Punguza ujuaji usio kuwa na kichwa wala miguu.
Ww hapo unaweza kunitajia bidhaa kutoka Israel, Singapore,Taiwan au Finland ambayo unaitumia kwenye maisha yako?
Lakini hayo mataifa niliyo yataja ni moja wapo wa mataifa yenye teknolojia ya hali ya juu sana ulimwenguni lakini mara nyingi huwa ni kwa ajili ya mahitaji yao ya ndani.
Urusi inatengeneza bidhaa za kila aina sema makampuni yake hayajajitanua na kuwa makubwa, na mara nyingi ili uone bidhaa za Urusi inabidi uende kwenye nchi za Ulaya mashariki ,Asia ya kati na baadhi ya mataifa ya magharibi na hata America ya kusini hizo nchi ndio watumiaji wakubwa wa bidhaa za Urusi na sio razima uzitumie ww kutoka bara la giza.
Hata kwa upande wa mitandao ya kijamii warusi siyo watumiaji sana wa mitandao ya kijamii ya kimagharibi bali wana mitandao ya kijamii ya kwao wanayo itumia, hata mtandao wa Telegram una kutokea Urusi bila shaka hili ulikuwa hulijui.
Alafu kingine unacho takiwa kutambua ni kuwa sio razima kila nchi iwekeze kwenye eneo moja ,,yaani kisa tu Ujerumani na Japan wanewekeza kwenye magari basi na Urusi ikimbilie huko huko?
Nyinyi ndo huwa mnafeli kwenye biashara kwa kuiga biashara za watu bila kujua huyo mtu mpaka anaingia kwenye biashara hiyo amepita njia ipi.