Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Kikao cha baraza la usalama kimemalizika.

Raisi Putin ametoa kauli kwamba endapo Ukraine watafanya tena mashambulizi yoyote ya kigaidi ndani ya shirikisho la Russia, majibu yake yatakuwa ni makali zaidi.

Taarifa zaidi ya kauli hiyo ya Putini kufuata.
 
Ndo keshatangaza kupeleka watu ukraine...

Atatengeneza false flag
 
Hii habari ya Belarus kutangaza vita na Ukraine sijaiona kwenye chanzo chochote Cha habari, sijui comred kaiokota wapi[emoji848]

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Ukiona Lukashenko katangaza vita ujue pressure aliyopewa na Putin ni kubwa mno. Hata hivyo bado ni risk kwa Putin kulazimisha Belarus iingie vitani. Hapo anahatarisha serikali ya Lukashenko iliyoko rehani ambayo Putin mwenyewe ndio anailinda. Kupotea kwa Luka linakuwa pigo kwa Putin. Watafanya calculations zao vizuri ila makosa yapo. Mbona hata kabla ya hii vita intelligence service ya Russia ilimhakikishia Putin kwamba Ukraine ni wanyonge na watajisalimisha kama walivyofanya Crimea
 
Serikali ya Moldova imemuita mara moja balozi wa Russia nchini humo kujibu masuali kwanini Russia imetumia anga lake kupitisha makombora matatu kati ya makombora yalokwenda kupiga miji ya Lviv, Ternopil na Zhytomoyr kutokea bahari nyeusi.

Wakati huohuo jengo la ubalozi wa Ujerumani mjini Kyiv nao haukuachwa na mashambulizi ya makombora ya Russia kwani yadaiwa kuwa baadhi ya shughuli za Ukraine zafanywa humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…