanistan aka kimbia, WW2 alijificha kwenye barafu north lole. Ngoja tuone sasa
 
Anayefikiria kuwa USSR itarejea kama ilivyokuwa, ni wishful thinking! Nchi kadhaa zilizokuwa ndani yake tayari ziko katika 'bloc' nyingine.
Hata Urusi haitarajii kuirejesha USSR.

Baadhi ya oblast zilikuwa ni jamii tofauti kabisa na Slav na baadhi walikuwa maadui zao toka miongo kadhaa nyuma.
Mfano: Poland

Urusi inajali sana upanukaji wa NATO kuelekea kwenye mipaka yake hasa ya Magharibi na hili wamelielezea mara nyingi.

Kwamba upanukaji wa NATO unahatarisha usalama wake, hakuna aliyejali.

NATO imesisitiza kila Taifa Lina haki ya kuchagua Mataifa ya kufungamana nao.

Lakini tujiulize je Trinidad and Tobago au Mexico iamue kuingia CSTO, Marekani itakubali? Haraka sana Marekani atakuja na kusisitiza Monroe doctrine kwamba America ni backyard yake, unaifahamu hili pro Amerika.

Kwa nini Sasa Urusi asisitize hata yeye ana area of influence ambayo haiingiliwi na Taifa lolote.

Sifa ya Wamarekani ni ndome la kuwili
 
Utakuta mapiganoooooo miaka kadhaa,halafu Putin anakamatwa ananyongwa hah! Kama Sadam ilikuwa hivihivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…