LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Kwa jinsi ilivyo its better akae na urusi atafute suluhu kuliko kuruhusu nchi yake kugeuka uwanja wa vita,
Malaki ya raia watapoteza maisha na miundombinu itaharibika na haitarudi kuwa kama zamani tena
Its better to die as a free man than to live on your knees.
 
Sijaipenda kabisa move hii ya pili.

Urusi imevamia Ukraine kijeshi nchi hiyo kwa kutumia majeshi ya anga,ardhini na nchi kavu.

Wamevamia kutoka Kila upande wa Ukraine.
Wanajeshi wa Urusi walionekana wakiingia mijini kutoka Kila upande.

Urusi imevamia Ukraine yote.
sio Tena majimbo yanayotaka kujitenga ya Donestk na Luhansk.

Jeshi la Urusi limevamia kwa kulenga na kupiga miji mikubwa kama Kiev,mariupol,Kharkiv,Odessa na Kramatorsk.

wenyewe Urusi wanasema wamepigwa sehemu za kijeshi TU na wala hawatashambulia maeneo ya kiraia.

Putin amesema lengo ni kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Ukraine.

Nimeshuhudia kupitia tv jengo moja kubwa nje Kuna askari wa Ukraine wanachoma nyaraka,mtangazaji anasema huenda ni jengo la Kijasusi.
Helkopta za Urusi zimaonekana kutawala katika miji iliyovamiwa.

Karibu Mkuu wa NATO akijibu maswali amatanabahisha kuwa NATO haitapeleka wanajeshi wake.
Marekani imelaaani na rais wa Marekani anaiombea kwa Mungu Ukraine katika kipindi hiki kigumu.

Waziri Mkuu wa UK amesema vikwazo vikali vitaongezwa.

Putin anasema hii ni Special operation yake ni kwa ajili ya "kui "neutrilize country's military capacity," kuiodhiofisha kijeshi Ukraine.

Rais wa Beralus amesema majeshi yake hayajaingia Ukraine kuongozana na Urusi ila yakihitajika yataingia.

Aisee hii Dunia haiko swa kabisa.
Ukweli ni kwamba majeshi ya Urusi yanajipigia TU Kila yanapotaka

NATO wamemtosa Ukraine,
Stoltenberg karibu Mkuu wa NATO anasema NATO jukumu lake ni kulinda Wanachama wake haitaingiza jeshi.
Sasa sijui walipokua wanasogeza majeshi sijui walikua wanafikiria nini.sijui walipeleka ili kupiga picha!

Marekani kamtosa Ukraine,
Uingereza kamtosa ukraine.

Kusema kweli kutoka moyoni huruma imeniingia sikupenda move hii ya pili.
Hiki kizazi cha akina Hitler Bora kingekufa WWII,Sijui Li Putin kwa nini halikufa.

Wanaleta kero kwenye modern world.Ikiwezekana wataalamu wa usalama watafute namna ya kuliua hili jamaa Ili Dunia ipumue.
 
Ndio ukweli huo,kwa nini uwazuie former Soviet states kuamua marafiki wanaotaka?
Kwa nini USA wahujumu Wasovieti? Wao hawana haki ya kuwa na mfumo tofauti wa kisiasa? USA ndiyo iliratibu 100% anguko la USSR. Maumivu hayo wengine yangali kumkichwa!

Hongo za USA zinazotiririka kwenda Ukraine huzioni? Umeshajiuliza kwa nini?
 
Sijaipenda kabisa move hii ya pili.

Urusi imevamia Ukraine kijeshi nchi hiyo kwa kutumia majeshi ya anga,ardhini na nchi kavu.

Wamevamia kutoka Kila upande wa Ukraine.
Wanajeshi wa Urusi walionekana wakiingia mijini kutoka Kila upande.

Urusi imevamia Ukraine yote.
sio Tena majimbo yanayotaka kujitenga ya Donestk na Luhansk.

Jeshi la Urusi limevamia kwa kulenga na kupiga miji mikubwa kama Kiev,mariupol,Kharkiv,Odessa na Kramatorsk.

wenyewe Urusi wanasema wamepigwa sehemu za kijeshi TU na wala hawatashambulia maeneo ya kiraia.

Putin amesema lengo ni kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Ukraine.

Nimeshuhudia kupitia tv jengo moja kubwa nje Kuna askari wa Ukraine wanachoma nyaraka,mtangazaji anasema huenda ni jengo la Kijasusi.
Helkopta za Urusi zimaonekana kutawala katika miji iliyovamiwa.

Karibu Mkuu wa NATO akijibu maswali amatanabahisha kuwa NATO haitapeleka wanajeshi wake.
Marekani imelaaani na rais wa Marekani anaiombea kwa Mungu Ukraine katika kipindi hiki kigumu.

Waziri Mkuu wa UK amesema vikwazo vikali vitaongezwa.

Putin anasema hii ni Special operation yake ni kwa ajili ya "kui "neutrilize country's military capacity," kuiodhiofisha kijeshi Ukraine.

Rais wa Beralus amesema majeshi yake hayajaingia Ukraine kuongozana na Urusi ila yakihitajika yataingia.

Aisee hii Dunia haiko swa kabisa.
Ukweli ni kwamba majeshi ya Urusi yanajipigia TU Kila yanapotaka

NATO wamemtosa Ukraine,
Stoltenberg karibu Mkuu wa NATO anasema NATO jukumu lake ni kulinda Wanachama wake haitaingiza jeshi.
Sasa sijui walipokua wanasogeza majeshi sijui walikua wanafikiria nini.sijui walipeleka ili kupiga picha!

Marekani kamtosa Ukraine,
Uingereza kamtosa ukraine.

Kusema kweli kutoka moyoni huruma imeniingia sikupenda move hii ya pili.
Walisema hivyo toka mwanzo ila alichofanya Putin ni ku take hiyo advantage.

Ina maana kwa sasa hawataruhusu Nchi yeyote ya Eastern Europe kujisogeza na NATO..

So njia yeyote ya wao kuwa safe ni ku build uwezo wao wenyewe kijeshi Ili baadae wakichagua upande waweze kukabiliana na Russia,jambo ambalo ni gumu.
 
Kwa nini USA wahujumu Wasovieti? Wao hawana haki ya kuwa na mfumo tofauti wa kisiasa? USA ndiyo iliratibu 100% anguko la USSR. Maumivu hayo wengine yangali kumkichwa!

Hongo za USA zinazotiririka kwenda Ukraine huzioni? Umeshajiuliza kwa nini?
Sio kuhujumu,bali ni mbinu za kutafuta resources zaidi kwa akili,hawakutumia Jeshi and so ni wajibu wa Russia kutumia mbinu zinazokubalika kwenye Dunia iliyostaarabika.
 
Hivi Tanzania idadi ya wanajeshi jwtz ni wangapi?
Kwa hali kama hizi ,ni bora kuwa independent kwenye masuala ya Uchumi,hukawii kuwa umeolewa na aidha China, US au Russia.

Pili AU iwe na treaty kama ya NATO maana huko tuendako mivutano itazidi hasa kadiri China anavyopata nguvu.
 
Huku kwetu tanzania naona kila mtu kawa mshangiliaji wa kusifu urusi kuwa mbabe.

sawa ni mbabe ila unafahamu mzozo wa vita vya pili vya dunia ulianzaje.

Hii ni historia ambayo inaweza kutokea na kwa nini mataifa makubwa yamebaki kukemea na sio kuunga mkono.

Urusi bado inatafuta njia ya kurudisha maeneo yake iliyopoteza kwa kuvunjika umoja wa USSR.kuvinjika kwakwe ni moja ambalo taifa tunalitegemea labda linaweza kuipa nguvu ukrain ni USA akifatiwa na washirika wake.

katiba taarifa ambazo watu wengi wanaziipuzia kuwa urusi alishaandaa kila target ya nchi yoyote itakayo taka kuungilia jambo lolote.

na kama hizi nchi zitaingilia basi ile sinema inayo itwa Terminal ikionesha kila nchi ikilusha kombora ndio itakuwa mwanzo wa vita vya tatu kwenye dunia.

sisi tunaoshangilia hata dawa kufikisha vijijini ngumu embu tujitafakari kuomba amani ya dunia.

kutokufikia na uchumi kuyumba wa dunia na vita ambazo kila kona zimetawala
 
Ndiyo maana kirefu cha JF ni JESHI la kwenye FINGERTIPS!
Yaani ukifungua JF Vita inapiganwa na Ukraine kazidiwa hatari..Ila ukiangalia international news unaona Mambo tofauti from reporters ..naona hapa BBCwanajeshi wa Russia wamekufa na ndege zimetunguliwa za Russia...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Take it from me, hakuna vita hapo!

Kwa watu wa dini wenye mioyo minyoofu, hiyo ni ishara kubwa sana kwamba sasa uovu wa wanadamu umefikia kikomo kama ilivyokuwa wakati wa Gharika na Sodoma na Gomora.

Mungu yule wa Gharika na Sodoma na Gomora ndiye yule yule ambaye tunaye sasa. Hajabadilika.

Amekuwa na subira kwa muda mrefu, sasa:"Enough is enough "
We ndo Mungu?

Usishirikishe Imani kwenye vitu visivyo na uhusiano. Wakati Nato wanaipiga Iraq, Iran, Syria ulikua wapi kutabili?
 
Mrusi hajawahi pigana vita ya maana akashinda, alipigwa Afghanistan aka kimbia, WW2 alijificha kwenye barafu north lole. Ngoja tuone sasa
 
Anayefikiria kuwa USSR itarejea kama ilivyokuwa, ni wishful thinking! Nchi kadhaa zilizokuwa ndani yake tayari ziko katika 'bloc' nyingine.
Hata Urusi haitarajii kuirejesha USSR.

Baadhi ya oblast zilikuwa ni jamii tofauti kabisa na Slav na baadhi walikuwa maadui zao toka miongo kadhaa nyuma.
Mfano: Poland

Urusi inajali sana upanukaji wa NATO kuelekea kwenye mipaka yake hasa ya Magharibi na hili wamelielezea mara nyingi.

Kwamba upanukaji wa NATO unahatarisha usalama wake, hakuna aliyejali.

NATO imesisitiza kila Taifa Lina haki ya kuchagua Mataifa ya kufungamana nao.

Lakini tujiulize je Trinidad and Tobago au Mexico iamue kuingia CSTO, Marekani itakubali? Haraka sana Marekani atakuja na kusisitiza Monroe doctrine kwamba America ni backyard yake, unaifahamu hili pro Amerika.

Kwa nini Sasa Urusi asisitize hata yeye ana area of influence ambayo haiingiliwi na Taifa lolote.

Sifa ya Wamarekani ni ndome la kuwili
 
Utakuta mapiganoooooo miaka kadhaa,halafu Putin anakamatwa ananyongwa hah! Kama Sadam ilikuwa hivihivi
 
Back
Top Bottom