LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Sasa hzo picha mbili utatujazia uzi kwa kuzipost kila mara kwa taarifa yako airport imeshatekwa huko
 
Kuna watu wanadhani bara la ulaya hadi america kukichafuka kwa vita Africa itakuwa na usalama naona hamuoni mbali

Vita sio kitu cha kuombea kabisa, uchumi wa mafuta na maligafi nyingine muhim zimeshikiliwa na wazungu yaani ikitokea vita vikubwa vikubwa vimezuka tegemeeni anguko la uchumi la kutisha, bei za bidhaa zitapanda mara kumi mtakuja kulia lia hapa mna ugumu wa maisha

Mpo kwenye nchi ambayo inatembeza bakuli kila kukicha kwa wazungu na ushahidi mnao kuwa ni ishara kuwa nchi mnayoishi pesa za pato la ndani hazitoshi kupambana na shuhuli za maendeleo ndio maana kila kukicha kazi kukopa kwa wazungu sijawahi sikia mnakopa Russia

Hadi madawa ya TB na mengine mengi ya kurefusha maisha ni misaada ya wazungu, wale leo hii wakiingia vitani vita ikawa ya kutisha nawahakikishia mtarudi hapa kumlaumu mrusi kwa nini ameanzisha vita

Ombeni amani na maridhiano msiombe vita mtakuja kulia lia hapa
 
Hatukusababisha vita sisi wacha wauane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…