Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Marekani yaendelea kumiminisha vifurushi vya silaha

$400M additional US assistance for Ukraine will be advantageous both for defense and for the liberation of Ukrainian lands.
Modern equipment + a modern #UAarmy will defeat soviet scrap metal + murderers, rapists & looters.
Thank you to POTUS @SecDef and the American people.

 
Russia mwameelezea tactical reasons za kusogea pembeni.

Kijeshi imeeleweka ila kwa wanazi wanaassume wameshinda vita.

Vita ina moves nyingi.

Let’s see
Nilijua Putin atafanya ziara Kherson kama wenzake wa NATO wanavyofanya ziara Kyiv kumbe wapi. Ila angefanya ziara kisha leo hii wanakimbia eneo hilo ingekuwa mbaya zaidi
 
Sera za Brussels dhidi ya Moscow zimeharibu uchumi wa EU "vibaya sana," Budapest imesema.

Vikwazo dhidi ya Urusi havijafikia malengo yoyote yaliyotajwa na Umoja wa Ulaya na vimerudi nyuma kwa kuumiza uchumi wa nchi wanachama, Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary Peter Szijjarto amesema.

EU, pamoja na Marekani na nchi nyingine kadhaa, ziliweka vikwazo vikali dhidi ya Moscow katika kukabiliana na operesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine, ambayo ilizinduliwa Februari.

"Vikwazo ambavyo vimeanzishwa na Umoja wa Ulaya [dhidi ya] Urusi vimeshindwa. Ni kushindwa kabisa," Szijjarto aliambia Roya News ya Jordan Jumapili.

Ilisemekana na Tume ya Ulaya kwamba vikwazo vitatusaidia kumaliza vita hivi haraka iwezekanavyo na kwamba vitaleta uchumi wa Urusi kwenye magoti yake. Nini matokeo? Ni kinyume kabisa.

"Vita vinazidi kuwa vya kikatili ... na, wakati huo huo, uchumi wa Ulaya unateseka vibaya sana," Szijjarto alisema, akiongeza kuwa bara limekumbwa na "shida kubwa ya nishati," pamoja na mfumuko wa bei na kuongezeka. bei za vyakula.

Waziri huyo alisema kuwa Hungary ililipa €7 bilioni ($ 6.9 bilioni) kwa uagizaji wa nishati mnamo 2021, lakini inapaswa kulipa € 19 bilioni ($ 18.9 bilioni) mwaka huu. "Hilo ni kubwa. Na haya ni matokeo ya sera ya vikwazo iliyofeli."

Szijjarto alisema kuwa, badala ya vikwazo vya kiuchumi, EU inapaswa kuzingatia kufikia amani katika eneo hilo. Alisema kuwa suluhu nchini Ukraine inaweza kuja kama matokeo ya mazungumzo kati ya Urusi na Marekani.

"Kimsingi, ni sisi pekee barani Ulaya ambao tunabishana kwa ajili ya amani," alisema. Waziri huyo wa mambo ya nje alitetea uamuzi wa Hungary wa kukataa wito wa kyiv wa kutuma silaha na kutoshiriki katika mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine. Hatua hizi "zinachangia kuongezeka" badala ya kusaidia kumaliza mzozo, alisema.

Uchumi wa Hungary unategemea sana nishati ya Urusi, na serikali imepinga mipango ya Brussels ya kupiga marufuku kabisa uagizaji wa mafuta na gesi kutoka Moscow. Baada ya mazungumzo magumu, Budapest ilipokea misamaha kadhaa kutoka kwa vizuizi vya kambi nzima juu ya ununuzi wa mafuta ya Urusi.

Hungary ilisema wiki hii kwamba haitaunga mkono kifurushi cha mkopo cha pamoja cha EU, ambacho kitatenga euro bilioni 18 ($ 17.9 bilioni) kwa msaada kwa Kyiv.
 
Ni noma, na madai ni kuwa watu waliokufa ni wengi
 
Russia hana tishio la kivita, anapigana amerelax.

NATO wanajua hili, ndo maana hawawez mpa Ukraine silaha za kishambulia Moscow na miji Mikubwa.

Wanajua kitakachotokea
Kwa kujipa matumaini kiasi hiki hata baada ya Russia kushindwa vibaya hii vita, mlipaswa mfanye kazi ICU kuwatia wagonjwa moyo walio katika hatua za mwisho za uhai wao.
 
Hii game warusi tumepigwa. Tungeimaliza mapema kwa kuingia full force ila sijui ni huruma na diplomasia za kishamba zilifanya Ukraine na washirika kujipanga. Hatuwawezi tena. Putin hakuwa na mipango ya kueleweka kuhisu nini anapaswa kufanya na nini anataka ndani ya hii vita. Hakuwa na sera ya kueleweka.
Wengi tuliamini angeweza kutokana na mifano ya Syria ila nadhani Syria alishinda kwa kuwa US hakuwa na watu sahihi wa kushirikiana nao taarifa za intelligence na recon. Leo US ana assets kibao za ISR kwenye anga nje kidogo ya Ukraine ambazo kisheria Urusi hawezi kuzishambulia kwa sababu haziko ndani ya eneo la vita japo zinafanya op kumsaidia Ukraine.

Ndege kama P-8, RC-135V/W, E-8 nk zinakusanya taarifa zote battlefield anapewa Ukraine so Ukraine anakuwa anajua kila kinachoendelea uwanja wa vita so anapopanga mashambulizi ndo maana mengi yanafanikiwa. Taarifa kama hizi US asingewapa waasi wa Syria kwa sababu sio taasisi iliyokuwa inaaminika inaweza kuongoza nchi so US kuwaamini na taarifa sensitive kama hizo.

Urusi alipaswa kuipeleka fasta hii battle kabla hawa jamaa hawajajipanga ila kwa kinachoendelea ni kama alikuwa anawapa nafasi wajipange. Hizi ni nchi zaidi ya 30 zenye uwezo mkubwa kijeshi na kiuchumi so huwezi kutegemea kama watakosa dawa ya kukudhibiti unapokuwa na mipango ya vita isiyoeleweka.

Putin katuangusha. Sichangii tena humu ntakuwa napita kusoma michango ya watu
 
Kwa kujipa matumaini kiasi hiki hata baada ya Russia kushindwa vibaya hii vita, mlipaswa mfanye kazi ICU kuwatia wagonjwa moyo walio katika hatua za mwisho za uhai wao.
Mkuu mambo vp? Kwa yaliyotokea, Embu niambie umeyaelewa malengo ya Russia? Anataka nini? Ni kwann hakupeleka drones kherson badala yake akaharibu miundombinu nje ya eneo wanajeshi wake wanaposhambuliwa? Halafu ni kwann Ukraine hapewi misaada ya kuweza kulipiza kisasi ndani ya Urusi?
 
[emoji298]️In Poland, a new section of a metal fence was built on the border with Belarus, which should reduce the risk of illegal crossing of the border between the two states, - said Stanislav Zharyn,
Inasikitisha saana
 

Tangu siku ya kwanza sikuwahi kuelewa Putin na siyo Russia anataka nini Ukraine na nina uhakika hata wengi waliopo Kremlin sidhani kama na wao wanamwelewa,rejea ushauri wa yule Kamanda kabla ya hii vita na jinsi alivyomblast kwa hasira baada ya kutopenda alichoshauliwa.Hii vita inapiganwa tu blindly kutegemea na Bwana Putin siku hiyo anataka nini otherwise asingekuwa anahangaika kila mara kubadilisha hata makamanda wanaoendesha hii operation.

Ukraine anapokea msaada kulingana na uhitaji wa wakati huo,utakubaliana na mimi kuwa misaada iliyotolewa March to June si sawa na inayotolewa sasa hivi.Hapa tumshangae zaidi Putin maana ndiyo kiumbe pekee anaejua nini anakitaka Ukraine.
 
Me nadhani si huruma Ila Russia alifanya kosa la kum-underestimate adui yake na hili kosa ndo lililomgharimu mpaka kuja kushtuka kashachelewa wakati huo adui yake akaongezewa misaada. Kumbuka hata Marekani na washirika wake hawakutarajia kilichotokea CIA ilisema Ukraine itaanguka ndani ya wiki mbili-tatu na kwamba Russia itakua imeshalimaliza jeshi la Ukraine. Putin nae kwa mbwembwe akaja kwenye TV akatangaza wanajeshi wa Ukraine waweke silaha chini na wampindue Rais wao sababu kama wakiendelea kupigana warusi hawatakua na huruma kwao.

Ujue baada ya kilichotokea Afghanistan ile Marekani kuondoka tu,Taleban wakakamata nchi fasta baada ya wanajeshi wa Afghan kukimbia na zana zinyi za Marekani kudakwa,Marekani ilikua inasita kuipa Ukraine zana zake nzuri nzuri kidogo wakihofia zitakamatwa na warusi lakini kama ulifatilia mwanzoni baada ya Majeshi ya Urusi kushindwa kuiteka Kiev ndipo misaada ikaanza kumiminika walianza na kupeleka Howitzer M777 ,Himars zikaingia mwezi julai hapo ndipo kivumbi Kwa Russia kikaanza wakaanza kupoteza miji. Na kwa Kasi hii anayoenda nayo Ukraine,Urusi ana kibarua kizito.

"There is no greater danger than underestimating your opponent.”
Sun Tzu, Chinese Military Strategist.
 

alizani ule mkwara wa atakae ingilia hii oparation basi jibu la rusia litakua ni la hapo kwa hapo. tena matokeo yatakua ni haijawahi tokea akajua watamuigopa kama walivyo muachia kule georgea na crimea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…