LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mkuu umeandika kweli ila kwenye asessment yako umejumlisha S400, S500 na S550
SU 57
T14 ARMATA
Siwezi andika vitu vya ajabu. S-500 gani unazosema, regiment yenye hizo systems chache sana iko deployed Moscow area. Hautokaa uione inatumika nje hasa kuvamia adui. Hawana hata regiment moja ya hiyo system na mpaka December mwaka jana bado walikuwa wanafanyia analysis.

Su-57 ni mpya, nikikuambia nionyeshe wapi Russia anazo hata Su-57 6 tu utakosa! Hana hela ya mass production na bado hajamaliza testing kabisa kuruhusu ziwe mass produced. Hawezi poteza good publicity na marketing strategy mbovu kwenda na Su-57 idondoshwe ionekane ni ndege bwege wakati anataka aiuze. Wapi uliwahi ona ndege moja tena fighter inabadili matokeo ya vita?

T-14 Armata the same applied na Su-57. Hivyo vifaru hata 50 hawana. Nani kakwambia vifaru 50 vinaweza fanya maajabu na kuamua matokeo kwenye nchi kama Ukraine iliyopewa msaada wa US made Javelin anti tank missiles.

Ili uishinde Ukraine unataka numbers. Numbers hazitoki kwenye silaha mpya zinazooneshwa kwenye maadhimisho wakati factories can't roll out mass production. Kitu pekee nilichoona ni matumizi ya Ka-52 Alligator ambayo ni modern helicopter. Moja imedondoshwa na US made Stingers MANPAD
 
Hivi unafuatilia haya mapigano. Hilo jeshi la Urusi mnaloliona linatisha mbona silioni? Urusi imepeleka special forces kufanya landing Kyiv mida ya mchana, Ukraine wamefanya counter attack wakiwa surrounded na Russia ameperform very poor. Nakwambia Urusi angekuwa amevamia Poland hapa tungekuwa tunashangaa
 
Acheni kuwa mnatazama video YouTube mnafanya conclusion kwenye battleground. Ndio yule yule aliyekuja kusema Su-57, T-14 Armata na S-500. Silaha ziko kwenye testing wewe unasema matumizi. Mbona hata US anazo hypersonic missiles on testing au kisa hazioneshi YouTube?

Kwanza hakuna nilikosema makombora ya Russia yatashindwa kufika mainland US. Nimesema Mrusi gani atafika US, taja kwa njia ipi na kupitia wapi au chombo gani
 
Bado kuna elements za uhai wa Ukrainian air defence capabilities pamoja na airstrikes za mwanzo asubuhi ya jana. Milipuko imetokea mjini Kyiv usiku huu, Western intelligence communities zinaendelea kutoa accurate data na briefings ila CNN ilisema kutakuwa na attack mjini Kyiv possibly artillery or missiles at 03:00 local time na sioni kama imetokea. Huwa siwaamini CNN moja kwa moja.

Ministry of Defence inasema losses kwa Russia ni 30 tanks, 130 armoured combat vehicles, 6 helicopters, na ndege 7. Ukraine imekwishapoteza wanajeshi 137
 
Kuna ndege moja kubwa imedondoshwa mjini Kyiv muda si mrefu, kwa mlio wa engines inaweza kuwa IL-76 airlifter. Sidhani kama itakuwa ni bomber. Kuna uhai bado kwenye air defence ya Ukraine, vigumu kufanya landing bila kuwa na anti access/aerial denial (A2/AD)
 
Vyanzo vyako vya habari ni vipi?..
Vyombo vyongi vya habari viko biased..either vipo upande wa Ukraine au vipo upande wa Russia.
Kupata reliable news info. ni kazi.

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Watu wanatumia nguvu kulingana na adui.

Nguvu dhidi ya ukraine sio itakayotumika Vs any NATO member.
 
we ni mjenda wa marekani au Urusi, au ni shabiki tu
 
CNN inasema kuna Su-27 ya Ukraine imedondoshwa na SAM ya Urusi
 
Unam- underrate sana Russia, nadhani movie za kimarekani zimekufanya uwe hivyo.

Yani Poland ilete ubabe kwa Russia?? Hivi hiyo nchi mnaichukuliaje kijeshi??

Uzuri ni kwamba wewe upo nyuma ya keyboard na wala hujui chochote kuhusu vita, wamarekani na wababe wenzie wanatambua Russia ni nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…