Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Zaidi ya watu 10 wa Kherson Oblast wamekufa baada ya makombora kudondoka kwenye mji uliotajwa kukombolewa na Ukraine wiki 2 zilizopita.
Urusi iliwataka watu wote waondoke upande wa kulia wa mto Dnipro na hatimae na majeshi yake yakaondoka upande huo ambapo majeshi ya Ukraine yaliingia kwa furaha na kutangaza kuukomboa mji huo.
Dalili za kukosekana kwa usalama mjini humo zilianza mapema wiki hii wakati Serikali ya Ukraine nayo ilipowataka wananchi waliobaki waondoke na kwamba iko tayari kuwalipia gharama zote za kuhama,
Mashambulizi ya Kherson yamekuja siku 3 tu tangu mvua nyengine ya makombora yalipopiga miji yote mikubwa ya Ukraine na kusababisha umeme na maji kukatika katika maeneo hayo.
Mashambulizi hayo vile vile yamekuja siku chache tu tangu waiengereza waliposema Urusi imebakiwa na makombora yanayotosha kupiga Ukraine kwa mfululizo yasiyozidi siku tatu.
Katika hatua nyengine Rais wa Ukraine amesema Urusi hawajui kupigana. Wanachojua ni kupiga watoto na kulipua vinu vya umeme na maji.