Mjadala wa elimu ni mjadala mgumu sana na huongozwa nadharia kadhaa . Kwanza yatupasa kujua elimu sahihi ni ipi kinyume na kile kinachodhaniwa ni elimu.
1. Ipo elimu anayotaka msomaji
2. Ipo elimu inayotakiwa na jamii
3.Ipo elimu kwa ajili ya kuendeleza elimu yenyewe.
Unapoipima elimu kama ni bora
1. Wapo wanasema elimu ni bora pale inapo saidia kutatua changamoto ya jamii
2,Wapo wanaosema elimu bora
ni uwezo wa aliyesoma kutenda
kama alivojifunza
3. Wengine wanaona elimu bora haina mipaka ya kijamii yaani msomaji akijaribiwa katika jamii yoyote aweze kujibu maswali ya fani yake . Hii ni elimu kwa ajili ya elimu fani ama taaluma yenyewe
4.Wapo waliovurugwa wanasema elimu sahihi haitambuliki na ni vigumu kuitambua . Hawa wamevurugwa.
Tukija kwenye taasisi za elimu ambazo ni pamoja na vyuo navyo vitaingia katika misingi ya nadharia na vigezo kadhaa
Baadhi ya vigezo
1. Quality ya wahadhiri na idadi
2. Elimu ya vitendo
3. Kazi za kutafiti
4. Mchango wa wahitimu katika jamii. na mengineyo
Ni kama tu hapa Tanzania unaweza kuta mwanachuo wa Ustawi wa jamii ama CBE akijiunga masters UDSM atapata shida sana na atadhihirika tu japo anaweza kuwa na GPA kubwa kuliko mwenziwe aliyehitimu SUA ama IFM ama UDSM. Lakini linapokuja swala la interview ya KAZI huyu anakua bora zaidi kwakuwa amesomea KAZI zaidi ya hawa waliosoma kwa manufaa ya taaluma zaidi.
Kila nchi ina vyuo vya aina zote hizi. Vipo vyuo vya USA haviaminiki kabisa kadhalika Russia na Kwingineko. Na vipo vyuo vinaaminika na kuheshimika sana. Lakini vyote ni vyuo. Vyuo hutoa taaluma . Vyuo havifundishi tabia . Mwanachuo anachangamana na jamii pana sio mwanafunzi wa Primary.
Zipo nchi zinaaminika kwa taaluma fulani fulani mfano uhasibu na mambo ya IT , Uganga , Ulinzi , electronics nk. Sisikii sana vyuo vya Japan lakini wajapani wapo vizuri baadhi ya sector.
Cuba , RUssia hata India wanajulikana kwenye elimu ya Uganga na tiba. .
Haya mambo ya elimu ubishi wake hauna hauna mwisho . Hata mimi naungana na wanaosema elimu bora haijulikani na ni vigumu kuitambua.
Sent from my TECNO RC6 using
JamiiForums mobile app