LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Ngoja nilale nisubiri updates za hapo baadae baada ya jamaa yetu putin kuamuka na kuwapiga Ukraine cha asubuhi kwanza kabla ya negotiations kufanyika leo.
Uzuri sisi na ndugu zetu wa Moscow tunatumia muda sawa.
 
umeandika utopolo we toka uzaliwe uliona jambo gani linskubalika na watu wotee...
 
Heko kila ulicho sema, sisi watanzania akili kisoda halafu unawaza pipa,
 
Ni Mpalestina gani aliipiga serikali yake?
Ni raia gani wa Iraq aliipiga serikali yake kwenye vita ile?
Kwa Libya nakubali
 
Uingereza imeiwekea vikwazo nchi ya Belarus kwa kuisaidia Russia kuanzisha mashambulizi kutoka nchini humo.

Lakini raisi wa Belarus Alexander Lukashenko yeye bado hajawekewa vikwazo hivyo.
 
Molotov cocktails zile lazima zinaleta maafa japo kidogo. Huwezi pakia petrol hovyo mji mzima alafu eti hakuna zinakoshika moto bahati mbaya
Hizo zilitumika sana wakati wa Vita kuu ya pili na si hii ya sasa itaua wengi wasofahamu namna ya kuzitumia.

Hata hivyo Russia imetoa onyo usiku huu watu waondoke itaanza kudondosha makombora makali yanopenya majengo hadi ardhini.
 
Urusi ikianguka silaha zake ndio zitazubaa kwenye masoko sasa. Marekani bunduki zao za M2 Garand za vita ya pili ya dunia zilitumika kwenye vita kibao hapa Afrika hasa kule Ethiopia. Yugoslavia baada ya kuanguka silaha zake ndio zinatumia Middle East. Marekani mbona huwa wananunua AK-47 na kuwapa magaidi ila wao huwapamba na kuwaita "moderate rebels".

Silaha zinadhibitiwa kukiwa na serikali imara. Na kuuza silaha sio kuanzisha vita, kwanza Marekani haijawahi wapa wapiganaji wa siri silaha inazotengeneza yenyewe
 
Ni Mpalestina gani aliipiga serikali yake?
Ni raia gani wa Iraq aliipiga serikali yake kwenye vita ile?
Kwa Libya nakubali
Uwe unajishughulisha akili yako wakati mwingine, huko Palestina PLO na Hamas wanaelewana? Iraq iko wazi kuna raia hawakumtaka Sadam na walishirikiana wamarekani kumuua. Na hiyo Iraq muamerika kaondoka kitambo, mbona hawatulii kama ilivyo Libya? Mrusi ni muhalifu tu kama wahalifu wengine.
 
I agree with you humu kuna baadhi ya amateurs wanafanya mtazamo kwa kushabikia nchi fulani. Urusi kaonesha performance mbaya sana ukizingatia anapigana na competitor mdogo. Zile columns za magari ya jeshi zinazoenda bila air cover, kukosa supplies, kupigana bila kwanza kuharibu airforce ya adui na viwanja vyake, etc.

Urusi hajanishawishi kama anaweza wage an all out war with NATO. Hata asipowekewa vikwazo akawa na uchumi uleule na support kubwa kwake ila uwezo wake kwenye field ni hauridhishi. Unapigana na jirani, alafu some of your troops wanakosa mafuta wanatelekeza silaha. Ukisafiri 10,000 km itakuaje si majeshi yanakuwa isolated.

Tatizo la Urusi ni logistics. Vita na Japan napo Urusi ilifeli kufanya mobilization ya wanajeshi na silaha kutoka central na Western kwenda far East. Vita ya kwanza walikuwa poor hivihivi walipigwa na Ujerumani karibia battle zote, ila Ujerumani ya WW1 ilikuwa inapiga hakuna mfano. Vita ya pili ndio walifanya mass production pale Stalin alipodai "Quantity has a quality all its own" wakatoa units nyingi za silaha ila ubora wa kawaida na walishinda kwa hili.

Wanajeshi wa Urusi kufa sana haiwatishi kivile. Vita zao zote huwa wanakufakufa. Nchi inayoogopa zaidi wanajeshi kufa ni Israel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…