Nchi zetu za ulimwengu wa tatu zinategemea sana sarafu za kimataifa zilizo kwenye uhitaji mkubwa ili kuendesha uchumi wetu na hiyo inatokana na importating rate kuwa kubwa zaidi kuliko exporting rate, na kwenye kuimport sarafu zinazotumika zaidi ni international currencies ambazo mostly ni USD na Euro.
Kutumia Gold kama njia mbadala ya foreign exchange inawezekana sema ni changamoto kutokana na upatikanaji mgumu wa dhahabu ulivyo ukilinganisha na pesa. maana siyo kila nchi ina reserves ya dhahabu.
Kuhusu USD kufa, haitakiwi ife maana italeta changamoto kwenye foreign exchange market hasa sisi nchi masikini ambapo pesa zetu hazipo kwenye demand ya Uchumi wa dunia ukilinganisha na USD, Ruble, Pound, Euro na n.k.
Sema tunahitaji kuwepo na sarafu zaidi hata ya tatu zinazouwiana kwenye demand ya foreign exchange market na ndo maana tunatamani Ruble iendelee kuwa sarafu imara na inayohitajika kwenye uchumi wa dunia ili iendelee kushusha ufalme wa USD ambapo USA anatumia sarafu yake kama silaha ya uchumi.
Kuhusu USD mjomba mimi naona inatakiwa ikufe tu, kuendelea kua in high demand ndiko kunakompa mwanya US aendelee na karakasha lake la ku-print kila mwaka.
Ona mjomba, sidhani kama nchi zingine zitaangamia. Ni kweli nchi nyingi zimehifadhi reserve zao katika dollar, Euro, Sterling Pound n.k, Pia zipo nchi ambazo wame-peg fedha zao kwa hizo stable currecy kama Euro na Dollar.
Huu ni uhuni waliofanya wenzetu, kutushikiza vijibom ili in case vikilipuka basi tulipuke wote, so inapelekea USD ni currency ya Taifa lingine ila na sisi huku uchochoroni kutoka taifa lingine tunakomaa kuitetea na kuilinda kuliko fedha zetu wenyewe.
As far as I know, Central Banks hutunza au kuweka akiba zao kwenye "Values", wakiona zinashuka thamani wataz-dump chap tu kwa exchange ya vingine vinavyoweza kutunza thamani.
US dollar zile karatasi tu mjomba, na wao wanajua. Ila ndio washageuza mataifa mengine majalala. Mjomba US anaprint dollars ila hakai nazo kihiiivo. Katika nchi zinazoongoza kwa kua na Largest Gold Reserves ni yeye.
1. US tani 8.1k
2. Germany tani 3.3k
3. France tani 2.5k
4. Italy tani 2.4k
5. Russia tani 2.3k
6. China tank 1.9k
7. Switzerland tani 1.1k
8. Japan tani 846
9. India tani 754
10. Netherlands tani 612.
Hii list ya Top tena utaona US kachimbia kibindoni dhahab nyingi kuliko wa pili, wa tatu na wa4 kwenye list Combined.
Kwenye hio list nchi ya10, Netherlands. US kaweka kibindoni dhahabu karibu mara 12 ya Netherlands. Kuna nchi zaidi ya 200. So you get a point wamehifadhi nini kwenye central bank zao. Ni karatasi za hawa mabeberu, huku wao wamezitunza hizo mali.
Na Gold kua scarce or limited in Quantity ndicho kinachoipa thamani. Gold ingekuwa inapatikana kama Mawe au kokoto mtaani isingekua na thamani hiyo iliyonao leo.
Kitendo cha gold kupatikana in a limited quantity ndio kunaihakikishia ukuaji wa thamani yake miaka nenda rudi. Na iko stable haiathiriki kwa inflation kama hizi Fiat curencies tunazotumia.
Forex huikuiti dhahab ikizungumzwa kiivo kwasababu kule kuna Ma-Trader kibao sio Investors wengi. Mfanya biashara hutaka faida papo kwa papo so ile buy and sell zimewatawala. Na hii buy and Sell kwenye Gold haina faida. Kwasababu Gold Iko very stable, zile shake za apa na pale ili ununue au kuuza chap chap ni za nadra.
Case ambayo iko tofauti kwa Investors, wanaofanya Buy and Hold kwa mda mrefu, unanunua unatunza. Hapa Gold ndio huwa taam. Kwenye long run inagain Value, tumeanza mwaka 2012 1,oz ya dhahabu ikiwa dola 1,600, miaka ya kati ilishuka mfano kama 2016 ilifikia dola 1100 lakini sasa 2022 1,oz ya dhahabu ipo kwenye 1,826.
Maana yake nini, ni kwamba kama mtu angekua anamiliki dhahabu ujazo wa 3,527oz ambazo ni Kilo 100 za dhahabu. 2012 kipindi cha ounce 1 kwa 1,600 dolla alikuwa na asset ya dolla 5.6Mil, kwa kuitunza tu hivi sasa angekuwa na asset ya dola 6.45Mil. Hilo ongezeko sasa litafakari kwa Nchi ambapo wanaweza kununua nyingi zaidi.
Hapo usisahau kujiuliza vipi kwa wale waliozipata miaka ya 2016 ilipokuwa around 1,100 hivi dola. Ni kwamba waliwekeza 3.8Million dola sasa wana 6.45Mil dola. Of course hizo ndizo real assets ambazo Russia kayafungua macho mataifa mengine wajifikirie.
Tarehe kama ya leo mwaka jana Euro 1 ilikuwa na thamani ya 2,770. Kama ningeweka akiba ya Euro 50k bank, ambazo ningeweka bank Million 138.5 za kibongo ili account iwe updated with Euro 50k. Sasa endapo ningeitaka hivi sasa nitapata Euro zangu 50k kwa rate ya 2,467. Yani nitapewa Mil 123.5 za kwetu.
Hio ni Loss ya mwaka mmoja tu kwa kuhifadhi pesa hizo. Kutoka 138 up to 123, drop ya kama Mil 15 hivi. Je umewaza kwa mataifa yaliyo hifadhi Euro nyiiiiiiiingi zaidi hali ikoje? Ni mbaya na hizo hasara wanazipata kwasababu ya maamuzi ya kijinga ya hao Morons wa hapo EU.
Tukisema zibaki nje ya mipaka yao tutaendelea kua WATUMWA wao siku zote. Tutakuwa tunaathirika kwa kila ujinga unaofanywa na Viongozi wa mataifa hayo.
Binafsi naweza sema Hatuitaki dola wala Euro, zikufe tu [emoji23] au ziendeleee kua local huko huko kwao. Wakiyavuruga athari ziishie huko huko kama ambavyo hapa nchini tukizingua tunajiumiza wenyewe na Tanzania Shilling yetu... Inabidi itafutwe ama Tutafute another means of exchange kwenye International Trade. Sio hayo makaratasi yao. Hatukuumbwa nayo tuseme bila hizo hakuna kinachowezekana.