Hujanielewa mkuu, nimetoa mfano wa gunduzi kama kielelezo kwamba technology yao na elimu waliyokuwa nayo ni kubwa na si kuwabeza, sijaja hapa kushindana nani kagundua nani hakugundua, nafikiri umepata point yangu.
Mara nyingi mataifa makubwa katika gunduzi ni suala la kuachana gap la muda tu, lakini hawa wakisikia flani katengeneza hiki na wao wanakuja na gunduzi kama ile au iliyoboreshwa zaidi ili wasiwe nyuma ki technology.
Kwenye suala la sayansi na technology na vumbuzi za kisayansi wenzetu wana ma kachero, huyu anaiba taarifa nyeti za project flani huyu nae anaiba za yule analeta huku ndivyo mambo yanakwenda, thats why mimi sioni China kama ipo weak kujifunza, kuiga na kuboresha hasa military tech kutoka Russia na USA, tazama sasa wapo vizuri sana.
Ndio maana we mwenyewe umeeleza hapo Ukraine walikamata kifaru cha T-90M na NATO wanakichunguza, kuna mazuri watajifunza juu ya hio silaha na kuboresha zao, kuna vitu watakizidi kuna vitu kitawazidi vifaru vyao, baada ya hapo watatangaza vifaru vya T-90M hamna kitu, hakifai, very weak, kumbuka pia hio ni vita ya business/uchumi.
Mfano Russia kuna ndege walirusha 1884 kuna engineer mmoja aliitwa Alexander Fedorovich Mozhaysky, huyo alirusha ndege ikaruka 1884 akidhaminiwa pesa na serikali, miaka 9 baadae nao Wright brothers wakarusha ndege 1903 huko USA ambapo ndio watu wengi tunajua walifanya gunduzi.
Russia 1957 anarusha Sputnik, USA 1958 anarusha Explorer 1, hivyo ndivyo mambo yanaenda.
View attachment 2437656
View attachment 2437658
Watu wengi wanafahamu mgunduzi wa kwanza wa bulb ni Edison, lakini si kweli, kwanza kipindi Thomas Edison anafanya majaribio kuna majaribio zaidi ya 20 yalikuwa yakiendelea sehemu tofauti duniani chini ya scientists tofauti.
Baada ya tu Humphry Davy kugundua the electric light na electric battery, scientists wengi waliamua kuingia kwenye field hio, Edison yupo credited kama mtu wa kwanza kuamua kuweka bulb za umeme sokoni, zilikuwa kwenye beta stage.
1874 Russian engineer Alexander Nikolayevich Lodyginaligundua na kuchukua hatimiliki ya gunduzi ya taa, kabla hata ya Edison.
Wasovieti wana gunduzi nyingi tu za kisayansi na technlogy zilizoleta faida duniani, hatuwezi kaa hapa tunashindana nani wa kwanza nani wa mwisho.
So my point is it doesnt matter nani wa kwanza nani kafuatia, sio kwamba asipogundua huyu dunia itaishi pasipo hio gunduzi kuna watu watatokea tu issue ni muda tu.