Russia mimi binafsi nilikuwa naamini hajatumia hata 20% ya jeshi lake sijui comment gani humu niliweka last week. Hata silaha zake ni outdated zaidi, silaha nyingi mpya ziko kwakwe uko ni hasara kufanya silaha zako latest zikamatwe kizembe. Nilikuwa najiuliza kwanini wanaokamatwa ni wadogo kiumri nikapata wanaojitetea wakikamatwa wanaonekana pia wapo conscripts wengi.
Hayo yote yanatokea kwa sababu niliyokwishasema wiki ya kwanza ya operation, Russia alikuja na jeshi kubwa na silaha nyingi kutishia Ukraine ikate tamaa ijisalimishe. Warusi waliamini kilichotokea Crimea wanajeshi wa Ukraine kujisalimisha, kuacha silaha na makamanda wengine kujiunga na jeshi la Urusi litatokea tena. Ndio maana siku chache baada ya assault yao kuwa repeled Putin aliomba wanajeshi wa Ukraine wampindue Zelensky, hakutegemea resistance na supply hakuwa nayo wala hakuwa na wanajeshi wa kupigana aliwapeleka watishie kwa show of force.
Wakati Ukraine ilipompata Zelensky asiye na washirika wa kutaka wapewe upendeleo akafuta uongozi wa nchi na kurekebisha uongozi wa jeshi.
Makamanda waliopigana na Russia mwaka 2014 karibia wote walisoma kwenye jeshi la Soviet Union hivyo walisoma na makamanda wavamizi wa Urusi na waliwahi kaa Urusi kwenye mizunguko ya kijeshi, kumbuka USSR imevunjika miaka 31 iliyopita. Within Ukrainian military kulikuwa na Russian symphathizers wenye Soviet nostalgia wengi ambao hawakupigana wala wasingepigana mwaka huu. Zelensky alitoa maofisa wenye tabia za Kisovieti (fuatilia tofauti ya wanajeshi wa Tanzania waliosomea Russia vs waliosomea NATO countries tabia zao) akaweka walio neutral au wamesoma Western. Nishasema humuhumu tafuta kwanini jeshi la Ukraine liliongozwa na Lieutenant General Valery Zaluzhny aliyepandishwa cheo kuwa General jana Jumamosi na Rais Zelensky. General Zaluzhny ana miaka 48 tu! Nilisema kuhusu alivyopigana frontline tangu 2014, kakaa sana field huyo hata mpaka vyeo ilikuwa ngumu kumpandisha haraka.
Haya mambo hayaitaji uyajue siku vyombo vya habari vinavyoyakazania. Nimeanza ufatilia mgogoro wa Ukraine since 2014 na huyu Zaluzhny kipindi bado mdogo jeshini hana vyeo, ni graduate wa 2007 kwenye military academy. Nimetazama sana documentaries zao, propaganda za Russia, mchafuko wa kisiasa ndani ya Ukraine. Leo hii anatokea mtu ambaye sijui kaijua Ukraine mwezi wa pili, ana matusi na hana hoja anasema ninalishwa propaganda za Westerns.