Marekani hahitaji kutumia reserve kuuza mafuta hivyo hawezi ishiwa reserve. Reserve ni kwa ajili yake tu, uzalishaji kwenye rigs zake ndio hutegemea demand kwenye soko la dunia. Na bado hazalishi sana kuuza mpaka vita hii ilipoanza ndio akaanza kuongeza mauzo nje. Marekani kwa sasa ndio mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani na anaweza toa hata mapipa milioni 15 kwa siku ila uzalishaji wake huwa ni wa gharama kubwa kuliko nchi kama Saudi Arabia ambayo mafuta yake hayatumii nguvu kuyapata wala kuyasafisha.
Ili Marekani azalishe sana anahitaji kujiandaa kwa mitambo na aingie gharama ambazo zinakuwa breakeven kwa miezi au miaka kadhaa. Hivyo ni risk kwake kuongeza uzalishaji kila bei ya mafuta inavyopanda. Yani huwezi mwambia Bakhressa ajenge kiwanda cha unga kingine kisa msimu huu mahindi yamezalishwa mara tatu yake, msimu ukiisha itakuaje atakuwa karudisha gharama za uwekezaji, au kuna demand itakuwepo baada ya huu msimu?
Na Marekani wakati mwingine anatumia fracking technology ambayo ni expensive ila anayo yeye tu ili nchi za kiherehere kama Saudi zikimbania mafuta asikome. Sasa OPEC+ kwa kawaida yao hucheza na soko la dunia, hawataki bei ya mafuta ishuke hivyo hulazimisha wazalishe kidogo kutengeneza uhitaji ili bei ipande. Wakizalisha sana wanatengeneza ziada ambayo itashusha bei. Ila kuna nchi kama Iran na Venezuela zinaweza ingia mikataba kinyume nao, na kulingana na taarifa hiyo ni kwamba Russia na Saudi tu ndio wamekubaliana labda wasubiri mkutano mwingine wa OPEC+ maana wao ndio wana kauli kubwa.
Wala India haiwezi kuwa hub leo au kesho. Viwanda hawajengi tu kisa kuna crisis mwaka mmoja, kuna uncertainties nyingi zinazingatiwa na lazima India iwe na conducive environment kuliko nchi nyingine. Mafuta ya dezo ya msimu mmoja hayawezi wafanya kina Pfizer na Moderna wakajenge factories India. Hata hii China wazungu na Wamarekani wanapenda sana wahame ila wataenda wapi? Nchi zinazokaribia ni India, Vietnam na Mexico ila hazina competent labour, usafirishaji wa uhakika na gharama nafuu (China ndio inaongoza duniani), internal market, n.k. Hapo kwa kiasi fulani China anafaidika yeye tu.
Uzalishaji wa Ulaya utapungua na hii ni crisis wanapitia ila wakitoka hapa Russia asahau kuwauzia gesi na mafuta. India na China zitaendelea kununua at discounted prices zipige hela, waliokuwa na vikwazo kama Venezuela na Iran watapewa fungulia mbwa wazalishe mafuta mengi, lobbying zitafanyika mafuta yawepo tu huwezi sumbua EU na Marekani kwenye nishati wakakosa namna ya kukuzunguka. Oil crisis ya early 1970s ilikuwa kubwa zaidi ya hii ila Marekani alivyotoka hapo alibadilisha mifumo mingi duniani.
Mambo sio mepesi ila ni magumu