Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

VLADIVOSTOK, Russia (Reuters) -Russia's biggest natural gas pipeline to Europe will not resume pumping until Siemens Energy repairs faulty equipment, Gazprom’s Deputy Chief Executive Vitaly Markelov told Reuters on Tuesday.
 
Kuna watu wengi walikuwa wqnajiuliza kuhusu uwezo wa urusi na kutumia muda mrefu na Kwa gharama kubwa kuiendesha hii operation, kuna watu walisema kuwa operation hii imechukua muda sababu ni

1) Ni kutokana na ukubwa na uimara wa jeshi la Ukraine

2) Ni uwezo mdogo wa urusi kijeshi

3) Ni Kwa kuwa urusi anajali Sana raia Kwa hiyo hataki kuua watu wasio na hatia, ndiyo maana anaenda taratibu Kwa uhakika ili kupunguza madhara ya kivita

Lakini kwangu Mimi naweza nikachukua namba tatu, lakini Siyo Kwa uzito huo,

Sababu ninayoiona Mimi hii operation inaenda taratibu Kwa mkakati maalumu kutoka Moscow, kitendo cha operation hii kwenda taratibu ni Kwa sababu hii

Wakati Vita inaanza mrusi alikuwa mkali na aliwapiga bit nchi zote za ulaya kuwa wasijaribu kuingilia ugomvi huo na atakaye jaribu atakiona cha Moto, na katika kipindi hiki ndicho urusi ilikuwa inatishia kutumia nukes, na KOSA KUBWA ambalo EU,NATO na USA walifanya ni kuogopa na kukaa pembeni Kwanza wakimsoma mrusi, katika kipindi wanamsoma mrusi ndipo west wakaanza Kwa kujaribu kupeleka silaha Ukraine na walipolleka silaha urusi akaonyesha kama kazidiwa na kurudi nyuma na kuachana na Kyiv, kitendo hiki kiliwatia moyo Sana Ukraine, NATO na USA Kwa kudhania kumbe wanaweza kuimaliza urusi,
Ndipo USA na NATO pamoja na EU wakaungana Kwa kupeleka silaha nyingi Ukraine ili waweze kummaliza moja Kwa moja urusi, na ikiwezekana wakomboe Crimea huku wakiweka vikwazo vingi zaidi Kwa urusi ili ashindwe kuiendesha operation yake yake, unajua baada ya urusi kugundua kuwa west wameshanasa akifanya nini? [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Ndipo Putin alikwenda China na taarifa zikavuja kuwa urusi imeishiwa silaha na chakula, hapa west wakavimba kichwa wakiona Zama za urusi zinaenda kuisha,

Baada ya west kupeleka silaha nyingi na za kisasa ndiyo muda mzuri mrusi alikuwa ameua ndege wawili Kwa jiwe moja

1) Kwanza alipata kujua technology iliyotumika kwenye kutengeneza silaha zile akaangalia udhaifu wake na pia aliangalia ni Kwa jinsi gani anaweza kuzidhibiti zisilete madhara makubwa

2) Kupitia hili nchi kama Poland ilisafisha ghala lake la silaha lote na kupeleka Ukraine, Kwa namna moja ama nyingine mrusi alisababisha nchi nyingi za ulaya zipunguze hifadhi zao za silaha Kwa kutegemea Ukraine atashinda Vita

Kitu ambacho hawakuamini ni pale mrusi alipoziangamiza zote na nchi nyingi zimejikuta zimeishiwa silaha mpaka zinaomba msaada

Sasa mrusi baada ya kuona jamaa wamekiuka makubaliano akaja na mtego mpya

1) akaweka vikwazo Kwa nchi za EU kuwa wakitaka gas wanunue Kwa rubo, ulaya walivyo vilaza wakaingia kichwa kichwa kwenye mtego wakagoma kulipia gas Kwa rubo mrusi akakata gas, nchi nyingi ulaya wakajikuta wanatumia gas Yao ya akiba Kwa kuwa hawataki kulipia Kwa rubo lakini baada ya siku chache Ile gas ya akiba ikaisha wakakubali kulipia Kwa rubo lakini tayari wameingiza damage kwenye hifadhi ya gas, na mrusi Kwa kujua west wamemaliza gas Yao ya akiba, akaja na mtego wa pili akapunguza kiwango cha kupeleka gas ulaya hii ikasababisha gas wanayoipata ni Ile itakayowawezesha kuishi sasa hivi tu hakuna gas ya akiba

2) baada ya kuona tayari vile zile nchi ndogo ndogo zimenasa akaanza kudeal na nchi kubwa kama ujerumani ambayo ina hifadhi kubwa,
Akafunga bomba la kupeleka gas ujerumani Kwa kisingizio kuwa pangaboi lilipo Canada ndilo linahitajika ili kuweza kufungwa ili gas iende ujerumani, yakaingia mabishano Kati yao wenyewe west na kipindi hicho chote ujerumani alikuwa anatumia gas yake ya akiba mpaka wanakuja kupata muafaka na kufunga bomba mjerumani kashatia damage kwenye hifadhi yake ya gas, kibaya zaidi mrusi akaja na tangazo la kupunguza kiwango cha kupeleka gas ujerumani kutoka 100% hadi 60%, hii maana yake ujerumani atumie hiyo gas bila kuweka nyingine akiba ,
Baada ya kufanikiwa hilo mrusi kaja na njia mpya kila mwezi anafunga bomba Kwa ajili ya matengenezo kipindi hicho nchi za EU zinalazimika kutumi gas ya akiba, lengo kuu la urusi ni kuhakikisha ulaya nzima kipindi cha baridi hakuna nchi yenye akiba ya gas

Sasa ulaya ndiyo wanagundua sasa lengo la mrusi ndiyo maana zimezuka hoja za kuwasha vinu vya nuclear vilivyopo ulaya ili kupata nishati, kibaya zaidi hii mitambo ya nuclear imekaa muda mrefu bila kufanya kazi kwahiyo wanahitajika wataalamu ili kuweza kufufua hiyo mitambo kibaya zaidi hao wataalamu wanapatikana urusi,
Kitu kingine hiyo mitambo inahitaji kufungwa vipuri vipya, ambapo hivyo vipuri vinapatikana Russia
Pia wanahofu kutokana na mitambo hiyo kukataa Kwa muda mrefu bila kutumika kuna uwezekano wa baadhi ya maeneo kuwa yameliwa na kutu na ikatoka mionzi ikavuja,
Kitu kingine ni kuwa hata wakiwasha hiyo mitambo ili upate umeme unaohitaji itabidi wasubiri kama mwaka mmoja, kitu ambacho matatizo waliyokuwa nayo ulaya hayawapi nafasi ya kusubiri Kwa muda huo

Sasa faida ambayo mrusi kapata baada ya hii operation kuchelewa ni

1) kujua ulaya Wana silaha gani na zinauwezo gani, na wamejua ni namna gani wanaweza kuzizuia ili zisilete madhara makubwa

2) kupunguza hifadhi kubwa za silaha zilizopo kwenye mataifa ya ulaya

3) kupunguza uwezo wa NATO na EU kwenye nishati hii inasaidia mpaka sasa kuwa hawana uwezo wa kuzalisha silaha nyingi Kwa wakati mmoja kutokana na upungufu wa nishati WA kuendeshea viwanda vyao vya silaha

4) kupitia vikwazo ambavyo ulaya wamaiwekea urusi nchi nyingi za ulaya zimeyumba kiuchumi na hivyo kupunguza uwezo wao wa kuendesha Vita ya muda mrefu na mrusi

5) mpaka sasa hivi mmarekani kajua wazi kitendo Chao cha kusubiria kumsoma Putin anawaza nini juu ya Ukraine lilikuwa kosa kubwa maana kama sasa hivi vikitokea Vita basi MTU pekee atakayewajibika ni USA Kwa kuwa ameshajua EU na NATO wamekwisha choka yaani hawana uwezo wa kupigana Vita na taifa kubwa kama urusi, Kwa hiyo akiingia Ukraine yeye ndiye atakayeandamwa na akipigwa yeye maana yake ulaya nzima imeanguka

Kiufupi mpaka sasa mrusi yupo kwenye nafasi nzuri ya kupigana Vita hasa muda huu ambao baridi linaanza ulaya, naona kila dalili ulaya ikisambaratika bila urusi kuingia vitani, na ikisambaratika ulaya na marekani inatafata maana bidhaa za marekani zitapigwa ban nchi za Asia na kusababisha marekani akose soko la kuuza bidhaa, na kutokana na hali ya uchumi wananchi watafunga mikanda na hapo ndipo anguko la marekani lilipo
Hongera MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Europe does not have GAS, RUSIA has Gas.

Rasia does not have the technology to process and supply its Gas, Europe has the technology to process and supply Rusian Gas.

so kinachoitwa GAS WAR, wote wawili wanaumia Rusia anaumia Europe anaumia.

Then wanakuja mashabiki njaa wanapiga kelele ohoo USA atasupply, mara ohoo Rusia kiboko.

yaani utoto utoto.

Hivi kwa akili yako unafikiri Russia hana tech? Pole sana Russia anawachora tu. Afu nataka nikupe kitu kingine kwa faida yako kwenye mkataba kuna terms wanakubaliana Ili project iwe na faida pande zote 2 kama wewe unatuuzia gas bhs sisi tutakuuzia tools na kufanya service nknk.

Lazma project iwe na masilah pande zote lazima wote mfaidike ndomana unaona hata Gazprom Germany wana parcent wanayo. Uwe unafuatilia mambo na sio kukurupuka kama unataka kuwa keyboard warrior sawa.
 
Hii vita imesababisha njaa kali sana hapo Somalia na Kenya mamia ya watu wanakufa kila siku, mashirika ya misaada badala ya kuendelea kusaidia hasa somalia sababu shughuli za kilimo ni kama simesimama kwa muda mrefu sababu ya machafuko sasa yanapeleka misaada zaidi kwa wahanga wa vita Ukraine.

then kuna watu wameshiba uji JF wanashangilia vita na kukumbatia wasababishi wa vita kama vile wanagombania mabwana.

Yaani jitu zima linajua kusoma na kuandika, lina ama computer au simu au vyote, lina access ya internet, labda hata lina mke na watoto nyumbani, na wazazi wategemezi juu, liko JF linaandika "Urusi anasiraha ambazo hakuna nchi inazo", yaani utafikilia labda ni punguani labda, yaani.
Embu elezia Special Military Ops ya Russia imeletaje njaa Somalia?

Ngoja nikueleweshe kodogo. Ishu ya njaa ya Somalia ni pana Sana. Imesababishwa na Mambo mengi. Kwa mfano:

1. Endless war in Somalia. Somalia wanapigana Vita kila siku. Je, Special Military Op ndio imesababisha Vita Somalia?

2. Ukame. Ukame unatokana na mabadiliko ya tabia nchi. Je, Special Military Op ndio imesababisha ukame huko Somalia?

3. Watu kuishi kwa kuhama hama kutokana na Vita. People are not settled. Je, Special Military Op ndio imesababisha watu washindwe ku Somalia?

4. African Union inatakiwa ijitoe kusaidia njaa ya Somalia. Je, Special Military Op ndio imesababisha AU kushindwa kusaidia Somalia?
 
Ngoja nikueleweshe kidogo.

Kwenye hizi big projects, nchi zinajitahidi Sana kuhakikisha kwamba makampuni ya nchi yake yananufaika.

Ndio maana unaona kwenye both projects za Nord Stream 1 and 2 makampuni ya Ulaya yanapata tender za construction services or maintenance.

Vilevile ukiangalia project ya gas kwenda China (Power of Siberia) utaona kampuni za China ndio zikinufaika (zikiongozwa na China National Petroleum na Stroygazconsulting Ltd Liability).

Point yangu Ni kwamba, utandazaji wa mabomba ya gas sio technology ambayo hipo exclusive kwa Europe, hata China anafanya hata Japan anafanya (Japan and Russia wana project ya gas)

Kwa hiyo tambua kwamba Technology sio ishu ya kufanya Russia ashindwe kusambaza mabomba ya gas.

Yes, Europe Ni soko zuri la gas, hii nakubali. Na vilevile, kupungua kwa gas volume inayoenda Europe ina impact kwenye Revenue za Gazprom, ndio maana Sasa wanatafuta alternative buyers wa gas.
Mkuu acha propaganda wafanye wenyewe wazungu, acha kutetea mambo yaliyo wazi.

hizo maswala za contracting hazifanyiki politically namna hiyo, tender atapewa yule aliye na "know how", financing is available globally.

Mara ya kwanza Urusi walipoanza katakata ya GAS, hata kama ni kwa military weapon purpose, lakini walisema GAS TURBINE ILIKUWA CANADA KWA MATENGENEZO NA CANADA HAWAKI KUIRUDISHI katika muktadha wa sunctions.
---- maake Rusia hawezi hiyo kazi, anategemea Canada, at least kwa taarifa zilizopo.

Sasa karudia tena katakata, nayo anasema hivyo hivyo, makampuni ya Ulaya yenye yanafanya hizo maintenance yako restricted na sunctions.

Mbona MACDONALD ilipofunga canteen zake moscow, immedietely kampuni ingine iliendelea kuziendesha??
 
Rasia does not have the technology to process and supply its Gas, Europe has the technology to process and supply Rusian Gas
Nadhani aukubahatika kusoma makala hii mwaka jana.
---

Embu elezia Special Military Ops ya Russia imeletaje njaa Somalia?

Ngoja nikueleweshe kodogo. Ishu ya njaa ya Somalia ni pana Sana. Imesababishwa na Mambo mengi. Kwa mfano:

1. Endless war in Somalia. Somalia wanapigana Vita kila siku. Je, Special Military Op ndio imesababisha Vita Somalia?

2. Ukame. Ukame unatokana na mabadiliko ya tabia nchi. Je, Special Military Op ndio imesababisha ukame huko Somalia?

3. Watu kuishi kwa kuhama hama kutokana na Vita. People are not settled. Je, Special Military Op ndio imesababisha watu washindwe ku Somalia?

4. African Union inatakiwa ijitoe kusaidia njaa ya Somalia. Je, Special Military Op ndio imesababisha AU kushindwa kusaidia Somalia?
Tatizo hausomi uelewe.
Nimesema mashirika ya misaada ya ulaya yaliyokuwa yanawasaidia hao wasomalia dhidi ya njaa ambayo inasababishwa correctly na hizo sababu ulizozitoa, yanaelekeza fedha kwa wahanga wa ukraine. hilo ni moja.

Pili, unless ubishi uko damuni mwako, vita pia imesababisha njaa, sio somali na kenya tu, bali duniani sababu nafaka za Ukraine na Urusi zimezuiwa vitani.

Tatu, hata hapa Tanzania, labda kama huwa unakuta chakula mezani, hujui bei yake, vita imeleta njaa mpaka nyumbani kwako, unless hauelewi economics of hunger.
 
Nadhani aukubahatika kusoma makala hii mwaka jana.
---

Mkuu nazungumzia existing technology "not under construction technology", hata sisi mbona kipanya anadevelop electric cars.
 
Mkuu acha propaganda wafanye wenyewe wazungu, acha kutetea mambo yaliyo wazi.

hizo maswala za contracting hazifanyiki politically namna hiyo, tender atapewa yule aliye na "know how", financing is available globally.

Mara ya kwanza Urusi walipoanza katakata ya GAS, hata kama ni kwa military weapon purpose, lakini walisema GAS TURBINE ILIKUWA CANADA KWA MATENGENEZO NA CANADA HAWAKI KUIRUDISHI katika muktadha wa sunctions.
---- maake Rusia hawezi hiyo kazi, anategemea Canada, at least kwa taarifa zilizopo.

Sasa karudia tena katakata, nayo anasema hivyo hivyo, makampuni ya Ulaya yenye yanafanya hizo maintenance yako restricted na sunctions.

Mbona MACDONALD ilipofunga canteen zake moscow, immedietely kampuni ingine iliendelea kuziendesha??
Siwezi kujadiliana na mtu ambaye anasema kwamba big projects between countries are not governed by political will.

Pili, ile gas turbine ni aina ya Seimens. Na hao Siemens ndio wenye obligation ya ku service hiyo turbine yao. Sasa ulitaka Russia afanyeje?
 
Hivi kwa akili yako unafikiri Russia hana tech? Pole sana Russia anawachora tu. Afu nataka nikupe kitu kingine kwa faida yako kwenye mkataba kuna terms wanakubaliana Ili project iwe na faida pande zote 2 kama wewe unatuuzia gas bhs sisi tutakuuzia tools na kufanya service nknk.

Lazma project iwe na masilah pande zote lazima wote mfaidike ndomana unaona hata Gazprom Germany wana parcent wanayo. Uwe unafuatilia mambo na sio kukurupuka kama unataka kuwa keyboard warrior sawa.
Awachore tu na mwisho awapake rangi lkn mwisho wa siku kichapo kipo palepale
 
Tatizo hausomi uelewe.
Nimesema mashirika ya misaada ya ulaya yaliyokuwa yanawasaidia hao wasomalia dhidi ya njaa ambayo inasababishwa correctly na hizo sababu ulizozitoa, yanaelekeza fedha kwa wahanga wa ukraine. hilo ni moja.

Pili, unless ubishi uko damuni mwako, vita pia imesababisha njaa, sio somali na kenya tu, bali duniani sababu nafaka za Ukraine na Urusi zimezuiwa vitani.

Tatu, hata hapa Tanzania, labda kama huwa unakuta chakula mezani, hujui bei yake, vita imeleta njaa mpaka nyumbani kwako, unless hauelewi economics of hunger.
Embu nieleweshi ni nafaka gani kwa hapa Tanzania imeadimika au kukosekana kutokana na Special Military Op ya huko Ukraine..?
 
Hivi kwa akili yako unafikiri Russia hana tech? Pole sana Russia anawachora tu. Afu nataka nikupe kitu kingine kwa faida yako kwenye mkataba kuna terms wanakubaliana Ili project iwe na faida pande zote 2 kama wewe unatuuzia gas bhs sisi tutakuuzia tools na kufanya service nknk.

Lazma project iwe na masilah pande zote lazima wote mfaidike ndomana unaona hata Gazprom Germany wana parcent wanayo. Uwe unafuatilia mambo na sio kukurupuka kama unataka kuwa keyboard warrior sawa.
yaani wewe unaishi dunia yako mwenyewe.
Hemu nielezeee, sisi tukinunua mafuta tunawauzia tools gani??

why lakini humanity is racing to embracing ignorance to Knowledge?
 
Embu nieleweshi ni nafaka gani kwa hapa Tanzania imeadimika au kukosekana kutokana na Special Military Op ya huko Ukraine..?
Ndio maana nakuambia tatizo ni ukula kulala, haujui hata bei za vyakula ilikuwa shillingi ngapi kabla ya special operation na sasa ni shillingi ngapi.

labda soda utakuwa japo unaona watu wanavyolipia bili wanapokununulia.

unajua kwa nini soda zimepanda bei?

Au njaa unafikiri ni ziku moja uamuke ukute mama ako anakuambia kaenda kununua maandazi kakuta hawajapika sababu ngano haipo?
 
Ndio maana nakuambia tatizo ni ukula kulala, haujui hata bei ya chakula ilikuwa shillingi ngapi na sasa ni shillingi ngap?

labda soda utakuwa japo unaona watu wanavyolipia bili.

unajua kwa nini soda zimepanda bei?

Au njaa unafikiri ni ziku moja uamuke ukute mama ako anakuambia kaenda kununua maandazi kakuta hawajapika sababu ngano haipo?
Naomba nikunukuu: ".... vita imeleta njaa mpaka nyumbani kwako.... "

Ndio maana nikakuuliza kwamba, nieleweshe ni nafaka gani kwa hapa kwetu Tanzania imeadimika kutokana na hiyo SMO.

Je, kutaja hiyo nafaka huwezi?

Pia, unaweza kunielewesha ni wapi au mji gani kwa hapa Tanzania kuna hiyo njaa iliyosababishwa na hiyo SMO..? Maan unasema Tanzania Kuna njaa.
 
usinivute kuingia kwenye narrow minded box lako.

dunia ya sasa haina njaa inayosababishwa na ukosefu wa nafaka, njaa iko regulated na bei.

Kama kipato chako ni shillingi 15, na ulikuwa unatumia shillingi 10 kwa chakula, na sasa unatumia shillingi 14, basi jua unakabiliwa na njaa.

hata hilo mpaka waje wakuambie wazungu?
 
Ulaya hawawezi kureplace gesi ya urusi kwa namna yeyote ile. Wataongea tu lkn mwishowe watarudi kununua.

Geopolitics is more chess than checkers.

EUROPE ECONOMY

Europe's plans to replace Russian gas are deemed 'wildly optimistic' — and could hammer its economy

Hii ni kutoka cnbc

Kataa gesi ya urusi ukanunue ya senegal kwa bei maradufu ya ile ya urusi alafu urusi auze ya kwake china kwa bei ya kutupa. Alaf wewe na china mtumie gesi kuzalisha bidhaa alafu tukutane sokoni [emoji1787]
alafu tukutane sokoni [emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usinivute kuingia kwenye narrow minded box lako.

dunia ya sasa haina njaa inayosababishwa na ukosefu wa nafaka, njaa iko regulated na bei.

Kama kipato chako ni shillingi 15, na ulikuwa unatumia shillingi 10 kwa chakula, na sasa unatumia shillingi 14, basi jua unakabiliwa na njaa.

hata hilo mpaka waje wakuambie wazungu?
Nimeuliza swali very specific. Kama huna jibu, sema sina jibu na acha kuleta flip-flop.

Naona now unaleta ishu mpya ya "Dunia ya Sasa..." Kwa hiyo kama Somalia Kuna njaa na Tanzania kuna njaa pia..?
 
Back
Top Bottom