Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

The reason for Russia advance everyday inch by inch!
 
Habari za michongo Mnakaa buza kwalulenge na kutunga story hazina source ingia mtandaoni uone ghala kubwa la silaha crimea linawaka moto muda huu Himars ni moto wa kuotea mbali.
 
Aisee hivi nyie watu mkoje?! Propaganda gani hizi zilizopinda?! Eti Russia anapigana na dogo Ukraine?!?! Kwanini mnajitoa ufahamu?! Russia anapambana na zaidi ya nchi 30...anapambana na NATO, Europe, West yote Canada, EU, Australia, Japan na Ukraine yenyewe...Yaani nchi zote hizo zinapambana na Russia kiuchumi, kisiasa, kijamii na kijeshi...you can imagine hapo superpower ni Nani..
 
Duh Hakika Tz iliwahi kua ya tatu kwa ujasusi duniani.
 
Vita haina cha super power wala nini.

Ona urusi kaenda vita miezi 6 na nchi ndogo sana kijeshi.

Marekani nae alitolewa mbio na Vietnam, Somalia na vinchi vingine vidogo mpaka one man army Osama Bin LD nae alimtoa kamasi
Kama Ukraine kwa uwezo wa Kijeshi iliokua nao nchi Pekee kwa upande wa NATO ambayo ingeweza ikawashinda Ni Turkey na USA tu lkn bado umeona Ukraine ilikua Ni nchi ndogo ya Kijeshi.

Hakika Kuna Muda kazi ya fuvu hua Ni kushikilia magego ya meno tu.
 
Hehehe,sema ukweli
1. Ukraine ilianza kupewa misaada toka mwaka 2014,na sio kuanzia mwezi march.
2. Ukraine ina jeshi kubwa,na hakuna nchi yoyote ingeweza kupigana nayo kwa nchi za ulaya.
3. Ukraine haipigani peke yake,hili unalijua, kuna wanajeshi wengi kutoka nchi za NATO,na mercenaries wanatoka nchi nyingi za magharabi.
3. Tungetegemea Urusi ndio ishindwe kwa sababu, Ukraine inawasaidiwa na EU, US kwa intelligence,silaha,pesa, propaganda, Urusi imewekewa vikwazo vingi na vikubwa kuliko nchi yoyote duniani.
4. Urusi haipo kwenye "real war" Ila inafanya SMO. Yaani,inapigana vita,huku ikitoa misaada ya chakula na mahitaji mengine kwa wananchi,huku ikijenga miji iliyoharibika kwa vita.
5. Urusi haijatumia jeshi lake Kamili, (30%)yaani professional soldiers,inatumika vijana waliofanyuwa recruitment ya mda kuingia vitani, Urusi ikiingia kwenye vita kamili na kutumia silaha,utaionea huruma Ukraine. Usifikiri marekani ni mjinga kutamka hadharani kwamba hawezi kuingia vitani na Urusi moja kwa moja.
 
Wawanyonge kabisa
 
Na zimeishiwa silaha kwenye maghala Ila Dume anaendelea kuchukua maeneo 🤣🤣💪🇷🇺
 
Braza shkamoo aseee😁😁😁




⭐️⭐️⭐️⭐️⭐️
 
Acha mahaba, mbona russia ameinjinia vita kule syria dhidi ya hawa hawa nato waliotaka kumtoa asad na akashinda!?
 
Breaking News: Ma benki makubwa zaidi Marekani JPMorgan na Bank of America zimerudi Russia [emoji635] . Hizi ni Bank namba 1 na 2 kwa ukubwa (assets) Marekani [emoji631].

Hii ni kutokana na ongezeko la watu wengi huko Wall Street kutaka kununua bonds (Hati fungani) za Russia.

Benki hizi ni miongoni mwa benki 6 kurudi kwenye soko la Russia ikiwa baada ya Treasury Department ya US kupiga marufuku investors kununua hati fungani au hisa zozote kutoka Russia mwezi wa 6 mwaka huu.

US Treasury Department wametoa muongozo mpya unao ruhusu benki hizi kurudi kwenye soko hilo.

Barclays, Citigroup, Deutsche Bank na Jeffries Financial Group pia wamerudi.

Taratibu, kimya kimya na kwa kunong'onezana ili kuficha aibu sunctions za mchongo zinamegwa.
 
Kwa mwendo huu, hadi mwakani, sanction pekee itakayosalia itakuwa Lavrov asikanyage Marekani. Zingine zote zinaenda kuyeyuka.
 
Wanasema ukiinanga sana Russia na kusapot west ni rahisi sana kupata viza kwa sabab jamaa ukishawapa data zako wakat wa maomb wanafatilia sehem zote ulizotumia email,namba ya sim km kiunganish.

Na ndio maana jamaa wanahaha kusapot hata yale ambayo wao wenyew hawayaelew ili mrad wapate wepes wakat wa kujilipua.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…