Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

@ulimi waupanga

Tunaomba MKUU ukija uje kwa data na ustaarabu kama huu tujengeane hoja kwa hoja

Ila kama hujaelewa hapa sifikirii kama utaelewa tena
 
Yes bro! Wala hakukua, hakuna na hakutakuwa na uzito juu ya kusema hilo neno "samahani" maana halikuwa lengo langu vile ulivyo nitafsiri kwamba nakutusi ama kuku-kejeri.


Naam bro! [emoji4]


Pa1 bro! [emoji2772][emoji41]
Bro mie niulize maswali machache! Moja: unafikiri kwa mawazo yako kati ya USA na Russia ni nani ananufaika/ atanufaika na soko la Ulaya la Gesi? Mbili: Unafikiri nafasi ya USA aliyokuwa nayo ya kuendesha shughuli za kijeshi ndani ya Ukraine kabla ya uvamizi wa Russia imepungua au imeongezaka? Tatu; Unafikiri haswa lengo la USA kuweka akiba ya mafuta ni kutumia yeye mwenyewe au kuyauza na kutawala soko endapo wazalishaji wengine watakuwa hawazalishi? Mwisho; Kabla ya Vita hii na sasa soko la Siraha la USA limepanda au limeshuka?
 
Ingewezekana akawezeshwa kujua kwamba kuendana na mifumo ya jeshi ,tecnolojia na mfumo wa adui KILA line inakuwa na component kadhaa ..Sijajua hizo line ni zenye kufanana ama KILA line na uimara wake ILA line two inategemewa kuwa ngangari zaidi.

VITU vya lazima mahandaki ya depth tofauti, mabomu ya ardhi I
artillery units na airl difference plus command post. Na kuwa na ASKARI wa aina tofauti snipers makomandoo . Kwaiyo line MOJA inaweza kuwa kikosi KIMOJA 1000 + au vikosi kadhaa kutegemea geographia na technology. SASA sijajua kuna distance gani Kati ya line MOJA na nyingine
 
Wajuvi mtusaidie hii ishu hapa ina faida gani na hasara gani kwa RUSSO

Na imewekwa kwajili gani ama malengo yapi hasa !!?

T14 Armata
Qibsyl
Jesus Mlokozi
Galip Vrl
Mr Tyang
Nawengine woooote
Kursk ni oblast muhimu kwenye ulinzi wa Urusi. Hata kwenye WW2 kulitokea Battle of Kursk na ndio ilikuwa decisive kufanya Ujerumani ibadilishe vita kutoka kuwa offensive na kuwa defensive. Vifo vingi sana vilitokea na silaha za kutosha zilitumika.
Ni kama 150km kutoka mpaka wa Ukraine, kama wanaweka third line of defense sio mbaya maana eneo linazungukwa na mito kadhaa ambayo si rahisi kuvuka riverbanks bila maandalizi yatakayoonekana kwa adui. Kwahiyo labda kwa sura ya nchi ya Urusi, maofisa wa jeshi wanaona ili ufanye sweeping movement sehemu isiyo na vikwazo vya kijiografia kupita ni Kursk. Hizo lines za mwanzo tufanye zishaanguka.

Ukitoka Kursk unakuwa na urahisi wa kufanya pincer movement kuelekea Moscow kama Wajerumani walivyofanya na direction moja ikaelekea Stalingrad. Hapo unaona kama Kurks itaanguka unamkaribisha adui deep within Russia.

Defensive lines hata hivyo zinakwepeka kwa kutumia maamuzi magumu na ya gharama. France ilijenga Maginot Line kwa gharama kubwa kulinda mpaka wake dhidi ya Ujerumani ila Ujerumani ikaivamia Poland ikapita uko kuingia France na pia ikapita misitu ambayo France haikutarajia kabisa. Hata Israel ilivamiwa na Egypt kirahisi baada ya Wamisri kujaza mainjinia wa kijeshi kubomoa defence line hasa ya mchanga pale kwenye bank ya Suez, Wayahudi waliita Bar Lev Line.

Hata hivyo defensive lines hazizuii adui ila zinamchelewesha wakati mnajipanga kukusanya reinforcements na kujiandaa kisaikolojia. Na wakati huo zinamchosha adui, na kama hana assault breachers na mainjinia wa kutosha. Adui akija haraka inavunja sana moyo walinzi.

Nchi ambayo inawaza kuvamiwa ndio huweka defensive lines. Hutokaa usikie Marekani imefanya hivyo maana haijawahi waza kama itavamiwa kwenye ardhi yake. Na sidhani kama kuna nchi dunia hii inawaza kuivamia Marekani kwake. Urusi ina landmass kubwa na ina mipaka ya ardhi mingi. Marekani inahitaji kuelewana na Canada na Mexico kuzuia adui, Urusi inahitaji nchi jirani kibao.
 
Umeenda vizuri kasoro hapo pa kujenga kituo
 
Nchi ambayo inawaza kuvamiwa ndio huweka defensive lines. Hutokaa usikie Marekani imefanya hivyo maana haijawahi waza kama itavamiwa kwenye ardhi yake. Na sidhani kama kuna nchi dunia hii inawaza kuivamia Marekani kwake. Urusi ina landmass kubwa na ina mipaka ya ardhi mingi. Marekani inahitaji kuelewana na Canada na Mexico kuzuia adui, Urusi inahitaji nchi jirani kibao.

Kwamba Marekani haiwazi kuvamiwa,aisee kwa kweli hii ndio naisikia Sasa hivi.Ila hapa umetupiga changa la macho.

Jibu ni kwamba,Marekani inawaza sana kuvamiwa na Urusi,china,na Korea Kaskazini.

Sidhani kama Kuna nchi duniani inawaza kuivamia Marekani,aisee hauko siriasi kwa kweli.

Urusi iliwahi Hadi kutoa ramani ya maeneo ya kupiga hapo Marekani.
Nchi nyingine zinazowaza kuivamia Marekani ni China na Korea Kaskazini.
Bila kusahau mgogoro wa Cuba.
 
Ahsante MKUU
 
Mie nataka kuuliza ama kujua moja tu US silaha kule UKRAINE anauza ama anatoa msaada(mkopo)

Kama sirikali ya KIEV inasema wazi kama haiwezi jiendesha endapo watakosa misaada tokea huko EU

Unahisi US na wenzie hapo KIEV wanauza ama !!!??
 
Ukiingia mzozo wa kijeshi na Amerika, nchi alizoweka kambi zake ni kuwatangazia kitakachotua kwenu ni nuclear tu!

Amerika silaha inayomfaa ni nuclear tu!
 
Shukran sana MKUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…