LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Mkuu umeandika kweli ila kwenye asessment yako umejumlisha S400, S500 na S550
SU 57
T14 ARMATA
Siwezi andika vitu vya ajabu. S-500 gani unazosema, regiment yenye hizo systems chache sana iko deployed Moscow area. Hautokaa uione inatumika nje hasa kuvamia adui. Hawana hata regiment moja ya hiyo system na mpaka December mwaka jana bado walikuwa wanafanyia analysis.

Su-57 ni mpya, nikikuambia nionyeshe wapi Russia anazo hata Su-57 6 tu utakosa! Hana hela ya mass production na bado hajamaliza testing kabisa kuruhusu ziwe mass produced. Hawezi poteza good publicity na marketing strategy mbovu kwenda na Su-57 idondoshwe ionekane ni ndege bwege wakati anataka aiuze. Wapi uliwahi ona ndege moja tena fighter inabadili matokeo ya vita?

T-14 Armata the same applied na Su-57. Hivyo vifaru hata 50 hawana. Nani kakwambia vifaru 50 vinaweza fanya maajabu na kuamua matokeo kwenye nchi kama Ukraine iliyopewa msaada wa US made Javelin anti tank missiles.

Ili uishinde Ukraine unataka numbers. Numbers hazitoki kwenye silaha mpya zinazooneshwa kwenye maadhimisho wakati factories can't roll out mass production. Kitu pekee nilichoona ni matumizi ya Ka-52 Alligator ambayo ni modern helicopter. Moja imedondoshwa na US made Stingers MANPAD
 
Usiwachukulie poa warusi they are not military slouches as you think.

Hiyo ni story ya zamani, mwaka jana tu waingereza walikuwa na inquiry nuclear submarine yao mpya ilifuatwa na chombo cha Russia kwa masaa kadhaa bila ya wao kujua; walipoona awajagundulika kwa muda mrefu warusi wakawawashia sonar tupo nyuma yenu.

EU kwenye hili ni wachokozi ni sawa na U.S kufikiria tu kuwa rafiki wa karibu na N.Korea achilia mbali kuweka military base; China awezi kuruhusu kirahisi ilo jambo miaka 800.

EU wamesogea kwenye mipaka ya Russia nje ya makubaliano yao mpaka imekuwa too dangerous for comfort kwa upande Russia na bado wanataka waimeze na Ukraine; jamaa washari.
Hivi unafuatilia haya mapigano. Hilo jeshi la Urusi mnaloliona linatisha mbona silioni? Urusi imepeleka special forces kufanya landing Kyiv mida ya mchana, Ukraine wamefanya counter attack wakiwa surrounded na Russia ameperform very poor. Nakwambia Urusi angekuwa amevamia Poland hapa tungekuwa tunashangaa
 
Sio kwamba mrusi kaingia vile kutokana na jinsi myukrein alivyo, sasa kama Ukraine haiko imara saana ya nini kutumia miguvu mingi zaidi.. Mrusi aamue kufanya lake kisha mpoland ammzuie, masihara hayo mzee, mtu mwenye nguvu ya kijeshi namba 2 duniani jnamdharau kiasi hiki, acheni ushabiki.
Hilo moja pili, ikitokea vita ya magwiji hayo itakuwa ni piga nikupige, hypersonic missiles za mrusi zitaland kwa mmarekani vizuri tu, mrusi ana makombora ya kupiga popote duniani, ila sema tu vita hii itapiganwa ndani ya urusi, mmarekani atajaribu kuingia na kushambulia kutokea kambi zake za karibu. Ila mrusi atapiga kutokea kwake na sio kuzuia tu, sio Chelsea ya mourinho ile.
Acheni kuwa mnatazama video YouTube mnafanya conclusion kwenye battleground. Ndio yule yule aliyekuja kusema Su-57, T-14 Armata na S-500. Silaha ziko kwenye testing wewe unasema matumizi. Mbona hata US anazo hypersonic missiles on testing au kisa hazioneshi YouTube?

Kwanza hakuna nilikosema makombora ya Russia yatashindwa kufika mainland US. Nimesema Mrusi gani atafika US, taja kwa njia ipi na kupitia wapi au chombo gani
 
Bado kuna elements za uhai wa Ukrainian air defence capabilities pamoja na airstrikes za mwanzo asubuhi ya jana. Milipuko imetokea mjini Kyiv usiku huu, Western intelligence communities zinaendelea kutoa accurate data na briefings ila CNN ilisema kutakuwa na attack mjini Kyiv possibly artillery or missiles at 03:00 local time na sioni kama imetokea. Huwa siwaamini CNN moja kwa moja.

Ministry of Defence inasema losses kwa Russia ni 30 tanks, 130 armoured combat vehicles, 6 helicopters, na ndege 7. Ukraine imekwishapoteza wanajeshi 137
 
Kuna ndege moja kubwa imedondoshwa mjini Kyiv muda si mrefu, kwa mlio wa engines inaweza kuwa IL-76 airlifter. Sidhani kama itakuwa ni bomber. Kuna uhai bado kwenye air defence ya Ukraine, vigumu kufanya landing bila kuwa na anti access/aerial denial (A2/AD)
 
Vyanzo vyako vya habari ni vipi?..
Vyombo vyongi vya habari viko biased..either vipo upande wa Ukraine au vipo upande wa Russia.
Kupata reliable news info. ni kazi.

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Hivi unafuatilia haya mapigano. Hilo jeshi la Urusi mnaloliona linatisha mbona silioni? Urusi imepeleka special forces kufanya landing Kyiv mida ya mchana, Ukraine wamefanya counter attack wakiwa surrounded na Russia ameperform very poor. Nakwambia Urusi angekuwa amevamia Poland hapa tungekuwa tunashangaa
Watu wanatumia nguvu kulingana na adui.

Nguvu dhidi ya ukraine sio itakayotumika Vs any NATO member.
 
Assessment niliyofanya mpaka sasa kwa Russian landing forces, their military gears, troops, tectics nakuhakikishia Russia hana uwezo wa kuvamia Marekani. Labda hiyo Marekani uwe unaisema iliyochorwa kwenye kikaratasi chumbani kwako umeiweka uvunguni mwa kitanda. Poland tu the way walivyo wanaweza mount resistance kwa invading Russian forces. Uturuki hii pekee inaweza zuia landing kama iliyofanyika leo.

Silaha kubwa zilizotumika leo: ukituma Mi-8s na Ka-52s unakutana na MANPADS na short range air defence systems, ukituma tanks ardhini unakutana na Uturuki au Poland wanazo German made Leopard 2 na ATM za kutosha. Ukija na Sukhoi na MiG haziko stealth hata bila ground radar Poland wakinyanyua AWACS mbili tu angani zinatoa mwongozo wa fighters zao kushambulia adui akiingia anga lao. Russia ikitumia artillery, self propelled howitzers na MRLS kama Smerch, Uragan hao members wa NATO karibia wote huwa wana counter battery radars. Kitu pekee ambacho Russia ana edge ni missiles hizo Kalibr zilizotumwa kama 160 hivi. Russian navy ilikuwa na meli zaidi ya 12 baharini na imeteka mji wa Maliupol na navy base ya Ukraine. Meli zinaleta shida kiasi, hakuna ASM za range kubwa ila landing crafts zitazuilika. Kuna nchi kibao hapo zinaweza hold more than a month zikivamiwa na Russia.

Ukraine sio level za Urusi na haina silaha za kutosha, wala sioni kama ina mobilization ya maana, kwanza jeshi ni 160,000 hivi ukiongeza na reserve wasiofika milioni moja. Hata hivyo Ukraine imefanya counter attack mida ya jioni, imepeleka mashambulizi kujaribu kuzuia airports za karibia na mji mkuu kutekwa. Naamini wakishindwa wataweka craters kwenye runways ili ndege za Urusi zisitue hapo.

Siwezi ilinganisha Russian na Marekani, ikitokea vita kati yao doctrine zao zinaonesha kabisa kwamba Russia atakuwa na defensive position na US atakuwa na offensive position. Hatotokea mwanajeshi yeyote wa Urusi aingie ardhi ya Marekani. Kwa mfano atapita wapi na kwa kutumia nini?
Kuhusu nuclear capabilities achana na idadi ya warheads sema nuclear delivery systems, preemptive strike capability na response. Hawazidiani sana idadi ya makombora na hawahitaji kutumia hata robo yake kumaliza vita.

Vita ya Russia vs USA haipo. NATO vs Russia haipo zitakuwepo operations za kuunga mkono au kumpinga third party
we ni mjenda wa marekani au Urusi, au ni shabiki tu
 
Kuna ndege moja kubwa imedondoshwa mjini Kyiv muda si mrefu, kwa mlio wa engines inaweza kuwa IL-76 airlifter. Sidhani kama itakuwa ni bomber. Kuna uhai bado kwenye air defence ya Ukraine, vigumu kufanya landing bila kuwa na anti access/aerial denial (A2/AD)
CNN inasema kuna Su-27 ya Ukraine imedondoshwa na SAM ya Urusi
 
Hivi unafuatilia haya mapigano. Hilo jeshi la Urusi mnaloliona linatisha mbona silioni? Urusi imepeleka special forces kufanya landing Kyiv mida ya mchana, Ukraine wamefanya counter attack wakiwa surrounded na Russia ameperform very poor. Nakwambia Urusi angekuwa amevamia Poland hapa tungekuwa tunashangaa
Unam- underrate sana Russia, nadhani movie za kimarekani zimekufanya uwe hivyo.

Yani Poland ilete ubabe kwa Russia?? Hivi hiyo nchi mnaichukuliaje kijeshi??

Uzuri ni kwamba wewe upo nyuma ya keyboard na wala hujui chochote kuhusu vita, wamarekani na wababe wenzie wanatambua Russia ni nani.
 
Back
Top Bottom