Kingine kuna Mis-conception kuhusu tamaduni. Inaposemwa kua "Wa-afrika waliacha tamaduni zao wakachukua za mbeberu ndizo zilizowafikisha hapa" wengi wetu huwa tunawaza mizimu na mengineyo.
Lakini kuna point ya muhim zaidi huwa haionekani kwa walio wengi.
Iko hivi, leo unaponyanyua mguu ukazama kijiji flan hapa hapa TZ, ukawakuta wanakula kwa kutumia vijiti. Ukawaambia wanapaswa kutumia vijiko ndio bora zaidi. Wakibadili matumizi ya vijiti kuja vijiko ilhali hawazalishi vyuma vya kutengeneza vijiko hiyo ni faida kwa nani?
Naam, sasa hiyo ndio Concept ya Culture transformation ukipenda iite mabadiliko ya life style.
Kila badiliko la culture ni fursa! Ulikuwa na desturi ya kutembea kutoka Mwenge hadi Ubungo, ukahamia kwenye usafiri. Tiari ni Fursa kwa wasafirishaji.
Kwenye biashara, fursa zipo mafungu mawili, naomba nitumie haya maneno mawili kwa ajili ya Illustration, ie Natural na Artificial "Fursa"
Fursa za "asili" ni zile basic kwa maisha ya mwanadam, mfano kula ama chakula. Zunguka pote duniani, as long as kuna viumbe wanaitwa binadam. Fursa hii ya Chakula ipo.
Pili katika Fursa Artificial, hizi ni fursa za ziada ambazo zina link moja kwa moja na tamaduni za watu. Fursa zilizo mlengwa wa "Life style"...
Taratibu tu tutaelewana.
Sasa mnamo Karne ya 17, 1800+ kulikuwa na mapinduzi ya Viwanda huko Europe. Circle ya Viwanda iko hivi, unahitaji malighafi uzalishe, baada ya kuzalisha utahitaji soko ukauze. So upatikanaji wa viwili hivyo, ie Malighafi na Soko ndiyo yanayofanya viwanda viendelee kua Hai.
Mahitaji ya hivyo vitu ndio yakahitaji umiliki wa maeneo mengine duniani. Sasa katika maelezo tujikite Afrika, Afrika yetu rasilimali zipo za kutosha, so kitendawili cha kwanza kimepata mteguzi, je cha pili? Soko?
Naam, hapa ndipo uenezwaji wa tamaduni zao ukaanza ku-play part yake. Tukitoa mfano wa Zaman ambao wengi hatukuepo itakuwa ngumu kueleweka. Hebu tuwaangalie wa Masai waliopo hivi leo...
Tanzania Nzima ya leo ikiwa na tamaduni za kimasai, Industry ya Madawa itakuwa na hali gani, Kwenye viwanda vya nguo itakuaje, na sehem nyinginezo? Huo ni mfano tu.
Sasa kuna swali la muhim ambalo kila mtu ajiulize, kwan sie kua na tamaduni zao wananufaika nini na tunapoteza kipi...
Sikia tulikutwa tunavaa Ngozi, wakatwambia Suti na Tai ndio Vazi zuri, wakati huo hatuna kiwanda cha kuchakata pamba kutengeneza suti, so wao ndio wakazileta... Lakini in exchange of rasilimali zetu.
Katika mabadiliko ya Tamaduni ni creatiom of demand, kisha wanajihusisha na supply. Na hiyo tunaita Business, ile ikawa ni biashara tena biashara ya kinyonyaji.
Kuna sehem niliwahi kusema tumebadilishiwa tamaduni, tumepigwa tattoo ya utumwa. Maana yangu ndio ilikuwa hiyo.
Tulikuwa na taratibu zetu za kufanya biashara, tulikuwa kwenye mfumo wa barter trade. Bidhaa kwa bidhaa, tukatolewa huko tukapelekwa kwenye mfumo huu tulio nao leo ambao wao wamejimilikisha.
Yes katika mfumo wa barter trade kwao ulikuwa mgumu na wasingeuweza kwasababu fika hawana cha kufanyia exchange, em fikirieni kila rasilimali hadi leo wanaagiza kutoka nje, ungekuepo ule mfumo wa barter trade bila haya makaratasi yao wangeishije, wangebadilishana na kipi?
Ule mfumo wa zaman ulimpa nguvu sana mwenye mali, ila huu wa sasa unampa nguvu zaidi anayemiliki hizo printers. Afrika tumezikacha tamaduni zetu, tumeikacha life style yetu na kua watumwa wa viwanda vyao... Of course tukawa soko rasmi la hawa viumbe.
Leo hii hadi Panadol, ya kupunguza maumivu tunaagiza kutoka nje, lakini hatujiulizi before colonialism, Mababu zetu walijitibu kwa kutumia nini.
Sasa huo utegemezi ulioletwa kama product ya kuacha tamaduni zetu, ya kuacha life style yetu ndio iliyotufikisha hapa tulipo.
Mna makaa ya mawe, hamyatumiii kwa kisingizio cha "Climate change", mnaenda kuchukua mafuta kutoka kwao. Tumejaza mapori yenye mizizi ya kila aina ya ugonjwa yet tunafata vidonge kutoka kwao as if hizo dawa wanazitengenezea mawinguni.
So linapokuja issue ya tamaduni ningependa ifahamike kwa mtazamo huo, sio issue za kuabudu mizimu. Ingekuwa kuabudu mizimu kunaleta maendeleo basi Jamii zote za asili zinazofanya matambiko zingekuwa top kwa kila kitu.
Napenda na napenda zaidi kuhamasisha watu kujifunza elim tofauti tofauti, ni Raha sana. Ile wide view unayokua nayo kwenye jambo flani inakua kubwa. Na hata kwa jambo ambalo unakuwa hulifaham ukielekezwa basi walielewa kwa mapana zaidi kuliko mtu mwenye aina flan ya uelewa.
Me sio medical professional ila naelewa kwanini sindano ya kalio wala sio usoni au mguuni 😂. Coz kwenye kalio kuna bulk of muscles, so sindano inayochomwa hapo ni special for muscles, ilhali ya mkononi ni kwenye Vein.
Hata napokutana na Daktari zuzu, walau hawezi kuniingiza chaka kizembe.
Most huwa tunawaza biashara ni kuuza na kununua, ila biashara ina mambo mengi mno bahati mbaya hayapo kwenye syllabus watoto wasome. Culture, nairudia kwa herufi kubwa CULTURE, ni neno fupi ila pana sana.
Mwisho kila kitu kina faida na hasara, ndani ya cultural transformation faida zipo na hasara zipo ambazo ukizitizama ni kubwa kiliko faida iliyopatikana.