Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Naona si mchango tu! Bali ni taaluma yako mkuu. Ahsante kwa kutupa extra curricular activities
 
Ni vigumu sana developed country kufirisika. Ujerumani ilipigwa kila kona ikachakaa kwenye WW1 haikufirisika, ikatoka mwaka 1923 ikapata hyperinflation haikufirisika, ikatoka ikaingia WW2 ikapigwa haikufirisika. Ikajitenga na kujenga Berlin war bado ipo kiuchumi. Sasa Russia ifirisikie kisa bonds ambazo hazifiki hata $100 billions.

Default haiifanyi ifirisike ni dalili ya kitu fulani kuendelea. Hilo la kesi lingefaa watu wameweka hela zao pale ingawa sijui kama kuna sheria za kuilazimisha Marekani iruhusu matumizi ya USD. Kina Venezuela na wengine wengi wangeshafungua kesi kulazimisha Marekani iwaruhusu kutumia $
 
Na wewe unaona ni sawa kabisa kupewe msaada wa kujengewa choo kama kweli hao mabeberu wanawapenda inatakiwa wawape fomula waliopitia wakawa matajiri sio kutuletea msaada choo halafu tunashangilia
Si tushasema mabeberu hawatupendi na awana maana. Waambie Russia watufundishe au kataa hiyo misaada ya mabeberu
 
Hiyo misaada wewe mwenyewe unaitumia na hapa uko busy unatumia JF ambayo ina mkono wa Mmarekani au sio wewe? Hiyo misaada haikwepeki, haichagui nani atatumia.
Na hao EU huo upumbavu ndio maamuzi yao, ni kama upumbavu wa Russia kuvamia Ukraine. Wote ni wapumbavu kama ndio tafsiri yako ya kufanya maamuzi. Na Russia anafanya upumbavu kuendelea kuwauzia gesi
 
Ishu hapa sio kufilisika MKUU sababu wajuvi mnajua kama hapo usemapo kwamba hawawez filisika kwahio BOND wanayodaiwa
Ishu tunaanza kujaj hao jamaa wanaosema kama RUSSIA kashindwa kulipa hiko kiasi
Yaani hiki kitu chakushindwa wamekitoa wapi yaani wamezingatiaje kumtangaza jamaa kama kashibdwa kulipa hio BOND anayodaiwa !!!??
Yaani umfumbe mtu macho useme hawezi kuona
Narudia tena biibiisii siiamini wewe hope unaiamini nenda kasome wameielezea hio habar
Wakakwes shen kama sisi tunavyokwes shen kama unamzuiaje mtu kula halaf useme hawez kula sio useme kama umemzuia asiweze kula
US wameizuia RUSSIA isitumie pesa zao zilizopo huko nje kwakua UNSWIFT leo wanalalama kipi
Wawe wapole au wangojee jamaa wakafungue acc za RUBO wapewe pesa zao waende wakazifanyie exchange mbele huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kina nani wamekataa kulipwa? Creditors na walioweka vikwazo ni makundi mawili tofauti. Kwenye kununua bonds ilikuwa specific zitalipwa kwa USD na ndio mara zote hulipiwa uko sasa unasemaje "wakubali kulipwa kwa Ruble". Kama ni hivyo hakuna maana ya makubaliano yale
 
Misaada kutokukwepeka sio kweli ila ufinyu wetu ndio unatufanya tuishie hapo MKUU
Halaf aliokwambia kutumia JF nimsaada nenda kamwambie akwambie tena
Kuhusiana na RUSSIA kuwauzia GAS hao jamaa wala sio UPUMBAVU nibiashara kama nyengine nabiashara sio haram
Shida nikwamba kufanya Upumbavu sio shida ila shida kutaka kuingilia UPUMBAVU wawatu wakat demokrasia inauhuru wake
Twende taratibu MKUU naona unaelekea kunielewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa zitalipwa kwa USD wanalipwaje kwa USD wakat miamala yakufanya kwa USD imepigwa pini !!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofautisha Biashara na Msaada wewe, kueni na akili basi, mnajichetua hadi lini wajomba? Asingepiga kazi akapata fedha za kununua Smart anayotumia kumuezesha kuingilia JF, USAID ndio wangempa au? Wewe? Biashara unaita msaada? USAID ndio wamempa bundle sio? Dah kweli mahaba niue! Huu upopoma wako sio level za ubinadam. Ni usukule level 3581901.
 
Ukimfumba mtu macho ataendelea kuona au ukimziba mdomo atakula? Haijalishi umefungwa macho na vyuma, tutasema hujaona kisha tutoe sababu kwa nini hujaona ni kwa kuwa ulifungwa macho. Hatutasema umeona kwa kuwa ulilazimishwa kufunga macho. Fact hapo ni kuwa kilichotokea hujakiona.

Default ni nini kwa uelewa wako
 

Kwa niaba yangu naomba piga spana za utosi huyo sukari ya machalii wa namanyire mi niko nyuma yako nakuombea😃😃😃.
 
Upopoma unao wewe. Kumbe basi tuseme EU na Marekani wanataka biashara na Venezuela na Iran. Yanini kusema ni wapumbavu wakati wanaenda kufanya exchange, yanini kuwaita wapumbavu endapo watakataa kufanya exchange na kujihusisha na anayefanya nao.

Kama biashara sio msaada kinachowaliza SWIFT kufungwa ni nini? Si sio msaada ule
 
Duh, na SWIFT nayo ni msaada? Unatumia nini kufikiria ndugu? Unajua kweli maana ya Msaada? Msaada ni nini?
 
Ulivyokazana kutetea huo uozo sasa he he he, Hivi waliompa vikwazo Venezuela na Iran ni wakina nani na kwasababu zipi? Hivi leo ukipita duka la Mhehe kule Iringa ukamtukana weee, ukamfungia kibanda chake ukijidai utapata vingine zaidi sehem nyingine, huko kwingine umeeda umevikosa. Unarudi kwake kumuomba akuuzie ulivyovitukana mwanzo... hilo kwako ni Ujanja sio Upuuzi eh?
 
Kuna vita za aina nyingi [emoji41][emoji41][emoji41]
 
Umeongea in detail sana, nikupongeze kwa hilo, sidhan kama kuna sehemu ya kujaza nyama wala kupunguza mnofu kwa kile ulichokiandika ila naweza ongeza viungo tu kunogesha mchuzi.

Natamani sana kila taifa au jumuiya za kimataifa zingekuwa na sarafu yake inayotumika kama foreign exchange currency, mfano AU tuwe na sarafu yetu, Ulaya wanakuwa na sarafu yao, Southern America wanakuwa na sarafu yao, North America wanakuwa na sarafu yao, Asia, Australia nao kila bara linakuwa na sarafu yake. Hiyo itasaidia kuondoa ufalme wa sarafu moja na kuondoa upuuzi wa kutumia pesa kama silaha ya uchumi.

Au kama nchi nyingi duniani zikiamuka kutoka kwenye ukoloni mamboleo na kuamua kujitegemea, yani kila nchi itumie pesa yake inapofanya exportation, mfano Tanzania tuanze kuuza tanzanite yetu kwa Tsh, kenya nao wanavyo export waviuze kwa Ksh. Inshort kila unapofanya importation ya bidhaa kutoka nchi flani basi uwe tayari kutumia sarafu ya hiyo nchi inayokuuzia kama Russia anavyo wafanyia EU. Hiyo itasaidia sana most of currencies kuwa katika high demand, stable and value.

Sema hilo linawezekana endapo tu nchi ikiwa na maamuzi magumu na viongozi wenye akili kama putin, maana nchi nyingi zimeshageuzwa watumwa na USA kwa kuweka reserves zake in USD. Binafsi natamani sana ukija kununua dhahabu ya Geita-Tanzania au Almasi ya Mwadui-Shinyanga basi uje na mzigo wa Tsh na siyo USD, pengine USD1 itakuwa sawa Tsh200.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…