Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Haya majamaa yanatuma silaha mpaka yanaishiwa ila Russia yuko stable
20220623_064055.jpg
 
Samahani mkuu, hapa unakosa. Finland haikushinda mwaka 1940. Hivyo walipaswa kukubali kutoa sehemu ya ardhi yao kwa Urusi. Ila walifaulu kujitetea vizuri kiasi kwamba Urusi haikushinda kweli, ilipoteza askari wengi sana. Mwishoni pande zote mbili zilichoka.
Labda inafanana na Ukraine wa leo kiasi. Maana Urusi iliamini inaweza kuchukua maeneo kwa sababu ni kubwa, jirani mdogo anajitetea vizuri - mwishoni watamaliza kama Finland 1940?
Ungesoma "between the lines" ungeelewa ...shida ni uwezo wako wakufikiri una Kikomo..... Umeuwekea ukuta mwisho kufikiri ni hapa basi ukifika Hapo hautaki kufikiri zaidi.
 
Kuna vitu viwili naomba tuelewane:

1)kuwa kwenye hiyo race au jamii kwa asili nikimaanisha kuzaliwa mfano mbantu kwa sababu wazazi wake ni wabantu na kizazi kabla Yao.

2) kujitambua au kujinasibisha na jamii Fulani.
Kuna watu duniani hujinasibisha na jamii Fulani kwa sababu mbalimbali mfano dini, Utamaduni ama lugha.

Ila kwa case ya sudani wanajinasibisha na uarabu ila wenyewe hawana hiyo asili.

Mfano mtazame Omar Al Bashir
View attachment 2269205

Mpaka sasa hivi sijaelewa hoja yako.
Kwahiyo Omar Al Bashir siyo mwarabu!?

Kama siyo mwarabu yeye race yake ni ipi!? Mbona wapo Wahindi weusi.
Black color ni kwasababu ya Melanin.
View attachment 2269211

Kwa hoja yako hiyo, utakuja kusema msomali ni Mwarabu. Ndiyo au si ndiyo?

Kwa hoja yako hiyo utakuja kusema Ethiopian ni waarabu?

Kwa hoja yako hiyo utakuja kusema Aboriginal wa Australia ni waafrika?

Kwa hoja yako hiyo, utakuja kusema jamii za San na khoi sio waafrika?

Yes, watu wa Sudan sio waarabu ila kuchanganya tamaduni, lugha na Imani ya dini ya kiislamu ndio wamejitanabaisha kuwa wao ni waarabu na kuwa included kwenye Arab league.

Ila pia Misri ya kale ilitawala mpaka eneo la Sudan ya Leo hivyo athari ya tamaduni ndio sababu.

Je wakomoro ni waarabu? Kama sio kwa nini wanatambulika kama Taifa la kiarabu na wapo Arab league.

Je, kwa nini Wazanzibari waliomba uanachama na wakawa eligible? Je waarabu.

Inabidi usome human race ila nachoamini pro Russia unajua ila upo kwa ajili ya kuchallenge?!!!

Tujielimishe View attachment 2269227View attachment 2269228View attachment 2269229View attachment 2269230

Sura na mwonekano wa wasomaliView attachment 2269252

Ngoja tufanye kama Muhtasari,

kisiju pwani kwanza inaonesha wafikiri mwarab ni ngozi nyeupe tu.

According to study, kwanza Arab haielezewi kama ni Race, Wanadai Arab sio race, Arabs are not a distinct ethnic group, since there are both white Arabs na black arabs. Wanadai kua Some have blue eyes na wengine wana red hair; wengine are dark skinned; na walio wengi zaidi wapo somewhere in between.

Baadhi kama hao the black Sudanese Arabs ambao wana-claim descent ln the male line from Arabs of Mohammed's time, na yasemekana wanaweza kua correct in their claim.

Wala huezi tumia language as a sufficient criterion of Arabness since kuna wengi katika wayahudi wanaozungumza kiarabu lakini are not normally called Arabs.

Leo hii nyanyua mguu either mtandaoni au kwa watu kaulize Arab ni nini hakuna atakayekupa majibu yaliyonyooka, hata wao wenyewe wanajua ilivyo ngumu kutafsiri Arab n nini.

Neno Arab ina connotation of "people who speak clearly." hii ipo contrasted with ajam, or "people who speak indistinctly." Ingawa ajam (Kiajemi) came to be used specially of Persians, Na mfano wa hii contrast inafanana to that between Greeks and "barbarians."

Umeizungumzia Arab league, Yes arab league imeanza 1945, ilikuja kwa lengo la kuunganisha mataifa ya kiarabu ambayo nyuma hayana historia ya kua pa1 sababu kubwa ikiwa kwenye mvutano wa utawala na ukabila.

Kwa membership ln the Arab League the primary criterion ni language, Arab league ni muungano wa Arabic-speaking countries. Hapa utakuwa umepata majibu kwanini Djbout, Mauritania na Comoros wapo ndani ya Arab league.

Djibouti yupo ndani ya Arab league kwasababu ni Arab Speaking Country sio kwamba kwasababu ni Weupe kama waarab wale kwa mujibu unaowawaza kwamba kama ni weupe.

Afghanistan na Iran ni Muslim countries with over 97% percent lakini hawapo Arab league kwasababu sio Arab speaking Countries na vile vile sio waarab, Lakini wapo eneo moja. Iran wanazungumza kiajemi, Persian Language, Afghanistan wana-zungumza Pashto sio arabic.

Mtu anvyoitamka Arab, ni kama anavyoitamka Asia, anavyoitamka Europe n.k Ndani ya Asia kuna Chinese, Japanese, Korean, Mongolian n.k ndani ya Europe kuna Dutch, Polish, Irish, British, Welsh, Scottish, Portuguese n.k

Upande wa Arab nako kupo vile vile, in term of geneology, waarab wana-wagawa katika mafungu matatu, Ancient Arabs, Pure Arab (Walio kuepo kabla ya Abraham na Ishmael) na Arabized Arabs (Waarab waliofatia baada kwenye uzao wa Ishmael).

Ukija kwenye ethnic, Being Arab inabase kwenye criteria nyingi tu mfano
1. Genealogy kama waliopo Saudia,
2. Ancestry kama wale Afro Arab waliopo Comoro
3. Self Concept, kwamba naamua kujivalisha au kujinasibisha na Uarab.
4. Attribution of Identity, hii category wapo hao Sudan Kaskazini, ambao pia huwa wana claim hiyo ya pili kua chimbuko lao nyuma kabisa linatoka uko.

Nyinginezo ni kama Cultural, Language, Political (Hapa ndipo kuna Djibouti na Somalis), Society na Nationality.
 
Ninavyojua Ukraine walipiga kura mara kadhaa. Kwa jumla idadi kubwa walitaka kuwa nchi huru na kujiunga na Ulaya. Ila Crimea (iliyokuwa sehemu ya Urusi hadi 1956 na kuwa na wasemaji wengi wa Kirusi) naweza kuamnini kwamba kura ilikuwa kwa kujiunganisha na Urusi. - kuhusu sehemu za Donbas? Sijui, ila siuamini kura ilikuwa safi. Wengine (kama Charkiv , pia mji wa wasemaji wengi wa lugha ya Kirusi) walisimama upande wa Ukraine.
Kuhusu sehemu za Donbass haujui na mgogoro umeanza tangu Maidan Revolution 2014 ..Leo 2022 haujui na unashupaza shingo ndio utajua ya Lithuania, Latvia,Moldova huko !!?? Ikiwa hili lililo wazi haujui ..... Unasema hauamini kura kama zilikuwa sahihi , ila unaamini Mapinduzi ya Maidan yalikuwa sahihi!!?? Na ulimwengu unajua Nini alifaya Marekani katika hiyo kitu au nikusaidie kasome (EUROMAIDAN, ORANGE REVOLUTION AMA MAIDAN REVOLUTION) ndio uje tuongee maana umesema HAUNA UJUALO KATIKA HILO... Kachukue chakula cha ubongo tuongee vizuri .....
 

BRICS developing global reserve currency – Putin​

It will be based on a currency basket of the five-nation bloc, according to the Russian president
BRICS developing global reserve currency – Putin


President Vladimir Putin said on Wednesday that the BRICS countries – Brazil, Russia, India, China, and South Africa – are currently working on setting up a new global reserve currency.
“The issue of creating an international reserve currency based on a basket of currencies of our countries is being worked out,” he said at the BRICS business forum.
According to the Russian president, the member states are also developing reliable alternative mechanisms for international payments.
Earlier, the group said it was working on setting up a joint payment network to cut reliance on the Western financial system. The BRICS countries have been also boosting the use of local currencies in mutual trade.
 
Hata Finland walishinda , walimchakaza Urusi halafu wakampa Urusi asilimia 10 ya Ardhi ya Finland kama zawadi Kwa kupigwa na Finland. USIFANYE FUVU LAKO KUWA KABATI LA MENO,MACHO NA ULIMI TU ....LINATAKIWA KUBEBA UBONGO PIA (KAMA UNAO).
Sasa hapo ndiyo umeandika mafii gani !!! Ukiona nchi inatoa ardhi yake kwa adui yake anaye pigana naye vita basi ujue kashindwa vita huyo aliye toa ardhi ni kama sasa hivi USA inamshauri ukraine akubali kumwachia mrusi ardhi kwa kupata amani .
 

BRICS developing global reserve currency – Putin​

It will be based on a currency basket of the five-nation bloc, according to the Russian president
BRICS developing global reserve currency – Putin


President Vladimir Putin said on Wednesday that the BRICS countries – Brazil, Russia, India, China, and South Africa – are currently working on setting up a new global reserve currency.
“The issue of creating an international reserve currency based on a basket of currencies of our countries is being worked out,” he said at the BRICS business forum.
According to the Russian president, the member states are also developing reliable alternative mechanisms for international payments.
Earlier, the group said it was working on setting up a joint payment network to cut reliance on the Western financial system. The BRICS countries have been also boosting the use of local currencies in mutual trade.
USA [emoji631] Kwisha habari zake ..... uchumi wa makaratasi wa USA sasa unakwenda ku expire [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuhusu sehemu za Donbass haujui na mgogoro umeanza tangu Maidan Revolution 2014 ..Leo 2022 haujui na unashupaza shingo ndio utajua ya Lithuania, Latvia,Moldova huko !!?? Ikiwa hili lililo wazi haujui ..... Unasema hauamini kura kama zilikuwa sahihi , ila unaamini Mapinduzi ya Maidan yalikuwa sahihi!!?? Na ulimwengu unajua Nini alifaya Marekani katika hiyo kitu au nikusaidie kasome (EUROMAIDAN, ORANGE REVOLUTION AMA MAIDAN REVOLUTION) ndio uje tuongee maana umesema HAUNA UJUALO KATIKA HILO... Kachukue chakula cha ubongo tuongee vizuri .....
Mambo ya Euromaidan miaka 8 iliyopita sijagusa. Nimesikia mambo mengi tofauti. Kuhusu mawazo ya watu wa Ukraine nimeona tu matokeo ya uchaguzi uliofanywa baadaye. Kwa mfano walipompa Bwana Selenski kura nyingi. Sijasikia huu ulikuwa uchaguzi wa uwongo.
 
Kingine kuna Mis-conception kuhusu tamaduni. Inaposemwa kua "Wa-afrika waliacha tamaduni zao wakachukua za mbeberu ndizo zilizowafikisha hapa" wengi wetu huwa tunawaza mizimu na mengineyo.

Lakini kuna point ya muhim zaidi huwa haionekani kwa walio wengi.

Iko hivi, leo unaponyanyua mguu ukazama kijiji flan hapa hapa TZ, ukawakuta wanakula kwa kutumia vijiti. Ukawaambia wanapaswa kutumia vijiko ndio bora zaidi. Wakibadili matumizi ya vijiti kuja vijiko ilhali hawazalishi vyuma vya kutengeneza vijiko hiyo ni faida kwa nani?

Naam, sasa hiyo ndio Concept ya Culture transformation ukipenda iite mabadiliko ya life style.

Kila badiliko la culture ni fursa! Ulikuwa na desturi ya kutembea kutoka Mwenge hadi Ubungo, ukahamia kwenye usafiri. Tiari ni Fursa kwa wasafirishaji.

Kwenye biashara, fursa zipo mafungu mawili, naomba nitumie haya maneno mawili kwa ajili ya Illustration, ie Natural na Artificial "Fursa"

Fursa za "asili" ni zile basic kwa maisha ya mwanadam, mfano kula ama chakula. Zunguka pote duniani, as long as kuna viumbe wanaitwa binadam. Fursa hii ya Chakula ipo.

Pili katika Fursa Artificial, hizi ni fursa za ziada ambazo zina link moja kwa moja na tamaduni za watu. Fursa zilizo mlengwa wa "Life style"...

Taratibu tu tutaelewana.

Sasa mnamo Karne ya 17, 1800+ kulikuwa na mapinduzi ya Viwanda huko Europe. Circle ya Viwanda iko hivi, unahitaji malighafi uzalishe, baada ya kuzalisha utahitaji soko ukauze. So upatikanaji wa viwili hivyo, ie Malighafi na Soko ndiyo yanayofanya viwanda viendelee kua Hai.

Mahitaji ya hivyo vitu ndio yakahitaji umiliki wa maeneo mengine duniani. Sasa katika maelezo tujikite Afrika, Afrika yetu rasilimali zipo za kutosha, so kitendawili cha kwanza kimepata mteguzi, je cha pili? Soko?

Naam, hapa ndipo uenezwaji wa tamaduni zao ukaanza ku-play part yake. Tukitoa mfano wa Zaman ambao wengi hatukuepo itakuwa ngumu kueleweka. Hebu tuwaangalie wa Masai waliopo hivi leo...

Tanzania Nzima ya leo ikiwa na tamaduni za kimasai, Industry ya Madawa itakuwa na hali gani, Kwenye viwanda vya nguo itakuaje, na sehem nyinginezo? Huo ni mfano tu.

Sasa kuna swali la muhim ambalo kila mtu ajiulize, kwan sie kua na tamaduni zao wananufaika nini na tunapoteza kipi...

Sikia tulikutwa tunavaa Ngozi, wakatwambia Suti na Tai ndio Vazi zuri, wakati huo hatuna kiwanda cha kuchakata pamba kutengeneza suti, so wao ndio wakazileta... Lakini in exchange of rasilimali zetu.

Katika mabadiliko ya Tamaduni ni creatiom of demand, kisha wanajihusisha na supply. Na hiyo tunaita Business, ile ikawa ni biashara tena biashara ya kinyonyaji.

Kuna sehem niliwahi kusema tumebadilishiwa tamaduni, tumepigwa tattoo ya utumwa. Maana yangu ndio ilikuwa hiyo.

Tulikuwa na taratibu zetu za kufanya biashara, tulikuwa kwenye mfumo wa barter trade. Bidhaa kwa bidhaa, tukatolewa huko tukapelekwa kwenye mfumo huu tulio nao leo ambao wao wamejimilikisha.

Yes katika mfumo wa barter trade kwao ulikuwa mgumu na wasingeuweza kwasababu fika hawana cha kufanyia exchange, em fikirieni kila rasilimali hadi leo wanaagiza kutoka nje, ungekuepo ule mfumo wa barter trade bila haya makaratasi yao wangeishije, wangebadilishana na kipi?

Ule mfumo wa zaman ulimpa nguvu sana mwenye mali, ila huu wa sasa unampa nguvu zaidi anayemiliki hizo printers. Afrika tumezikacha tamaduni zetu, tumeikacha life style yetu na kua watumwa wa viwanda vyao... Of course tukawa soko rasmi la hawa viumbe.

Leo hii hadi Panadol, ya kupunguza maumivu tunaagiza kutoka nje, lakini hatujiulizi before colonialism, Mababu zetu walijitibu kwa kutumia nini.

Sasa huo utegemezi ulioletwa kama product ya kuacha tamaduni zetu, ya kuacha life style yetu ndio iliyotufikisha hapa tulipo.

Mna makaa ya mawe, hamyatumiii kwa kisingizio cha "Climate change", mnaenda kuchukua mafuta kutoka kwao. Tumejaza mapori yenye mizizi ya kila aina ya ugonjwa yet tunafata vidonge kutoka kwao as if hizo dawa wanazitengenezea mawinguni.

So linapokuja issue ya tamaduni ningependa ifahamike kwa mtazamo huo, sio issue za kuabudu mizimu. Ingekuwa kuabudu mizimu kunaleta maendeleo basi Jamii zote za asili zinazofanya matambiko zingekuwa top kwa kila kitu.

Napenda na napenda zaidi kuhamasisha watu kujifunza elim tofauti tofauti, ni Raha sana. Ile wide view unayokua nayo kwenye jambo flani inakua kubwa. Na hata kwa jambo ambalo unakuwa hulifaham ukielekezwa basi walielewa kwa mapana zaidi kuliko mtu mwenye aina flan ya uelewa.

Me sio medical professional ila naelewa kwanini sindano ya kalio wala sio usoni au mguuni 😂. Coz kwenye kalio kuna bulk of muscles, so sindano inayochomwa hapo ni special for muscles, ilhali ya mkononi ni kwenye Vein.

Hata napokutana na Daktari zuzu, walau hawezi kuniingiza chaka kizembe.

Most huwa tunawaza biashara ni kuuza na kununua, ila biashara ina mambo mengi mno bahati mbaya hayapo kwenye syllabus watoto wasome. Culture, nairudia kwa herufi kubwa CULTURE, ni neno fupi ila pana sana.

Mwisho kila kitu kina faida na hasara, ndani ya cultural transformation faida zipo na hasara zipo ambazo ukizitizama ni kubwa kiliko faida iliyopatikana.
 
Sasa hapo ndiyo umeandika mafii gani !!! Ukiona nchi inatoa ardhi yake kwa adui yake anaye pigana naye vita basi ujue kashindwa vita huyo aliye toa ardhi ni kama sasa hivi USA inamshauri ukraine akubali kumwachia mrusi ardhi kwa kupata amani .
SI history mnayoletaga hapa FINLAND ALISHINDA VITA ....!!?? UNAJUA KWANZA MAANA YA "SARCASM".... UKIIJUA RUDI KUSOMA ULICHOKIQUOTE HALAFU UJE TENA SAWA.
 
Mambo ya Euromaidan miaka 8 iliyopita sijagusa. Nimesikia mambo mengi tofauti. Kuhusu mawazo ya watu wa Ukraine nimeona tu matokeo ya uchaguzi uliofanywa baadaye. Kwa mfano walipompa Bwana Selenski kura nyingi. Sijasikia huu ulikuwa uchaguzi wa uwongo.
Ila majimbo ya Donbass kujitenga kupiga kura ya kujitenga ni uwongo SI ndio!!?? Itoshe kusema tena UMEJIPANGIA MIPAKA YA KUFIKIRISHA HILO FUVU.... Adios.
 
Mkuu niseme nini ukliniambia sina akili sawasawa kulingana na uwezo wako mkubwa? Nikupongeze? (au kuhurumia??)
Sasa unashupaza shingo Kwa matukio ya Leo bila kushirikisha mizizi ya mgogoro unaambiwa unasema hujui..bado unashupaza shingo, unaambiwa topic hizo kasome unasema za miaka nane nyuma ... Na bado unakumbushia matukio ya miaka ya 1991 ambayo ni miaka 30 nyuma ila matukio ya miaka 8 nyuma hutaki kuyajua na hujui ...utakuwa na AKILI GANI SASA KAMA SIO ZA KUTAWAZIA TU.... yaani utoe reference ya miaka 30 nyuma tukubali ila tukikupa ya miaka 8 nyuma hutaki aseee ..... Au ndio mpaka wafikirie mabeberu wako wakupe jike ndio uongee!!?
 
Naomba kutoa certificate of appreciation kwa hawa pro Russia maana kwa elimu mnayoitoa humu, PUTIN anajipiga piga kifuani huko aliko na taratibu watu wameanza kuelewa ukweli
Certificate of appreciation ni kama ifutavyo
Ask-Q
Sikirimimimasikini
Jesus Mlokozi
lee van cliff
Extrovert
STRUGGLE MAN
Champagnee
NYUNDO YA MOTO
Galip Vrl
Mtoto wa nzi
Bwana Utam
TUJITEGEMEE
green rajab
Mathanzua
1954
spanerboy
kt the irreplaceable
mohamedidrisa789
Washawasha
Msulibasi
Tafakari yetu
Jumong S
Bugucha
Lucha
East
NB:
certificate bado zinaendelea kutoka,so endeleeni kutupa madini pro Russia
Ni Mimi mfilisiti pekee ambaye sikupendezwa na njama za kumuua SAMSON.
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji16][emoji120][emoji3577][emoji3577] tuko pamoja sana asee
 
😂😂😂

Ukiyakuta hapa yalivyokomaa na Marekani, mara California washenzi kweli hawa watu. Njia pekee y kujikimu kimaisha wameona ni kuuza viungo vyao. Hawana mawazo mbadala.

Siku wakianza kuuza pumzi zao nishtue, na tenda kama hizo za kutosha tu Mada Fanta hawa.
 
Sasa unashupaza shingo Kwa matukio ya Leo bila kushirikisha mizizi ya mgogoro unaambiwa unasema hujui..bado unashupaza shingo, unaambiwa topic hizo kasome unasema za miaka nane nyuma ... Na bado unakumbushia matukio ya miaka ya 1991 ambayo ni miaka 30 nyuma ila matukio ya miaka 8 nyuma hutaki kuyajua na hujui ...utakuwa na AKILI GANI SASA KAMA SIO ZA KUTAWAZIA TU.... yaani utoe reference ya miaka 30 nyuma tukubali ila tukikupa ya miaka 8 nyuma hutaki aseee ..... Au ndio mpaka wafikirie mabeberu wako wakupe jike ndio uongee!!?
Muu tulia, upunguze jazba. Ukijibu tafadhali jaribu kuwa makini kidogo. Wapi nilisema sijui mambo ya Euromaidan?

Kuhusu Ukraine naangalia matokeo ya uchaguzi huru uliotokea mara mbili baada ya mambo ya Maidan.
Matokeo hayo yanaonyesha idadi kubwa ya wananchi wanasimama upande wa nchi yao.
 
Back
Top Bottom