Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Buseresere,
Kasungamile,
Isunganghoro,
Nyarugusu,
Nyakanazi
Katoro,
Chato,
Rubondo,
Msalala,
Kizugwangoma,
Nyampulukano,
Karumo,
Buhongwa,
Kisesa,
Ibinzamata,
Kizumbi,
Ipuri,
Ipilili,
Igalula,
Sikonge.[emoji14][emoji1787][emoji123][emoji3581]

Nyakamwaga, Bufunda, Lwakakombe/Busanda, Buyangu, nyabulolo sijaziona
 
Acha mahaba, mbona russia ameinjinia vita kule syria dhidi ya hawa hawa nato waliotaka kumtoa asad na akashinda!?
ISIS na wenzake sio wor
Yani hata wanaopeleka helmets na madawa nao inaita wako vitani. Aah uzuri visingizio vishapatikana, tumetoka kwenye kushinda Ukraine kwa siku tatu tumekuja kwa Russia inapigana na nchi 30
 
Ukute kafa au kaumia sana
Tatizo wanataka kuonekana kwenye kama sehemu ya morali na propaganda. Hapo wapo Ukraine, hata uende jengo gani usimame mbele Ukrainians wanaweza fuatilia kujua hilo jengo liko wapi. Walimtrack kirahisi alipopiga picha hiyo wakajua yuko hapo na wakafanya shambulizi baadae kidogo. Yawezekana alikuwa ashaondoka labda kama alichelewa sana. Kwa sasa wanapenda kupiga picha kisha wanazipost baadae
 
Naona umeshiba magimbi mkuu yani unaropoka tu ๐Ÿ‘Ž๐Ÿ‘Ž๐Ÿ‘Ž๐Ÿ‘Ž
 
Putin ana akili sana,hawa western huwa wanaanza kuharibu Taifa husika kwa kupandikiza culture zao mwisho wanakuweka katika kwapa zao.Mchezo huo wameufanya huku kwetu Africa hadi Leo tunagombana sababu ya dini zao za Kikiristo na kiislam,wametubalisha life style yote kiuchumi,kijamii hadi kisiasa-tunahangaika kila kukicha lakini hatuwezi.

Angalia mataifa yote yanayoleta resistance kwa western ni mataifa ambayo wanafuta culture zao kuanzia kwenye lugha,elimu,uchumi.Ukisha mruhusu MTU aangamize culture yako jua atakutawala kiurahisi sana.

Hata baadhi yetu tunaomtetea Ukraine na western ni kwa sababu culture zao zimisha tuingia katika Bongo zetu ndio maana hivyo.
 
Nashukuru kwakumuuliza swali nlotaka kumuuliza
Akikujibu unitag MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afghanistan ile iliyoishinda Soviet Union nzima?
Uliwahi kupewa ushauri huko nyuma na mdau mmoja hapa kama sio tameer basi ni abdulqadirj... Alikushauri vizuri tu kua muungwaa akivuliwa nguo huchutama.

In case hukuelewa maana ake, ni kwamba jaribu kuficha aibu zako. Ukiishiwa hoja kua mpole tu usilete mahaba ushabiki kujidhalilisha.

Soviet-Afghan War, miaka 9 kuelekea 10. Results ilikuwa ushindi kwa Afghan Mujaheed na withdrawal of Soviet troops eneo hilo. Sijawahi ona mahala popote pro Russia wakikana kuhusu hilo.

Je Unawajua walio kua nyuma yao hao Mujaheed?

Again in case huwajui ni hawa.
1. USA
2. Pakistan
3. Saudi Arabia
4. China
5. Egypt
6. UK
7. UAE
8. Israel
9. Of course na Iran akitoa support kwa Shia Factions Mujaheeed. Ushindi huo hakuna Pro-Russia hapa anaeukataa.

Hayo unajitoa ufaham kutoyajua.

Upande wa US na Taleban walijizoa kijiji kizima cha NATO. Ukifanya kujumlisha nchi za member wa NATO na wengineo zilikuwa over 50. Wataleban hawakua na support yoyote.

Tena kule wamepigana phase 2, phase ya kwanza Oct. 2001 hadi December 2014, January mapema tu ya 2015 wakaendeleza phase 2 hadi 2021 wakiondoka kwa aibu..

China, Iran, Russia, Pakistan, Saudi Arabia na Qatar kwa nyakati tofauti walituhumiwa kuwasadia watalebani lakini ni madai ambayo waliyakanusha.

Almost 20 yrs collective west wameondoka hapo Afghanistan kwa aibu. Kwanini hili mnalikataa, mnakwepa kukiri ukweli. Case ya Afghanistan pekee kama kumkichwa kuko vizuri inatosha kukujuza nani ni nani na nani ni nani.

Soviet Afghan War unai'refer miaka ya 1970+, unaizungumzia karne ya 20. US Afghan tunaongelea juzi, tunaongelea karne ya 21.

Hatuwakatazi kufanya reference za namna hiyo, ila mkizifanya mzifanye mkiwa open minded. Msichague cha kujifunza kwenye historia kwani haitawasaidia kitu zaidi ya kushibisha kiu zenu za mahaba.

Rejeeni tena kwenye historia mjifunze tawala na empire zinavyozaliwa, zinakua kisha zikaanguka. Mjifunze mengi mpate maarifa ndugu zetu wa mchambawima.

Truth denial ni dalili moja wapo za kurukwa akili. Sometimes mkiitwa wajinga, wapumbavu au hamjielewi msinune kwasababu dalili zote za hali hiyo mko nazo.

Katika text zote zilizo tangulia hakuna cha maana ulicholeta zaidi ya kuhamisha magoli.

Pole sana mjuba... Hujachelewa njoo tu tukupe ukwaju uchachue mahaba hayo ambayo kila ukicha yanakuvunjia CV zako za mda mrefu mitaa hii...
 

Endeleeni kujipa moyo na matumaini mkifikiri Russia ni Libya nawapa pole. Russia wenzenu wana plan A-Z kuwazuia ni ngumu sana. Waziri wa fedha wa Ukraine juzi amelalamika hawana fedha za kuwalipa wanajeshi wao vitani hivyo wanalazimika kuprint pesa zaidi, misaada inatolewa kiduchu sana. Ukraine anaachwa yatima maana misaada anapewa hakuna anachofanya maana kila siku Warussi wanamega maeneo taratibu.

Nikikuuliza silaha zote na misaada anayopewa pamoja na mbinu za kijasusi mpaka sasa amefanikiwa kwa asilimia ngapi??

Haya unayosema Ukraine angekua anapambana na Libya hivi ningekuunga mkono ila kwa Russia endeleeni kujipa matumaini kama waathirika wa HIV.

Kama mbinu anapewa na mataifa makubwa duniani bado silaha anapewa za kutosha lakini bado mnashindwa kumrudisha nyuma. Kubomoa madaraja ndo mnafikili kuna mzuia Russia?? Kweli Tim upinde akili zetu zimekaa kiupinde
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ