Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kweli mkuu siko vizuri kwenye historia ila natamka kama watu au wenyeji wa Igunga wanavyomjua Rostam Aziz mbunge wao mstaafu. Wao wanajua ni mbrushi siyo mwarabu. Inaonekana ni mbaluchi kama ulivyoandika. Asante nimejifunza kwako mkuu.
Wanaitwa kwa kiswahili Waburushi na sio wabrushi.

Na akiwa na tabia zisizofaa ni burushi mfano wa jitu.

Ila yule muungwana ni Mburushi.

Wapo bonde la Usangu huku nyanda za juu kusini wakiwa wamechanganyika na watu wa kabila la wasangu.
Wengine huko Tabora mpaka simiyu na Shinyanga.
 
Hahahaha 😂😂😁😀🤣 I am also recognized....thanks a lot...pamoja sana
 
Marekani angalau walidumu miaka 20 huko Afghanistan, unavyosema kweli. Je, Warusi walidumu miaka mingapi baada ya kuingia Afghanistan?
(Asante kwa kutumia maneno mazuri kama "upumbavu"! Usingeyatumia, ningejuaje wewe ni mwungwana?)
Sasa hii ni hoja inayohitaji kujibiwa kweli?

Kwa nini usiangalie kwenye serikari zao walizoziweka na zilidumu kwa muda gani?

Nani alitoka mapema na salama?

Kwa nini hakukuwa na casualties kubwa kipindi Cha Soviet kuliko hii instant withdrawal ya Mmarekani?
 
Mkuu hongera sana si kwa kujua hayo tu bali kwa kutenga muda wako na kuyaandika.
Inakera sana kuona tuna wapumbavu wengi mithili ya kina mk254, Yoda, jacal, FUSO, Imeloa nk ambao wamegeuzwa rasilimali na mabeberu katika kuendelea kufanikisha malengo yao ovu dhidi ya dunia yote... Kwa kifupi tu ni kwamba, Wayahudi walioko pale Mashariki ya Kati, Uingereza na USA ndio wahujumu uchumi wa dunia huku injini zao zikiwa ni hizi nyumbu ambazo ni kina mk254, YEHODAYA, tumainiEI, Annunaki, Yoda, Imeloa, jackal na wengine wengi.

Nafuatilia huu uzi kimyakimya ila katika mambo yaliyonikera mwaka huu ni hawa zero brain wa Pro NATO
 
Subiri mkuu warusi si watu wa mikwara ni watu wa vitendo
 
Wewe fanya subira tu...hicho kitu utakiona...na ndipo utakapotoa ushuhuda huku ukijipiga kifua Mara kadhaa kwa utakayoyaona....
Russia siyo mchezo....inaweza kuifuta dunia kwa muda wa nusu saa tu.....
 
South Sudan ndio weusi
Hata North sudan pia ni weusi, yaani waethiopia na watu wa Eritrea wanaweza kuwa weupe zaidi kuliko watu kutoka Sudan kaskazini.

Kinachofanya waingizwe kwenye Arab league ni Utamaduni wa kiarabu, lugha ya kiarabu pamoja na dini ya kiislamu.

Na sio Sudan pekee, Komoro, Somalia, Djibout naEritrea bila kusahau hata Zanzibar pia ipo eligible kuingia na kuhesabika kama Taifa la kiarabu ila mambo ya Muungano yakavuruga.

Ndio maana Faiza fox huwa anabisha na kutaka atambulike kwamba naye ni Muarabu [emoji38][emoji38][emoji38].

Baadhi ya picha za viongozi wa sudani na raia wa kawaida.
 
Wewe fanya subira tu...hicho kitu utakiona...na ndipo utakapotoa ushuhuda huku ukijipiga kifua Mara kadhaa kwa utakayoyaona....
Russia siyo mchezo....inaweza kuifuta dunia kwa muda wa nusu saa tu.....
Asante mkuu, hoja zito! Isipokuwa nisipokosei Urusi iko duniani. Unaamini kweli inataka kujifuta?
 
Asante sana,
NAMI nakuongezea na kukumbusha wataalamu wengine uliowasahau,
Triga,
Mbingunikwetu,
Hearly,
Bukyanagandi,
Idawa,
Deepond,
Mr Tyang,
Venus Star

Nikikumbuka wengine ntaongezea,
 
Walitegemea kuona maandamano haya yakitokea Moscow badala yake raia wa Moscow wapo busy na maisha yao as if nothing is happening in the world.

Ama kweli wazungu wenye akili walikuwa kina Sir Newton tu, hawa wa leo ni nyumbu kama nyumbu wa serengeti tu.

Operation ya Urusi inaenda kuwang'oa wanasiasa wengi sana wa Ulaya madarakani. Mfano hai wameuona wanasiasa wa ufaransa baada ya macron kupoteza watu wake wengi kwenye uchaguzi.
Acha iendelee kunyesha tuendelee kuona panapovuja. Viva [emoji635][emoji635] [emoji635]
 
Hata akili za kuhama na Moja kichwani za chekechea hana ....unajisumbua tu kaka.
 
"Tutaruhusu chakula na mbolea kutoka urusi na Ukraine kupitia bahari nyeusi endapo tu vikwazo vitaondolewa" Urusi.

Sasa naona tayari washatekeleza mashariti ya mwanaume "putin" halafu wanazuga kujificha ficha kama mwanamke alie fumaniwa.
Na bado Kipindi cha Baridi soon kitafika.

Kichwa kimoja cha Lavrov ni sawa na vichwa vyote vya EU.

Kichwa kimoja cha Putin nisawa na vichwa vya viongozi wakuu wote wa nchi za EU na United States.
 
Asante mkuu, bila shaka hoja yoyote haina haja ya kujibiwa. Kuhusu vifo sijui unalenga nini. Nimeona makadirio kwamba katika miaka kumi ya vita ya Kirusi Afghanistan wananchi 500,000 hadi 2,000,000 waliuawa. Katika miaka 20 ya vita ya Marekani idadi ya vifo hukadiriwa kati ya 179,999 hadi 212,000.
Wakati wa kuondoka? Sijaona takwimu, sikumbuki wengi walikufa maana Taliban hawakushambulia kituo cha mwisho cha Marekani kwenye uwanja wa ndege, na wanajeshi wa serikali ya Afghanistan walikimbia tu.
Sijui umeona wewe data?
Warusi walipopaswa kukimbia walifanya mikataba na Mujahedin lakini nimeona taarifa ya mapigano pale mwishoni na vikosi vya Ahmad Shah Massoud (mzee).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…