Huh Shangazi inaonekana hilo neno Semi Presidential System umeielewa tofauti.
Ilivyo ni kwamba, Nje ya Russia tumezoea mifumo ya aina mbili, Presidential System ambapo Raisi anakuwa na Power juu ya kila kitu mfano hapa Tanzania.
Na kuna Parliamentary system ambayo Bunge ndio lina Nguvu kuliko vyote.
Kwa Russia ni Semi presidential system ikiwa na maana President hana mamlaka over kila kitu. President ni Mkuu wa nchi tu ila serikali ipo kwenye mikono ya waziri mkuu.
Mfano, Hapa Tanzania ambapo Raisi ndio kila kitu, Yeye ndio mkuu wa nchi na yeye ndio mkuu wa serikali na yeye tena ndio anateua wakuu wa Other Branches of Government upande wa Legislative na Judiciary.
Ila kwa Russia, President ni Head of State, Mkuu wa Serikali na Waziri mkuu, Jaji Mkuu ambae ndio kiongozi wa Judiciary branches huwa anachaguliwa na Federal Council baada ya kupendekezwa na Rais.
Sio kama hapa bongo, Raisi akiamka anamtaka judge flani awe anajitangazia na kumuapisha ndio imetoka hivyo.
Kwa kukuelewesha zaidi ni kua chukulia mfano kule US, Congress ndio wanaidhinisha mipango ya Raisi, the same na Russia, Federal Assembly yani State duma na Federal Council ndio wanaoidhinisha. Hata hili la Ukraine liliidhinishwa na State Duma.
Kama mnamkumbuka ni State duma ndio waliompa Putin Go ahead ya kutoa majeshi nje ya mipaka ya Russia.
Anyway hii niliwapa ahadi nikipata mda nitaiandika tena kwa lugha ya taifa kila mtu aielewe.
Kikubwa cha kuzingatia ni kwamba Russia ni Multi ethnics Country, Kila jamii ina asili zao na tamaduni zao. Hivo taratibu zao. Kwa hiyo kuna zile sheria za pamoja. na kuna sheria za kila eneo. Yani Federal Laws and Local Laws.
Maeneno kama Chechnya na Ingushetia, kuna waislam zaidi ya 90%, hawa unakuta kwenye local laws wana apply sheria za dini. That's Shaaria Law.
Na hii kuheshimiana kwa kila kundi kupewa haki yake ndicho kimekuza umoja ndani ya Russia. Kama ni hapa Tz wachaga, Wasukuma wahehe kila asili ipewe haki ya kuendesha mambo yao on top of National Laws.
Again viongozi wa hizo federal state hawana title ya President, wanaitwa tu Head of Government of ..... Iwe sasa Moscow, Chechnya St. Petersburg and so.
Kingine nisisahau, hiyo tafsiri ya federation sijui umeitafsiri kwa mlengwa upi, nikuulize hii TFF, Tanzania Football Federation imeunganisha ni na nini?
Sasa namna unavyoiona FIFA na TFF ingawa sina hakika kama wewe ni mfatiliaji mpira, ndivo federal government na regions hizo zinavojiendesha. Kwamba Aliye chini like TFF anaregulate mambo yake in Accordance to FIFA.
Russia ni kubwa mno tena mno ndio maana 2000, Putin akaanzisha Federal District. Ili kudelegate power ya kuhudumia Raia wake. Hizo federal district ni kam mashirikisho ya Mabara... Ie CAF
So badala ya FiFA then CAF then TFF...
Na Russia pia ni Federal Government then Federal District then Federal Subjects (hizo regions zote Oblast to Republics en so)
Nikipata mda nje ya uzi huu ipo siku nitalisema. Hap hata robo ya maelezo yanayohitajika sijayaandika.
Kwa sasa tukae na hii tu picha, kwa mwenye uwezo wa kuizoom na aizoom
View attachment 2258503